NANI Tumkabidhi Nchi yetu ya Tanzania iliyojaa Neema TELE??

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,099
630
Wa Tanzania wenzangu,
Ninajiuliza nani anayefaa kukabidhiwa Nchi ya Tanzania mwaka 2015.

Nchi yetu Tanzania ina kila kitu ambacho Nchi yeyote inakihitaji ili iweze kusonga mbele. Lakini sisi tumeshindwa.! Tatizo ni Viongozi wetu, uzalendo au Elimu yetu? Nini hatuna rasilimali, ardhi, siasa safi, amani, viongozi au nguvukazi? Tatizo liko wapi?????

Swali la mwisho linanijia NANI tumkabidhi Nchi yetu Uchaguzi ujao 2015??
 
Tukirekebesha tukawa na Siasa Safi isiyoongozwa kwa misingi ya Rushwa na Ubaguzi wa aina yoyote ile tunaweza kufanikiwa kupata UONGOZI BORA na tutakapopata uongozi bora itasabisha watanzania wawe katika njia sahihi kuelekea katika mambo yote ya kunufaika na rasilimali zao.
 
Tanzania kuna kila kitu. Au ni laana wakuu?? Hii nchi ilibidi iwe nchi ya Viwanda, Sekta ya Kilimo ndio ilibidi iwe na heshima.

Vijana leo wangekuwa busy na kazi viwandani na kwenye kilimo na biashara ingeshamiri. Lakini hamna kitu.

Au Vijana hatuzioni FURSA??
 
Suala la nchi sio kitu chepesi kama kukabidhiana sinia la pilau kwenye sherehe za hitma na kipaimara...Ni vyema tasnifu yako ikamulika mbali zaidi ya hapo...
 
mwakyembe
sumaye
dk slaa
john pombe makufuri
lowasa
sita

HAPO VIPI ?
NAOMBA MNICHAGULIE MMOJA AWE RAISI
 
Sijaona wa kumwamini hata mmoja mpaka sasa! Wengi ni wachumia tumbo tu, si CCM wala si upinzani.
 
Back
Top Bottom