Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 19,680
- 59,798
Kabla ya wakoloni kuja Africa tuliishi kwa namna yetu. Bahati mbaya historia ya Afrika imepotezwa kwa makusudi au kupotoshwa.
EAST AFRICA COMMUNITY KWA SASA
- The Republic of Burundi
- The Democratic Republic of the Congo
- The Republic of Kenya
- The Republic of Rwanda
- The Republic of South Sudan
- The Republic of Uganda
- The United Republic of Tanzania
- Somalia
- Comoros
- Mozambique
- Sudan
- Ethiopia
- Angola
- Republic of Congo
- Zambia
- Customs Union
- Common Market
- Monetary Union
Tayari Custom Union ilishapitishwa tangu mwaka 2005. Unaweza ukaipitia hapa na kusoma mambo kadha wa kadha Customs
Tayari Common Market ilishasainiwa mwaka 2010 na ilikuwa inatarajiwa kuanza kutumika mwaka December 2015. Kuna mambo kadha wa kadha yalitokea lakini ipo katika hatua za kuanza kutumika. NB: Kama sisi watanzania tutaendelea kulala mabadiliko yatafika na sisi bado tunabishana ndani ya nchi huku wenzetu wakijiandaa kutumia fursa.
Monetary Unioni ilishasainiwa mwaka 30th November 2013. Na ilikuwa inatakiwa ndani ya miaka 10 iweze kuanza kufanyiwa mikakati. Tayari kwa sasa tumo ndani ya miaka hiyo. Huenda baada ya muda hii itawekwa kwenye action.
NINI HATMA YA TANZANIA NA SIASA ZETU?
Tusipowekeza katika human capital na kuendeleza siasa hizi za kizamani, watu wa Tanzania watakuja kuachwa kutokana na fursa zitakazoendelea katika nchi mpya itakayozaliwa. Hili jambo kuna wengine wanaliona kama ndoto. Lakini kutokana na mabadiliko ya siasa za kidunia naliona linaenda kutokea siyo muda mrefu.
Sasa basi viongozi wetu wanawaandaa vipi watanzania kuweza kuingia katika hatua hizo zinazokuja? Itafikia wakati Tanzania itashindwa kuwa na sauti kutokana na kuzidiwa kura na wengine. Maana nchi zinazidi kuwa nyingi na influence ya Tanzania inazidi kupotea.
Tanzania tulikuwa tunaringa kwa kuwa na rasilimali nyingi. Ona sasa kiburi hatuna tena kutokana na jambo hilo maana DRC tayari naye ni member. Tanzania imekuwa nchi ya kawaida tu ndani ya EAC. Kama tutaendelea kuchelewesha mambo haya wenzetu watafanya wao na kutukuta sisi tunaachwa, au wachache wananufaika na mtangamano huu.
Nitaendelea kweka Statistical Data na References ili kufumbuana macho...