Tanzania Kisiwa cha Amani, Kubeba Mkutano wa Wakuu Nchi Zaidi ya 30 za Barani Afrika

Jun 4, 2022
68
184
Na:- Diplomatic Agent

Ni heshima kubwa kwa Taifa la Tanzania, Taifa la Kidemokrasia na lililojipambunua vyema katika masuala Diplomasia Kimataiafa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za zaidi ya 30 za Afrika utakaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 24 - 26 Julai, 2023 utakaojadili kuhusu uwekezaji katika rasilimali watu, chini ya kauli mbiu inayosema “Kuongeza Kasi ya Ukuaji wa Uchumi wa Afrika: Kuongeza Tija kwa Vijana kupitia Kuboresha Mafunzo na Ujuzi.” Mkutano huo utahudhuriwa na
Wajumbe 1,200.

Mkutano huo ume andaliwa na Benki ya Dunia na mwenyeji wa mkutano atakuwa Rais Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN. Viongozi Wakuu wa nchi za Afrika watakaohudhuria Mkutano huo ni:- Marais wa nchi za Benin, Centra Africa,
Ginea Bisau, Kenya, Madagascar, Malawi, Sao Tome, Siera leone
Somalia, Saharaw, Togo,
Zambia, na Zimbabwe.
Makamu wa Marais wa nchi za :Libya, Namibia, South Sudan na Uganda.

Pia, watashiriki Mawaziri Wakuu wa nchi za: Burundi, Cameroon, Eswatin, Cape Verde Ethiopia na Mawaziri kutoka nchi za: Algeria, Angola, Egypt Mozambique na South Africa. Pamoja na balozi wa nchi ya Ivory Coast.

Kwanini Tanzania na siyo nchi nyingine barani Afrika.

Benki ya Dunia imeamua kufanya mkutano huo mkubwa na wa heshima nchini Tanzania kutokana na Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa amani ambapo ajenda muhimu ya rasilimali watu itakayojadiliwa ilihitaji nchi yenye utulivu na watu kusikilizana.

Pia, suala la ajira kwa vijana ambapo azimio la Dar es Salaam litaziwezesha nchi hizo kujifunza kwa Tanzania kupitia mfumo wa vyuo vya VETA na vya ufundi mbalimbali Pamoja na miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa ikiwepo ya SGR na mingine mingi.

Vilevile, uwepo wa vivutio mbalimbali vya Utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ni mioungoni mwa maajabu saba duniani, mlima Kilimanjaro pamoja na visiwa vyenye marashi ya karafuu (Pemba na Unguja) Zanzibar, ambapo Wakuu wa nchi hizo watapata fursa ya kutembelea vivutio vya utalii wakiwa nchini.

My Take

Ni wito wangu kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam pamoja na maeneo ya jirani kutumia fursa hiyo kuweza kukuza mapato yetu na kukuza uchumi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla.

Watanzania ukarimu ni jadi yetu pasi na shaka wageni hao wataondoka nchini wakiwa na taswira nzuri juu wananchi wa Tanzania kwa mapokezi mazuri na yenye bashasha tele.

Idumu Amani na Umoja Wetu
Screenshot_20230724_170041_Adobe Acrobat.jpg
 
View attachment 2697883
Ni jambo jema ila mkataba wa DP World unaitia doa Tanzania.
 
Back
Top Bottom