Nani Rafiki wa Kweli, Nani Mtu Baki?

Jun 14, 2010
63
42
Kuna watu kwao twaitwa marafiki:

Wakifikwa na hitaji la chumvi kwa nadra watapata kutoka kwetu, ila kutoka kwa watu-baki wana hakika ya kupokea sukari!

Wakiugua hawawezi kupokea hata pakiti ya maji kutoka kwetu ilihali kwa watu-baki wanachangiwa hadi damu na kulipiwa ghalama za matibabu!

Mema yakiwafika tunakuwa watu wa mwisho kuwapongeza tena kwa maneno na mikono mitupu huku watu-baki wakishiriki furaha nao kwa hali na mali!

Kwetu wakiomba kanga au suruali wajisitiri tutawajibu hatuna na kuwasimanga lakini mtu-baki atawapa kanga, sketi, blauzi au suruali na shati!

Wakiomba; tukiwapa ushauri au msaada wowote, sisi hugeuza kuwa matangazo tofauti na watu-baki ambao hawawahesabii wala kukumbuka ni kiasi gani wametoa kwa wengine!

Ofisi zao kwetu ni kama zimefungwa maana bora hata tarishi wa ofisi hizo anaweza kutusogezea barua za maombi yetu kuliko wao!

Kwenye shughuli zetu wanataka wapate huduma na bidhaa bure wakati kwao hata kwa hela hatuhudumiwi!

Ni binadamu, hatujakamilika! Katika matukio yote yaliyoelezwa hapo juu lipi limewahi kukufika au umewahi kumtendea mwenzio?

Usiku mwema---Ni Idd Pili Mubaraak!
 
Back
Top Bottom