Rais wangu wote tulishuhudia kujiuzulu kwa Abdallah Natepe, Peter Siyovelwa, Ali Hassan Mwinyi na wengine. Ni kikao gani kilikaa kuwasafisha watu hawa? Mbona mpaka leo wapo safi? Hawakusafishwa kwa sababu wao wenyewe hawakuchafuka.
Walijiuzulu ili kulinda ustaarabu. Walijiuzulu bila kuchafuka wangesafishwa vipi? Huwezi kupungwa mapepo kama huna mapepo. Lakini kama una mapepo, hata upungwe vipi alama ya mapepo itabaki juu yako.
Inasikitisha kuona watu wazima wanaficha maiti chumbani kwa kuipulizia marashi. Inasikitisha zaidi tunapotaarifiwa kuwa, kusafishwa huko kunakuja huku kukiwa na wingu zito la tuhuma za rushwa, ushirikina, vitisho na hata ulaghai uliogubika mikakati ya kuhakikisha watuhumiwa wote wa ufisadi wanasafishwa.
Wana jf....Kumekuwa na msururu wa threads mpaka sasa hujui nini ni nini na wapi ni wapi!
Kunaonekana kuna MVUTANO MKUBWA!
Ni wazi kuwa KESI IMELETWA JF!
Sasa ili wananchi wanaofuatilia mijadala hii wasichanganyikiwe...Basi sasa MIMI NIKO RADHI KUSEMA KUWA...Huu ni muda wa kuangalia ni nani safi na ni nani si safi!
Kuna Mpango mahsusi kabisa wa kujaribu kumchafua MWAKYEMBE.
Kwasababu sasa tunajuwa stories zote za EPA NA RICHMOND..ECT ECT...
Ni vizuri tukaanza kutaja majina ya watu ambao kisheria wanatakiwa mahakamani.
Pia kwa wale watakaoleta siasa...Then na sisi tutawaonyesha ni kwanini na wao wameguswa na UFISADI.
Kwa kuanzia...NASEMA MWAKYEMBE NI SAFI...Baada ya hapo...Nitaendeleza kutaja wengine walio safi na wale CHAFU!
Mkuu,
Nilitegemea kuona watu tunaendeleza kampeni kuhakikisha wale wote wanaotuhumiwa kuhusika na kashfa zote hizo wanaikabili sheria na kuona mwisho wake.
Lakini hili jambo linaitwa "spinning" ndilo nilionalo linajaribu kujipenyeza kwa nguvu.
Lengo kuu la spinning ni kupoteza lengo kwa public kwa kuwa-manipulate na vijihabari mbuzi na midubwana mingine isiyo kichwa wala mkia.
Watu wanajaribu kuongelea kuhusu Mwakyembe huku wakiwapa nafasi watuhumiwa wajisafishe majimboni kwao .
Kama ni hivyo nami ntakuwa nalifuatilia.
TATIZO NI KUNA MAMLUKI KUTOKA BOTH ccm na chadema wanaovuruga mijadala ya upinzania kwa maslahi yao binafsi!
Wananchi kama mnataka tuwatajie nani ni safi na nani si safi tutafanya hivyo!
maana hapa kuna vita kati ya watu binafsi ndani ya vyama vyao!
HAKUNA ATAKAYE CHAGUA VYAMA...WANANCHI WATAWACHAGUA WAZALENDO!
NINGEPENDELEA HOJA YA MGOMBEA BINAFSI IPEWE KIPAUMBELE AMA ULE MUUNGANO ALIOUTANGAZA MTIKILA AMBAO UNADHAMIRIA KUFUNGUA KESI YA EPA!
HAO NDIO WA KUSIKILIZWA! NA SI MAMBO YA VYAMA!