Nani mbabe: Black Mamba vs King Cobra

Kuna kitu tuna changanya, kuna Cobra na king cobra hivi ni vitu viwili tofauti japo vina shabiiana kwa namna fulani.
Africa hatuna king cobra, tuna cobra tu.
King cobra wapo Asia tu, na ndo nyoka mwenye umbo na urefu mkubwa kwenye kundi la nyoka wenye sumu.
King cobra aliyekomaa ana urefu hadi ft 13/14..
Sasa fikiria kitu chenye urefu huo kisimame mbele yako, kinakuwa kinakutazama kama katoto.

Kwenye battle ya king cobra na black mamba, king cobra anamaliza pambano kwa sekunde kadhaa.
Cobra hata kwetu kijijini wanauawa sana.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Kuna kitu tuna changanya, kuna Cobra na king cobra hivi ni vitu viwili tofauti japo vina shabiiana kwa namna fulani.
Africa hatuna king cobra, tuna cobra tu.
King cobra wapo Asia tu, na ndo nyoka mwenye umbo na urefu mkubwa kwenye kundi la nyoka wenye sumu.
King cobra aliyekomaa ana urefu hadi ft 13/14..
Sasa fikiria kitu chenye urefu huo kisimame mbele yako, kinakuwa kinakutazama kama katoto.

Kwenye battle ya king cobra na black mamba, king cobra anamaliza pambano kwa sekunde kadhaa.
Nakazia
images-72.jpg
 
Mkuu usije ukajichanganya na black mamba. Hawa sumu yao ni deadly sana! Be careful. Cobra most of the time anatema mate, na mate yake ni hatari zaidi yakikufikia machoni. Ukiwahi kunawa kwa maji mengi na sabuni asilimia za kupona ni kubwa na hautapofuka. Black mamba akikugonga usikawie zaidi ya nusu saa (nadhani ni dakika 20) bila kufika hospitali UTAKUFA! Usione hizo mils 55 ukazidharau, ni hatari sana kuliko 400 za cobra

Nimekuonya!
Ukiwa mtu pori first aid kit ni muhimu ukigongwa unajitibu fasta
 
Nimetazama video clip za Wazigua wakicheza na nyoka hatari duniani
Black Mamba na Green Mamba sikuweza kuamini haya yanayokea nchini na hatuyajui

Mzungu ametetemeka mpaka goosebumps hakuamini watu wanacheza na nyoka hatari duniani

I wish siku moja nitimize na mimi ndoto to dance with koboko
IMG_3158.jpg

IMG_3156.jpg
 
Utakuwa humjui black mamba,
nyoka wote unaweza kucheza nao ila sio black mamba,
hanaga urafiki kabisa,
akihisi kwamba yoyote ameingia kwenye territory yake,
hakikisho la kwanza ni kukusaka hadi akupate mmalizane kwanza ndio mambo mengine yaendelee
Hakika
 
Hebu tujaribu kidogo kuwachambua hawa wababe wawili kisha tujue ikiwa watakutana nani atakuwa zaidi??

Black mamba na King cobra ni moja ya jamii hatari zaidi za nyoka duniani na maarufu hata kimuonekano kutokana na upekee wa maumbo yao.

BLACK MAMBA: Nyoka anayejulikana kwa kuua sana duniani na mwenye kasi zaidi kuliko nyoka wote ardhini.
  • Makabila mbalimbali ya kiafrika yanatumia utambulisho wake kama alama zao na wengine kumuabudu kama mlinzi na mungu wao katika maeneo yao.
  • Ameripotiwa kusababisa vifo vya maelfu ya watu kila mwaka.
  • Wakorofi na wako tayari kung'ata mara nyingi iwezekanavyo pale inapombidi kufanya hivyo kutokana na tishio la adui.
  • Kwa sababu hii wanahesabika kama TOP KILLER kati ya nyoka wote wanaotambaa ardhini. Karibia watu 20,000 kila mwaka wanakufa kwa kugongwa na nyoka huyu.
  • Wanapatikana zaidi hasa Afrika maeneo ya central na east Afrika.
UREFU
-Kwa black mamba aliyekuwa na kukomaa anaweza fikia urefu wa 6.6 - 8.2 feet (2 - 2.5m)

-Urefu wa meno ni 0.25 inches (6.5mm)

SPEED/KASI

-12.5 m/h (20km/h). Mara nyingi hutumia kasi yake kukimbia hatari kuliko kuwindia.

UZITO

-1.6 Kg

MUONEKANO NA RANGI

Black mamba huwa warefu pia wembamba. Wanapatikana kwa rangi ya kijivu au brown mbichi (light brown)

CHAKULA/DIET

• Wanyama wadogo na ndege.
*Imewahi kulipotiwa kukutwa kasuku wazima na hata Cobra wakubwa kwenye tumbo la Black mamba.

ATTACK NA UWINDAJI

- Wanapopata windo husubiri kwanza windo lake kuparalyze au kufa kutokana na sumu aliyowatia kupitia meno yake, ndipo huwa muda mahususi kwa kumla.
-Kawaida huchukua muda mchache sana kwa windo lake kufa baada ya kung'atwa na humeza windo lake kama lilivyo.
- Wana taya laini kujitegua ili kufit chakula mdomoni hata mara 4 ya saizi ya kichwa chake.

TABIA

• Ni wakazi wa eneo moja. Wanatoka asubuhi na baadae tena jioni kwa ajili ya kuwinda ama kupumzika nje kisha kurudi eneo lao.
• Ni waoga lakini hurudisha attack pale inapowalazimu na kukimbilia katika kichaka au shimo .

KING COBRA: Ni kati ya nyoka wakubwa na hatari zaidi duniani. King cobra hupatikana hasa Southeast Asia na India
  • Anapokutana na tishio hutumia ngozi yake karibu na kichwa kuitanua ili kuinekana hatari. Alama nyeusi nyeusi zilizopo katika hood yake hutishia baadhi ya wanyama wakali wanapokuwa karibu nae.
• Anauwezo wa kunyanyua 3/4 ya mwili wake toka ardhini huku kumfuata adui yake kwa lengo moja tu ( kuattack).

UREFU

-10 to 12 feet (3.3m) lakini wengine wanaweza kufikia mpaka 5.4 m.

UZITO

- 6Kg.

RANGI NA MUONEKANO

-King cobra waliokomaa wapo wa rangi nyeusi, light yellow, kijani na brown. King cobra ni mnene kidogo kuliko black mamba.

CHAKULA/DIET

-King cobra wanajulikana kama '' OPHIOPHAGONS" yaani snake eater. Anauwezo wa kula hata nyoka wenzake wenye sumu.
- Mlo pendwa ni pamoja na jamii za panya, mijusi, ndege na hata nyoka wengine kama chatu, cobra, jamii za vipers n.k.
-Mlo unapopatikana vizuri anaweza kukaa hata mwezi kutokana na mmeng'enyo chakula wake wa taratibu.

ATTACK NA UWINDAJI

-Anawinda kwa kutumia kemikali inayogundua haruru ya windo lilipo hata zaidi ya umbali wa mita 100 toka alipo.
- Sumu yake hatari inaweza kumpa paralyze na kumuua kabisa tembo ndani ya masaa 3 tu toka amng'ate iwe mguuni au kwenye mkonga.

TABIA

- Hawana eneo maalumu kuishi.
-King cobra hukutana pale tu wanapotaka ku-mate na jinsia nyingine.
-Wako active muda wote wa siku.
-Hupendelea kukimbia hatari au kuattack anapomlazimika.

====> Nini tofauti yao kubwa endapo mmoja wao atakutana na mwingine?

BLACK MAMBA


A)Hatari ila anatabirika. Yupo tayari kupigana au akimbie kujiokoa
B) Kwa kila ng'ato humuachia adui kiasi cha 55 mg za sumu mwilini.

KING COBRA

A)Hatari na hatabiriki, anajiamini na kuattack kwa mahesabu.
B)Anaacha kiasi kikubwa cha sumu 420 mg; mwilini kwa adui kwa mng'ato mmoja.
C) Imethibitishwa kuwa king cobra ndie nyoka anaetumia akili sana kabla ya kuattack.

HITIMISHO:
~Black mamba akikutana na king cobra; ajitahidi kupigana ashinde au akimbie.

~King cobra akikutana na black mamba; kwanza kakutana na chakula au apigwe na afe.

MSHINDI: King cobra🥇
Black mamba ni Ana zilizala sio dogo mkuu na pia hana tabia ya kumkimbia mwanadam yani yeye ni mtata kiufupi mkikutana kiumbe hafai hata kidogo, "enzi tunasoma 'tabora boys' aliingia mmoja kwenye bweni letu basi hakuna mtu alie ingia ndani siku hiyo mpaka alipo amua kuondoka mwenyewe".
 
Back
Top Bottom