habari za kuaminika toka ndani ya CHADEMA sinasema kwamba chama hicho kinapanga kufanya uchaguzi mkuu wake mwaka 2013. Kwa mujibu wa katiba wa chama hicho Mbowe na Dr Slaa watakuwa wamefikia kikomo cha muda wa kugombea nafasi wanazoshikilia sasa.
Ni wazi kwamba Mbowe hawezi kushuka chini kwa kuwa ameshashikilia nafasi ya juu zaidi ya uenyekiti. Dr Slaa ana nafasi ya kupanda kwa kuwa alishuka toka umakamu na kuwa katibu mkuu hivyo ana nafasi ya kupanda kuwa mwenyekiti.
Vyanzo vya habari vinasema Dr Slaa amekubali kwa shingo upande kuwa Mwenyekiti kwa kuwa dhamira yake ilikuwa ni kuachana na utumishi wa chama kuwapisha vijana.
Hata hivyo ametoa sharti kwa chama hicho kumteua kijana bora wa kufanya naye kazi kama katibu mkuu wa chama.
Swali, ni nani anafaa kuwa katibu mkuu wa chama hicho kikuu cha upinzani?
......ndiyohiyo