Pasco, unajifanya una imani saanaa!!?!! Hivi unajua watu aina ya RA akikujua unafanya kazi sehemu yenye mafta au maslahi yake tayari hilo ni goli? Ile tu kujua kuna nini wapi,kiasi gani, tena in proven writen way,!! Karagabaho!
ukwelikitugani, sijifanyi nina imani sana, mimi ni mkweli daima na ni ukweli, nina imani sana. Hayo madini yanayochimbwa sasa, mbona tangu wakati wa Nyerere tulishayaona?. Kwani hao wachimbaji wamevamia au tumewakaribisha?. Jee walitulazimisha au tumewapa wenyewe?.
Sasa wewe si uko hapo TPDC, hebe eleza kuhusu ghiyo siri ya mafuta na gezi ya Mtwara!. Wakati wewe unadhani ni siri, nimeshakuambia, walioigundua wameisha ipatenti kuwa ni yao, nchi yao imeshafanya maandalizi yote muhimu, nyinyi na TPDC yenu ni just rubber stamp ku ok mradi, na gesi wataichimba wao, mkataba utasema ni gezi tuu, wachimbani ni wenyewe, wahifadhi ni wenyewe, wasafirishaji ni wenyewe, nyinyi mtaambulia kuuziwa na kugaiwa peanut!. Mkataba utaonyesha wanachimba gesi, ukweli ni kuwa watachimba wese!.
Kwani kilichotokea kilichotokea Arusha kwenye ule mradi wa kuchimba bauxite ni nini?. Kila penye bauxite, chini kuna Tanzanite. Tumewapa mkataba wa kuchimba bauxite, wachimbaji ni wenyewe, wasafirishaji ni wenyewe, sisi yetu ni nini pale zaidi ya mashimo?!.
Serikali ya Chadema ingeingia Madarakani, Mhe. Zitto angeisafisha TPDC sijui mwenzetu kama ungesalimika, labda kama ungemuwahi na kujitambulisha kwake wewe ni member wa jf, ingekuwa spared.
Kuhusu TPDC naomba usizidi kuzungumza humu ukatupandisha wengine hasira, tangu mlivyoifanza TIPPER, mkajikabidhi mikononi kwa waarabu kuleta mafuta yalisafishwa kwa sasa kwenye mafuta hamna tena chenu, mpaka jengo la Mafuta House likawaaibisha, tena kama sio NSSF kuokoa jahazi, mbona mngetembea uch....
Baada ya gesi kugundulika, sasa ndio mnajifanya kuikumbatia mpate pa kutokea?, too little too late, meshawahiwa na wenye patent zao za gesi yetu!.