Nani kasema kwamba CHADEMA hawatachagua Mwenyekiti Taifa?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,305
33,924
Naona kama vile kuna vurumai kubwa sana mitandaoni na kwenye vyombo vya habari shabiki vya CCM, vikihanikiza kwamba Mbowe hataki kutoka madarakani au CHADEMA hawataki kufanya uchaguzi wa Taifa.

Hapa Iringa wiki ijayo kutakuwa na uchaguzi kwenye Majimbo Mawili ya Mafinga mji na Iringa mjini. CHADEMA imeweka utaratibu kwamba hakuna wilaya itakayofanya uchaguzi kama haijafikia vigezo vilivyowekwa na chama.

Kwa maana nyingine ili upate wapiga kura wa Mkutano Mkuu ni lazima chaguzi za chini zifanyike na ndiyo hatua walioko CHADEMA kwa sasa. CHADEMA si chama cha kufanya Mkutano Mkuu kwa kuokoteza wajumbe wake mitaani kama vifanyavyo baadhi ya vyama vingine.

Ni lazima CHADEMA itafanya uchaguzi wake wa Mwenyekiti wa Taifa kupitia Mkutano Mkuu wa CHADEMA. Ni kwa nini CCM wanataka CHADEMA ifanye Uchaguzi wa Kitaifa kwa kufuata shinikizo toka kwa CCM.

CCM ijue adui yao ni wananchi wengi wa Tanzania waliyoichoka na wala si CHADEMA. Mapambano yenu na CHADEMA ni kupoteza muda kwani nguvu ya CHADEMA inatokana na CCM kuwa dhaifu katika kuongoza Serikali.

Kama Mbowe atachaguliwa tena kuwa Mwenyekiti inakuwaje ni tatizo kwa CHADEMA ambao ndio watakuwa wamemchagua wenyewe? Mbona CCM haijawahi kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti wake wa Taifa hata mara moja na CHADEMA hawajawahi kuhoji?
 
bila shaka uhu mchaga wa marangu
 
Kwani chadema kuwatangazia umma na wanachama wao kwamba uchaguzi utafanyika tarehe flani I nachukua gharama kaisi gani mkuu?
 
Bado Sana. Kuna uvumi kuwa Lissu anakwenda ACT. Kisa uwenyekiti. Na Zitto
Umewahi kusoma ama kusikia mahojiano yoyote yale ya Lissu na waandishi wa habari siku za hivi karibuni? Kura iwe ya wazi au ya Siri Lissu atamchagua Mbowe kuwa Mwenyekiti wake wa Taifa.

Lissu akienda ACT kwani itakuwa ndio nini?
 
Inaonekana kuna watu wanajenga taswira kwamba kuendelea kwa Mbowe kuwa madarakani CHADEMA ni tatizo. Hivi Mbowe kuwa kwake madarakani amesababisha nini kilicho hasi hadi kuendelea kuwepo kwake madarakani liwe ni tatizo la CHADEMA?
 
Back
Top Bottom