Nani kama Mama?

Nani kama Mama?

JOTO LA MOTO

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2018
Posts
766
Reaction score
562
Mama.jpg

SHAIRI:NANI KAMA MAMA.
MTUNZI:MSANII JOTO LA MOTO.


Mama hutunza uhai, kiumbe kuwasilisha.
Tisa miezi tumboni, unayaanza maisha.
Bila mama hatujai, duniani tutakwisha.
Yupo nani kama Mama, katika hii dunia.

Amdharauye Mama, kwenye jamii hafai.
Apewe yote lawama, achukiwe kama tai.
Tumpe somo kusoma, akome hayo madai.
Yupo nani kama Mama, katika hii dunia.

Maisha bila ya Mama, ni magumu kusikia.
Sina neno la kusema,kupata hizo hisia.
Hata shule ukisoma, hupati kumfikia.
Yupo nani kama Mama, katika hii dunia.

Ana huruma asili, Mama tangu kuzaliwa.
Familia kuijali, majanga sije fikiwa.
Ataponza yake hali, mwanaye abaki powa.
Yupo nani kama Mama, katika hii dunia.
 
Kweli aise, Mama apewe heshima yake stahili.
 
Km angekuwapo binadamu mwingine mwenye uwezo wa kubeba mimba bas tungemfananisha naye
Sas hapo utaona MAMA anashindanishwa na hewa[emoji23]
 
Back
Top Bottom