Nani kama Mama Vs Nani kama Baba

Babu naona leo umetuamkia lakini ukweli utabaki pale pale hakuna kama MAMA ukielewa neno mama vizuri utaelewa na msemo una maana gani ingawaje sikatai na baba naye ana umuhimu wake ushawahi kuona watu wakijikwaa huwa wanaita nani/??
 
Kamanda hii sredi unaitendea haki.... yaani unanikonga moyo.

Nimekuvulia kofia.
 
hilo sio tatizo. Kwenye isue ya vichanga kutupwa hovyo wote baba na mama mnahusika, ukifuatilia sana wababa mnasababsha vichanga vitupwe kwa kuzikataa hizo mimba zenu. Hebu umtie binti mimba afu usimkatae uone kama kuna vichanga vitatupwa M/nyamala. ( sijasema wadada mbebe mimba hovyo then mtupe vichanga. Ni dhambi )
Muda si mrefu ulopita pale Mwananyamala kama sikosei miili ya maiti za vichanga ilikutwa imetupwa. Nani kama mama?
 
Babu naona leo umetuamkia lakini ukweli utabaki pale pale hakuna kama MAMA ukielewa neno mama vizuri utaelewa na msemo una maana gani ingawaje sikatai na baba naye ana umuhimu wake ushawahi kuona watu wakijikwaa huwa wanaita nani/??

Na hawa kina mama wanaotelekeza watoto nao bado wana sifa ya "NANI KAMA MAMA"?
 
Tatizo we unapost via mobile. sijui uko gesti gani mida hii?
Ntake radhi babu. Niko ofcn bana kwenye laptop nafanya kazi ya ofisi then mdogo mdogo naingia Jf bosi akpita hanishitukii.
 
Asha D,
Nimependa sana jinsi ulivyomwaga utetezi wako hapa,
lakini kikubwa nachogundua hapa kwa mawazo yako,
na ya akina dada wengine hapa JF,
NI KATIKA UZAZI, yaani kubeba mimba, kunyonyesha nk.
ndipo ambapo mama anaonekana yeye ndo yeye na hakuna mwingine,
lakini hebu tujiulize, maisha yanajidhihirisha katika phase hiyo tu?
mbona mnasahau hatua zingine za maisha baada ya kuwepo tumboni kwa miezi 9,
kunyonya n.k.?

Pili, kama ndo hivyo, je wale akina dada wanaotupa watoto chooni, vichakani nao tuwaite NANI KAMA MAMA?
Je, wale akina mama wanaokaa na watoto wa kufikia na kila kutwa wanawatesa kwa mateso ambayo hata JEHANAMU unaweza usiyakute, je nao tuwaite NANI KAMA MAMA?

ASANTE,
NANI KAMA MUNGU?
 
Babu naona leo umetuamkia lakini ukweli utabaki pale pale hakuna kama MAMA ukielewa neno mama vizuri utaelewa na msemo una maana gani ingawaje sikatai na baba naye ana umuhimu wake ushawahi kuona watu wakijikwaa huwa wanaita nani/??

Wanaita "YESUUU" ama JESUS
 
Teh teh mpaka kieleweke leo mkuu nani kama baba?

Hakuna kama baba. Huu ndo msimamo wangu na ndo ukweli mtupu.

Hakuna wa kumlinganisha na baba yangu asee. Acheni utani kabisaaaa!

Kama hoja ni kuzaa, siku hizi chupa nazo zinazaa!....NANI KAMA CHUPA?
 
Kamanda hii sredi unaitendea haki.... yaani unanikonga moyo.

Nimekuvulia kofia.

Unajua nini kamanda? Hii nyuzi yako imenigusa sana. Kuna baba wengi sana ambao hawatendewi haki yao. Wababa tunajipinda na wakati mwingine kujinyima ili tuweze kuwapa wanetu misingi bora ya maisha lakini bado tu hatuthaminiwi kama inavyostahili.

Wengine tunafanya mengi kuliko hata hao mama zao waliowazaa lakini wapi. Hatupewi haki yetu. Inasikitisha sana mkuu. Laiti watu wangejua jinsi wengine tunavyowahangaikia wanetu labda wangeweza kututhamini.
 
Nadhani hapa unaangalia zaidi uchakachuzi wa maisha lakini in real sense ukitazama neno mama na majukumu yake ndo maana huu msemo unasimama na tukianza kutazama majukumu ya mama yaliyochakachuliwa unakosea kwa sababu hao hawasimami kwenye nafasi ya mama.

Huu msemo unasimama kwa maana ya mama na uwezo,hekima,uvumilivu pamoja na majukumu yake yote aliyotunukiwa na Muumba na ndio ilivo babu na itakavokuwa siku zote.

Nadhani hujanielewa. Huyu binti naekaa naye, mama yake alimtelekea. Na mai waifu wangu ndo anamlea.

Huyu aliyemtelekea naye ndo "NANI KAMA MAMA" kwa kuwa tu alibeba mimba kwa miezi tisa?
 
Ntake radhi babu. Niko ofcn bana kwenye laptop nafanya kazi ya ofisi then mdogo mdogo naingia Jf bosi akpita hanishitukii.

Hahahaha....JF adikshen!

Nakutaka radhi............Nani kama baba?
 
Hao sio kina mama sababu hawajui wala hawako tayari kuwa mama,hapa anatazamwa mama aliye mama na amabaye amevaa uhusika wa kimama.
TUSICHANGANYE MADESA SASA HATA TUNAPOSEMA HAKUNA KAMA BABA SIO WOTE NI KINA BABA WENGINE NI WAMWAGA MBEGU TU.

Na hawa kina mama wanaotelekeza watoto nao bado wana sifa ya "NANI KAMA MAMA"?
 
Kama baba wapo. Kama mama hakuna.

Wakina nani kama baba? maana kwenye kubeba mimba siku hizi mama analinganishwa na chupa na kwenye kunyonyesha mama ana linganishwa na maziwa ya unga kibao yamejaa kwenye ma super market kwa hiyo walio kama mama wapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…