Nani kakuambia huwezi kutimiza malengo yako?

Jul 13, 2021
19
35
Hivi unajua unaweza Kutimiza Malengo Yako kama utaamini unaweza kufanya hivyo na tofauti na hivyo itakuwa vigumu.

Kushinda au kushindwa kunaanzia ndani ya fikra zako.

Kabla ya kuona uhalisia wenyewe, Je, fikra zako ni za ushindi au kushindwa?

Kila mtu unayemuona kwenye dunia hii ana masaa 24 kama ya kwako, tofauti inakuja namna katika kutumia masaa 24 hayo.

Kwahiyo...

Unaweza Kutimiza Malengo yako pasipo kujali umeshindwa au hujaweza mara ngapi, lakini ukiamini unaweza na kweli utaweza.

Kwa sababu ndani yako una nguvu kubwa ambayo inafanya kazi, unapoamua kusema mimi (Jina lako) naweza Kutimiza Malengo yangu pasipo kujali kizuizi gani kipo mbele yangu.

Unaweza Kutimiza Malengo Yako na ukapata matokeo makubwa kama ambavyo “Role model” wako wanaweza Kutimiza Malengo yao.

Swali la kujiuliza,

Kwanini unashindwa Kutimiza Malengo Yako?

Hujashindwa sema tu umehararisha kushindwa Kama kisingizio kuwa huwezi Kutimiza Malengo ni kitu ambacho sio kweli.

Japokuwa...

Kushindwa Kutimiza Malengo ni sehemu ya mchakato Kwahiyo huna sababu ya kukata tamaa, unajifunza kupitia kushindwa kwako na kusonga mbele ili kesho ushinde kwa kishindo.

Kwahiyo...

Nani kakuambia huwezi Kutimiza Malengo Yako?

Haijalishi ni nani aliyekuambia hata kama unamuamini kwa kiasi gani, tambua alichokuambia siyo kweli hata kidogo ni uongo ambao unageuzwa kuwa kweli.

Ni kweli huwezi Kutimiza Malengo Yako unavyojiona Hebu sema ukweli? Safi kwa kusema unaweza na kweli unaweza sana.

Unaweza sana mtaalamu! Usikubali mtu mwingine akuambie tofauti.

Ukweli huu utakuweka huru...

Unaweza Kutimiza Malengo Yako ni suala la wewe kuwa na maarifa sahihi juu ya malengo na namna gani uwe na mipango thabiti ya Kutimiza Malengo yako.

Na kushinda tabia hizi,

1. Tabia ya kughairisha mambo.

2. Tabia ya kusitasita.

3. Tabia ya visingizo na kulaumu.

4. Tabia ya kuridhika na kujichukulia poa.

Basi...

Fanyia kazi ambayo umejifunza kwenye makala hii.

Umejifunza nini kwenye Post ya leo? Comment hapo chini
_____
Ps, Unataka Kutimiza Malengo Yako si ndiyo? Basi Bofya link hapa chini sasahivi kuna episode nyingi zitakusaidia sana.
 
Back
Top Bottom