Nani kajibiwa na NIDA baada ya kutoa 100/=?

Nani kajibiwa na NIDA baada ya kutoa 100/=?

Alafu waseme kama wiki endi hawapo hewani, sio wanakauka alafu jtatu wanaingia ofisini na kuwahi kwenye 'kibubu' chao.
 
Mi nilivyoona wanataka 100 nikajikalia kimya!Nawajua hawa jamaa,rambirambi za lucky vicent hivi tulijengea makumbusho vilee eeeh!Na za wahanga wa tetemeko tuliwajengea wajane vijana kuliko dadaangu wa kwanza.Siwaaminigi hawa watu kwenye pesa nyuso zao huwa hazina soni kabisa
 
Aiseee huu ni upigaji mm kitambulisho nilipoteza na nimefanya replacement hawajanipa mpaka leo natuma wananijibu eti taarifa za usajili hazijapatikana
 
Naomba utaratibu wa ku claim 300 yangu iliyoliwq maana huu ni wizi kama wizi mwingine
Nenda polisi ukawafungulie RB, then sehemu yoyote ukiwaona ni kuwakamata tu. Yaani tupilia ndani
 
Yaweza kuwa wanaubia na klabu yangu pendwa ya Yanga, changia yanga, changia N**Da
 
Mnielekeze nikipiga hiyo menu nachagua nini
.
IMG_20190429_134649.jpeg
 
Naona 100 zinazidi kuyoyoma lakini jibu la namba ya kitambulisho sipewi. Kuna aliyefanikiwa baada ya kukubali makato ya Tsh 100 kupitia *152*00#?
Siku ya kwanza tu nilivyojaribu nimejibiwa na Kwa bahati nzuri nimepewa namba za kitambulisho.
 
Sijaelewa wazee baba na wazee mama.

Yaani hii ni huduma ya nini nami nobofye nina ka jero nimeweka sasa kwa mama muuza.
 
Ni kwamba utajibiwa kwa kutumiwa namba ya kitambulisho kama kitambulisho chako kipo tayari
Kwa hiyo kwa wale ambao hawakujiandikisha kutengenezewa vitambulisho wanaliwa pesa tu...

NIDA wawajulishe wale waliojiandikisha halafu vitambulisho vyao vipo tayari ili watume huo ujumbe wapatiwe namba ya vitambulisho vyao.
 
Mimi nilijibiwa muda huo huo kwa kutumiwa namba ya NIDA(kitambulisho)

Ni kwamba utajibiwa kwa kutumiwa namba ya kitambulisho kama kitambulisho chako kipo tayari
Kuna jamaa yangu nae wameshamjibu, nadhani ni kama ulivyosema. Kwahiyo wengi wa walio poteza 100 zao ni wale ambao vitambulisho vyao havijawa tayari.
 
Nimepewa namba ila wapo active sana Airtel...

Nilivyoingiza namba kwenye website yao kweli kimetokea kitambulisho changu
 
Nadhani kikubwa ni kwenda kwenye ofisi ulizoandikishwa hasa akina sie wa mwaka jana, ukifika pale unaonyesha majina yako matatu then wanaangalia kama kitambulisho chako kipo wanakupa. Zaidi ya hapo ni kuendelea kuliwa 100 kila siku.
 
Naona 100 zinazidi kuyoyoma lakini jibu la namba ya kitambulisho sipewi. Kuna aliyefanikiwa baada ya kukubali makato ya Tsh 100 kupitia *152*00#?
Hawajawahi nijibu niachana nao wanakula hela zangu tu
 
Mimi nilijibiwa muda huo huo kwa kutumiwa namba ya NIDA(kitambulisho)

Ni kwamba utajibiwa kwa kutumiwa namba ya kitambulisho kama kitambulisho chako kipo tayari
Hata kama kitambulisho bado si wajibu. Sasa unatuma kuuliza wanakaa kimya unarudia zaidi ya mara kumi khaa
 
Back
Top Bottom