Ukweli mchunga asante mzee tupatupa kwa kulijua hilo, ukweli ni kwamba operation UKUTA imefanikiwa kwa 85% kabla ata ya tarehe moja, ccm imeshindwa kujua mtego wa chadema, nao ccm ikaingia miguu miwili na matokeo yake ujumbe wa maudhui yamefika kwa wananchi bila ata maandamano wala mkutano wa siasa, ikumbukwe kuwa nia na mazumuni ya UKUTA ni kuwafikishia wananchi kile ambacho Chadema wanakiamini kuwa mkuu wa kaya anavunja katiba ambayo alihapa kuitetea na kuilinda.
Kwa minajili hiyo CCM wakaingia kichwa kichwa kupambana na ukuta, kwakuwa ndio chama tawala imepelekea vyombo vya dola asa polisi nao kuingia kichwa kichwa kupambana na UKUTA, na matokeo yake wao ndio wakawa wasambazaji wa UKUTA uku wakisahau kuwa UKUTA ni idea ipo vichwani, UKUTA sio maandamano bali ni fikra ambapo uwezi kuzitoa kichwani kwa mtu ,ila maandamano yaliwekwa ili zile idea zipate kuwafikia wananchi as the result ccm imejikuta ikiitangaza UKUTA bila kujijua, nachelea kusema kwamba UKUTA imefanikiwa kwa 85% kabla ata ya tarehe moja.
UVCCM wamestukia hii wakati ni too late, ndio mana na wao wakatangaza maandamano mwisho wa mwezi huu.
Kwa minajili hiyo na ni ukweli usiopingika chadema kuna great thinker wanaotumia akili za juu kufikili kisiasa kuliko chama tawala, natambua kuwa chama tawala kuna wasomi wengi kuliko chadema, je wapo huru kushilikisha akili zao na zikafanyiwa kazi?