Chama cha mafisadi ndio kimeshika utamu. Kwa hiyo kama viongozi wa serikali wanatoka katika chama cha mafisadi basi serikali pia imejaa mafisadi na ni fisadi pia. Utakuwaje sio fisadi kama mafisadi wanaachiwa wanapeta tu bila kuchukuliwa hatua zozote?
Sasa wewe unasubiri nani awachukulie hatua? Kuna sheria yoyote inayokuzuia kuwachukulia hatua? Tatizo lenu mnataka kufanya ufisadi ni political agenda. Mtu kama fisadi anatakiwa kupelekwa mahakani na mtanzania yoyote ana uhuru wa kufanya hivyo. Kama unashindwa mwambie Slaa awapeleke mahakamani kwa maana yeye ndiye mwenye ushahidi wote.