jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,331
- 25,236
CCM Kuongeza kiwango cha MadiniBy Mike Mushi | Published 11/26/2005 | Habari Mpya |
CCM Kuongeza kiwango cha Madini
Chama Cha Mapinduzi kinakusudia kuongeza kiwango cha thamani ya madini kutoka asilimia 0.3 ya hivi sasa hadi kufikia asilimia 3 iwapo chama hicho kitashinda katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk Ali Mohamed Shein amesema pamoja na kuongeza viwango vya madini hayo pia serikali ijayo itahakikisha inatengeneza vito vya madini hapa hapa nchini ili kuweza kuuza madini kwa tija.
Dk. Shein ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Londoni wilayani Manyoni.
Amesema suala la madini limepewa kipaumbele katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2005-2010 kutokana na ukweli kwamba sekta ya madini inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuinua uchumi wa nchi.
Amewaambia wananchi waliohudhuria mkutano huo kuwa ili kufanikisha azma hiyo serikali itatoa mikopo na elimu kwa wachimbaji wadogo wadogo kwa njia ya semina na mikutano ili waweze kujua namna ya kuchimba madini hayo kitalaam.
�Baada ya kupewa mikopo, mpewe elimu kwa njia ya semina, mikutano au warsha mjue namna ya kuchimba madini hayo kitalaam�. Aliwaeleza wananchi hao ambao wengi wao ni wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu katika eneo hilo.
Dk. Shein amethibitisha kuwa serikali ya awamu ya nne itaendelea kukaribisha wawekezaji wakubwa katika sekta ya madini na pia itaangalia upya sera yake ya madini ili iweze kuwanufaisha wadau wote.
Amesisitiza wananchi wakichague Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa ndio chama pekee kinachoonyesha jitihada za kuwawezesha wachimbaji wadogo wadogo kuweza kupambana na umasikini hali ambayo hatmae itawafanya kuwa na maisha bora.
Katika hatua nyingine Mgombea Mwenza huyo amewataka wachimbaji wadogo wa madini nchini kutumia fedha wanazozipata kwa kujijenga kimaisha kwa kuwa na nyumba bora, kutunza afya zao na kusomesha watoto na sio kwa anasa.
�Fedha ni fedheha, zikiwa nyingi zinachanganya kidogo hujui utazifanyia nini, unaishia sehemu ukiulizwa wewe nani na wewe unauliza pia wewe nani. Huo si utumiaji mzuri wa fedha�. Alisema Dk Shein
�Hata hivyo starehe zikizidi inachangia maambukizi ya ukimwi hilo nalo ni tatizo tukitambua ukimwi sasa ni janga la kitaifa. Hivyo hamna budi kuwa waangalifu na matumizi ya fedha�. Aliongeza.