Nani atangulie?

kipumbwi

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
3,056
8,716
NANI ATANGULIE

Kifo hakina chaguo, chabeba kimtakae

Wawili wapendanao, mke mume kichukue

Na hata kwa mkupuo, bora kifo kiamue

Ni nani atangulie, kati ya mke na mume?

Mke ndiyo kimbilio, watoto awapikie

Baba naye tegemeo, riziki awachumie

Mmoja akifa leo, watamani wazimie

Ni nani atangulie, kati ya mke na mume?

Kwa mke na mume nao, mapenzi nisikwambie

Hahitaji kati yao, mwenzie amkimbie

Waishi maisha yao, kwa pamoja wajifie

Ni nani atangulie, kati ya mke na mume?

Na hata wazazi nao, hawataki wasikie

Kije wasibu kilio, na wana wawalilie

Nawaza kila uchao, jibu unisaidie

Ni nani atangulie, kati ya mke na mume?

Ukweli jama sinao, na mimi mke ninae

Sasa nawaza mwenzio, na wewe uniwazue

Hili jambo ni tishio, hakuna alipendae

Ni nani atangulie, kati ya mke na mume?

Msimbe au mkeo, ni nani atangulie

YOB na mama yao, yupi nyuma abakie

Mlojo na mpenzio, kimya usijikalie

Ni nani atangulie, kati ya mke na mume?

Hapa naweka uzio, kadi tama niishie

Uliza na jiranio, majibu unitumie

Nipate wako upeo, roho yangu itulie

Ni nani atangulie, kati ya mke na mume?

Mwinyikombo Ally Mwinyikombo

Dar es Salama

0717423723

0767175191
 
Shairi zuri ila ni tofauti na mi nilivyofundishwa na walimu wangu shuleni.
Mfano;

mkeo,
yao,
mwenzio,
Hapo vina havijakaa sawa

niishie,
unitumie,
itulie,
Hapa ndo upo sahihi
 
NANI ATANGULIE

Kifo hakina chaguo, chabeba kimtakae

Wawili wapendanao, mke mume kichukue

Na hata kwa mkupuo, bora kifo kiamue

Ni nani atangulie, kati ya mke na mume?

Mke ndiyo kimbilio, watoto awapikie

Baba naye tegemeo, riziki awachumie

Mmoja akifa leo, watamani wazimie

Ni nani atangulie, kati ya mke na mume?

Kwa mke na mume nao, mapenzi nisikwambie

Hahitaji kati yao, mwenzie amkimbie

Waishi maisha yao, kwa pamoja wajifie

Ni nani atangulie, kati ya mke na mume?

Na hata wazazi nao, hawataki wasikie

Kije wasibu kilio, na wana wawalilie

Nawaza kila uchao, jibu unisaidie

Ni nani atangulie, kati ya mke na mume?

Ukweli jama sinao, na mimi mke ninae

Sasa nawaza mwenzio, na wewe uniwazue

Hili jambo ni tishio, hakuna alipendae

Ni nani atangulie, kati ya mke na mume?

Msimbe au mkeo, ni nani atangulie

YOB na mama yao, yupi nyuma abakie

Mlojo na mpenzio, kimya usijikalie

Ni nani atangulie, kati ya mke na mume?

Hapa naweka uzio, kadi tama niishie

Uliza na jiranio, majibu unitumie

Nipate wako upeo, roho yangu itulie

Ni nani atangulie, kati ya mke na mume?

Mwinyikombo Ally Mwinyikombo

Dar es Salama

0717423723

0767175191
Thread za kifo kifo hzi khaa!! Tunagwaya sasa
 
Shairi zuri ila ni tofauti na mi nilivyofundishwa na walimu wangu shuleni.
Mfano;

mkeo,
yao,
mwenzio,
Hapo vina havijakaa sawa

niishie,
unitumie,
itulie,
Hapa ndo upo sahihi
Mkuu hembu tujibie huo ushairi kwa kesho tafadhali!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom