Nani atakuwa Rais muokozi wa Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani atakuwa Rais muokozi wa Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lampart, Dec 24, 2009.

 1. L

  Lampart Senior Member

  #1
  Dec 24, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NANI ATAKUWA RAIS MUOKOZI WA TANZANIA???

  • Ni lazima atoke upinzani
  • Mwana-CCM yoyote hafai, hata akitoka mbinguni
  • Bila ya upinzani kuungana, mengine yote ni ndoto ya mchana

  Wakati ndugu zetu wa ZNZ tayari washajua nani atakuwa Rais wao baada ya uchaguzi wa 2010, sisi kutoka Bara bado tunatia mikono yetu gizani kumdhania huyu au yule atafaa kama Kikwete kweli atapumzika mwakani kutokana na matatizo yake ya akili.

  Kama Rais ajae atatoka tena CCM kama wengi wanavyotabiri, basi hatuna haja ya kupata shida ya kumfikiria nani ni mfanyakazi bora au dikteta zaidi katika kazi ambae atakuja kutufaa na kuiokoa hii nchi. Mwana-CCM yoyote yule atafaa. Hii nchi ni kweli imegombolewa na TANU, lakini haitookolewa na CCM. Ni lazima kiwe chama chengine cha kuleta mapinduzi hayo tunayoyalilia kila siku. CCM imemalizika na Kikwete kaizika – haina fire power tena!

  Yoyote atakaetoka CCM mwakani kama Rais mpya wa Jamhuri yetu, hatokuwa tofauti na Kikwete au na hao wawili waliopita, hata kama yeye hivi sasa ni waziri anaesifika kwa kulitumikia Taifa letu vizuri sana. Kuwa waziri mzuri na mchapakazi is one thing na kujakuwa Rais muokozi is quite another. CCM tayari ishajiwekea system yake mbovu na mtu yoyote atakaechaguliwa hatoweza kuenda kinyume na system hio, hata kama akiwa mfanyakazi mzuri sana. Kwahivyo, wale wanaomfikiria fulani anafaa watakuja kuvunjika moyo watakapokuja kumuona huyo waliemchagua ni sawasawa au zaidi ya huyu Kikwete, kwasababau system ya CCM ya kubebana ni tayari ishakuwa set up na ukikataa kuwabeba wenzio basi ujue utakuenda na maji.

  Ni juzi juzi tu hapa tulipomuona Nyerere mbaya alivyompeleka mbele Mkapa na sote tukawa tunamlilia Kikwete na Lowassa, kwani tukiona wao ni watoto wa new generation na mambo chini yao yangekuwa mazuri. Je, new generation imetupeleka wapi leo? Bado tu hatujaacha hii tabia ya kumuona mtu fulani atatufaa kutoka CCM? CCM yote haitotufaa seuze mtu fulani. CCM kishakuwa chama obsolete na kinafaa kipigwe marufuku, kama
  kilivyopigwa marufuku CCCP kule Urusi.

  Kwahivyo, tunapofikiria nani atatufaa - mtu yoyote kutoka CCM iwe out of our minds. Hata akitoka mbinguni, lakini akiwa
  mwana-CCM basi mambo yatakuwa haya haya tu kama yalivyo
  hivi sasa. Hii ni kwasababu ya system ya kubebana
  ilivyo na sio kwasababu ya mtu mwenyewe alivyo.

  Atakaeiokoa nchi hii ni Rais kutoka upinzani na sio kutoka CCM. Kwahivyo, badala ya kupeyana nambari za simu ili tumshawishi mtu fulani wa CCM agombee urais mwakani, ni bora tutumie nguvu zetu kuvishawishi vyama vya upinzani nchini vikubaliane kumuweka mtu mmoja kugombea urais. Wapinzani wakiungana CCM itaanguka na hapo ndipo tutakapopata muokozi wa kweli wa hili Taifa. Kutegemea fulani ni waziri machachari na hodari wa kazi yake kutoka CCM na atakuja kuliokoa Taifa ni sawa na kutokutumia akili zetu vizuri, kwani katika chaguzi zetu za Rais hapa Tanzania tunakichagua chama na sio mtu. Kwahivyo, CCM ikishinda urais na Rais mpya akawa anafanyakazi zake kinyume na system ya kubebana ya CCM ilivyo, definitely watamuweka upande na badala yake fisadi atawekwa kuwa Rais na mambo yataenda kama yalivyo hivi sasa!
   
 2. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  I say, wewe jamaa ushaniharibu akili yangu. Nilikuwa nishafurahi kuwa Magufuli ndio atakubalika kuwa Rais wetu, lakini kutokana na haya maneno yako ninaamini uyasemayo - yaani hata huyo Magufuli awe mfanyakazi hodari vipi, lakini madamu anatoka CCM itabidi afuate system ya CCM or else watampeleka na maji.
  Sasa kwa kweli hata sijui hii nchi itaongozwa na nani.
  Anyway, kama ulivyoeleza, bila ya wapinzani kuungana basi tutabaki tunacheza tu milele hapa Tanzania!!!
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Dec 24, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  We can't do the same thing all years and expect to get different results.
   
 4. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Kwahivyo Kichuguu unaamini kama ninavyoamini mimi kuwa Rais muokozi hatotoka CCM kama hii article inavyosema????
  Kama ni hivyyo basi tunafikiri sawa na huyu muandishi!!!
  Vipi sasa tutawafahamisha na Watanzania wengine kuwa if you do the same thing everyday u should not expect a different result?
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Magufuli is the choice!
  aNAWEZA, ANAJIAMINI, NA SI MFISADI(so far)
   
 6. L

  Lampart Senior Member

  #6
  Dec 24, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa ninafahamisha kwa haraka haraka tu kuwa CCM lisiwe chaguo letu tena hata kama tunamjua Waziri fulani ambae anaweza kutufaa.
  Any CCM memba itabidi afuate mkondo wa CCM na atatupoteza tu.
  Kuiweza Tanzania leo na kujua vipi nchi imeliwa na rushwa ni lazima Mkapa, Kikwete, Rostam, Lowassa, Chenge, etc etc wapelekwe Mahakamani na wajibu hoja na masuala kadhaa, sasa Raisi gani wa CCM atakaeweza kufanya hivyo na akabakia kuwa Rais????
  Watanzania ni lazima sasa tuamke na tusifikiria hata kidogo kumchagua memba wa CCM kuwa Rais wa Jamhuri yetu tukufu, kwani matokeo yatakuwa ni haya haya ya Kikwete.
  La muhimu ni kujitahidi wapinzani waungane na wamuweke mgombea wa urais mmoja, bila ya hivyo kazi yetu yote ni ya bure!
   
 7. L

  Lampart Senior Member

  #7
  Dec 24, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pakajimmy, bado hujaifahamu CCM. Hatusemi kama kila mtu katika CCM ni mlaji na ni corrupt au hajiamini au ni fisadi. A lot of CCM members sio mafisadi kabisa na ni makabwela kama sisi. Problem ni system ya CCM ni corrupt na Magufuli hatoweza kuikimbia. Akiwakimbia watamtoa na fisadi atawekwa. The only solution ni kupatikanwa Rais kutoka upinzani ambae hatokuwa tied to any strings za CCM!!!!
  Rais wa upinzani ataweza kumpeleka MKapa, Kikwete, Rostam, Chenge, Lowassa, Mahakamani. Magufuli is a good hardworking guy, lakini hatoweza kumpeleka Mkapa, Kikwete, etc Mahakamani. Akijaribu kufanya hivyo basi yatamkuta yaliomkuta Aboud Jumbe. Tafadhali, usicheze na CCM!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 8. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Ikiwa RAIS atakuwa huyu huyu aliyepo. Ni bora kusiitishwe uchaguzi mkuu kuokoa pesa. Maana atatuEPA tena, we all know he is unable to handle the presidency. WaTZ ni kama watu waliouza mafahari ya ng'ombe ili kusolve kesi ya kuku.
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  pj,
  look here!I KNOW YOUR JOKING,for the bolded part of your post
   
 10. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45

  Shida sio kuwa CCM haina watu wakuaminika.
  Sio kila mwana-CCM ni fisadi - tukisema hivyo tutakuwa tunajifurahisha.
  Kuna wana-CCM ambao kama wangelikuwa out of the CCM system wangefanya ya maana sana kwa jamii yetu, lakini wanashindwa kufanya hivyo kutokana na system ya CCM.
  Hata kama Magufuli anajiamini na sio fisadi, he won't be able to beat the CCM system ya kubebana na kufichana. Akajaribu kuenda kinyume na hii system ya CCM basi atakuwa-replaced.
  Hio kuchapa kazi kwake ni huko huko wizarani tu, akiwa Rais na akianza kuwagusa akina Mkapa, Kikwete, Lowassa, Chenge, Rostam. etc atakuenda na maji hapo hapo!!!
  Kabla hatujapendekeza jina la Rais ajae, kwanini hatujiulizi kwanini Kikwete akashindwa? Huyo Kikwete hakuwa chaguo letu na la sisi wote? Sasa kitu gani kilichomfanya awe hivi?????? Jibu ni system ya CCM ambayo hata huyo Magufuli hatoiweza kama ilivyomshinda Kikwete ambae kaamua to swim with the current ili asije kuachwa nje!!!
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Dec 24, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  I am sorry to say this, but CCM must GO for real changes to happen !!!,
   
 12. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Tumekusikia ndugu!!!!!
   
 13. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lampart,

  Umenena na chaguo sahihi kwa mgombea toka upinzani ni Dr. W. Slaa.
   
 14. L

  Lampart Senior Member

  #14
  Dec 24, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nd. Sabi Sanda,

  Dr. W. Slaa as long as anatoka upinzani ni sawa, kwasababu hatochelea kumpeleka Mahakamani Kikwete, Mkapa, Mwinyi, Chenge, Lowassa, etc etc, kujibu shituma zozote zile. Sasa hapo ndipo atakaechaguliwa kuwa Rais ataanza kufikiri kuwa kumbe kunakuwajibika mbeleni!!!!
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Dec 24, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280

  Hata mimi naamini hivyo ingawa sina uhakika sana kwani watu hugeuka. Tuliwahi kuwa na Dr. Kaborou akiikamata serikali huko Bungeni lakini baadaye akarudi huko huko CCM, na wala leo hii hatujui anafanya nini huko Afrika ya Mashariki alikopelekwa kama malipo yake. Vile vile inawezekana kuna ambao ni bora zaidi ya Slaa, hata hivyo kwa sasa hivi ninakuwa na imani naye hasa kutokana sio na uwezo wa kuona mambo kwa kina bali pia na ushujaa wake kisiasa.
   
 16. Kidege

  Kidege Member

  #16
  Dec 24, 2009
  Joined: Jul 18, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ni kweli kama rais atabaki kuwa huyu huyu, kuna haja gani ya uchaguzi! maana wana CCM watakuwa wameshajiandaa na EPA za kila aina, expecting a lot of semina elekezi pale snow crest Hotel huku watz tukikosa hata madaraja tu barabarani.
   
 17. Kidege

  Kidege Member

  #17
  Dec 24, 2009
  Joined: Jul 18, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  vile vile kwa kuwa Tz ni shamba la bibi, ni vyema sasa tuwaachie wapizani ili hata kama nao wataiba, waibe ili lile gap lipungue kwenye Jamii.
   
 18. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #18
  Dec 24, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  CCM MUST GO!ni wimbo wa kila anaejua kutaipu kwa kiibodi au kiipad!TATIZO NI MOJA TU,nani aingie????????
   
 19. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #19
  Dec 24, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280

  Hivi rais wa ZNZ baad ya 2010 ni nani?? Wengine hatujamjua. Au kwa vile sisi siyo waZNZ????
   
 20. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #20
  Dec 24, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  PJ cha kukumbuka kama mtoa mada hii alivyoandika ni kwamba kinachoitwa CCM ni system na system yoyote ina namna yake ya kuendesha mambo yake na hivyo mtu mmoja anayepewa dhamana ya uongozi hawezi kufanya chochote kinyume cha mfumo utakavyo.

  Katika hali ya kawaida Magufuli anaweza kuwa kiongozi mzuri ila usisahau kama alivyo kuwa waziri wa miundombinu (Mkapa regime) na kuruhusu ule wizi wa nyumba za serikali na yeye binafsi kuambulia chache alizo wagawia ndugu zake binafsi na bila kuzingatia sheria. Hapa rejea nzuri itakuwa samaki mmoja akioza wote wameoza. Kwa hiyo kama alivyofanya uamuzi huo wa kuuza nyumba za serikali kwa amri ya bosi wake Mkapa, atakuwa anatekeleza amri za wezi wenzie CCM hata kama kwa kuzaliwa ni msafi, msafi ndani ya CCM hajazaliwa bado.

  Ni mzuri ki utendaji lakini once sio kila vision yake itazingatiwa bila kuwa filtered na mwajiri wake ambaye ni CCM, tusitegemee jipya, fikiria upya PJ.
   
Loading...