Nani atakuwa Rais muokozi wa Tanzania?

NANI ATAKUWA RAIS MUOKOZI WA TANZANIA???

Wakati ndugu zetu wa ZNZ tayari washajua nani atakuwa Rais wao baada ya uchaguzi wa 2010, sisi kutoka Bara bado tunatia mikono yetu gizani kumdhania huyu au yule atafaa kama Kikwete kweli atapumzika mwakani kutokana na matatizo yake ya akili.

Atakaeiokoa nchi hii ni Rais kutoka upinzani na sio kutoka CCM. Kwahivyo, badala ya kupeyana nambari za simu ili tumshawishi mtu fulani wa CCM agombee urais mwakani, ni bora tutumie nguvu zetu kuvishawishi vyama vya upinzani nchini vikubaliane kumuweka mtu mmoja kugombea urais. Wapinzani wakiungana CCM itaanguka na hapo ndipo tutakapopata muokozi wa kweli wa hili Taifa. Kutegemea fulani ni waziri machachari na hodari wa kazi yake kutoka CCM na atakuja kuliokoa Taifa ni sawa na kutokutumia akili zetu vizuri, kwani katika chaguzi zetu za Rais hapa Tanzania tunakichagua chama na sio mtu. Kwahivyo, CCM ikishinda urais na Rais mpya akawa anafanyakazi zake kinyume na system ya kubebana ya CCM ilivyo, definitely watamuweka upande na badala yake fisadi atawekwa kuwa Rais na mambo yataenda kama yalivyo hivi sasa!

Maandishi niliyoweka red, sijapenda kabisa kauli hiyo. Ni kweli inawezekana kwamba tunamchukia Rais wetu lakini tumpe heshima yake jamani. Hivi wewe babako akiambiwa akili yake ina matatizo unajisikiaje? au ungekuwa wewe ndo kiongozi wa nchi ukaambiwa hivyo unajisikiaje? Tuache dharau zinazopita mipaka bwana. Huyu ni kiongozi wa nchi, kwanini tumdhalilishe hivyo? Wakati tunamchagua hatukuona kama akili yake ina matatizo? Iwaje leo tuseme hana akili? Uliyeandika haya lazima na wewe akili yako siyo timamu.
La pili, unasema wapinzani waungane! Ni nani aliyekwambia wapinzani wa tanzania wapo kwa maslahi ya taifa? Ingekuwa hivyo siwangeshaungana siku nyingi? Hawana lolote hawa, na kuamini kwamba wapinzani wataleta ukombozi tanzania ni kujilisha upepo. Upinzani wa kweli utatoka CCM, angalieni mfano wa Kenya, wapinzani wa kweli walitoka KANU na hao ndiyo waliokuja na wazo la muungano, siyo hawa wanaoangalia tu masilahi yao. Mara ngapi wamejaribu kuungana wakashindwa? Ndo maana mwenzao Makamba anawaita mapaka, wanavutana mikia badala ya kumkabili panya. Wala hakuna tumaini lolote kwa hawa wapinzania wa bongo. porojo tu!
 
La pili, unasema wapinzani waungane! Ni nani aliyekwambia wapinzani wa tanzania wapo kwa maslahi ya taifa? Ingekuwa hivyo siwangeshaungana siku nyingi? Hawana lolote hawa, na kuamini kwamba wapinzani wataleta ukombozi tanzania ni kujilisha upepo. Upinzani wa kweli utatoka CCM, angalieni mfano wa Kenya, wapinzani wa kweli walitoka KANU na hao ndiyo waliokuja na wazo la muungano!

kwani na hao kina Lyatonga na wengineo wao walitokea chama gani? si CCM!!
 
......... Hivi wewe babako akiambiwa akili yake ina matatizo unajisikiaje? au ungekuwa wewe ndo kiongozi wa nchi ukaambiwa hivyo unajisikiaje?

I say, Vangi unachekesha kweli. Wewe mwenzetu kwani husomi magazeti baada ya hizi habari za bure za hapa ukumbini JF????
Kwani aliyesema akili yake inamatatizo ni nani isipokuwa yeye mwenyewe pale uwanja wa ndege DSM. Au hukumuona kwenye TV akisema maneno hayo yeye mwenyewe???
Au ndio husomi magazeti mwenzetu na wala hutizami TV zetu za DSM????

Tuache dharau zinazopita mipaka bwana. Huyu ni kiongozi wa nchi, kwanini tumdhalilishe hivyo?

Yeye mwenye ndio aliyejidhalilisha. Hakuna hata Mtanzania mmoja aliemueleza kuwa ni mwenye matatizo ya akili isipokuwa yeye mwenyewe. In fact, wengine hata tusingelijua kama alipima akili yake huko T & T.
Kwanini sasa unaukataa ukweli, wakati yeye mwenyewe ndio aliesema kuwa kapimwa akili yake huko T & T??? Au yale kasema kudanganya toto???
Wewe mwenzetu ni kada wa zamani sana wa CCM - maanake hata maneno yake mwenyewe unayakataa!!!

Wakati tunamchagua hatukuona kama akili yake ina matatizo? Iwaje leo tuseme hana akili?

Sisi tunafuata ametueleza nini yeye mwenyewe pale airport. Huko nyuma hajatueleza kuwa alikuwa na matatizo ya akili, kama angelisema hivyo, basi wengi tusingelimpigia kura zetu!!!

Uliyeandika haya lazima na wewe akili yako siyo timamu.

Sasa haya tena unasema kwa chuki, lakini la muhimu ni kuwa hakuna aliyemuelezea Rais wetu kama anamatatizo ya akili isipokuwa yeye mwenyewe. Angelikaa kimya wala tusingelikuwa na wasiwasi huu.

Ndugu yangu Vangi, kama huna homa hutoenda hospitali kutaka kupimwa homa - unless unaona baridibaridi. Hivyo wewe mwenyewe imekupitia kuenda hospitali ya wandawazimu kupima akili yako??? Haikupitikii, kwasababu huna wasiwasi wa akili yako, the day ukienda basi ujue ni tayari wewe mwandawazimu!!!
Hakuna anaemchukia. Ni Rais wetu halali. Yeye mwenyewe anaropokwa ovyo na sisi tunanukuu aliyoyasema yeye mwenyewe pale airport. Sio kama hatumuonei huruma. Tunamuonea huruma sana, lakini hatuna la kufanya. Kwahivyo, ukitaka hizi aibu zisitoke mueleze mwana-CCM mwanzio asiseme mambo kama haya nje na waandishi wa habari, na wala asiende nje ya nchi kwa mapimaji kama haya, kwani anatutia aibu sote!!!

La pili, unasema wapinzani waungane! Ni nani aliyekwambia wapinzani wa tanzania wapo kwa maslahi ya taifa? Ingekuwa hivyo siwangeshaungana siku nyingi? Hawana lolote hawa, na kuamini kwamba wapinzani wataleta ukombozi tanzania ni kujilisha upepo. Upinzani wa kweli utatoka CCM, angalieni mfano wa Kenya, wapinzani wa kweli walitoka KANU na hao ndiyo waliokuja na wazo la muungano, siyo hawa wanaoangalia tu masilahi yao. Mara ngapi wamejaribu kuungana wakashindwa? Ndo maana mwenzao Makamba anawaita mapaka, wanavutana mikia badala ya kumkabili panya. Wala hakuna tumaini lolote kwa hawa wapinzania wa bongo. porojo tu!

Hapo juu ninakubaliana na wewe kuhusu wapinzani wetu nchini na kwahivyo ni juu yetu tuwashawishi kwa faida ya nchi yetu
 
Nakupa tano!!
 
NANI ATAKUWA RAIS MUOKOZI WA TANZANIA??

Kwahivyo, tunapofikiria nani atatufaa - mtu yoyote kutoka CCM iwe out of our minds. Hata akitoka mbinguni, lakini akiwa
mwana-CCM basi mambo yatakuwa haya haya tu kama yalivyo
hivi sasa. Hii ni kwasababu ya system ya kubebana
ilivyo na sio kwasababu ya mtu mwenyewe alivyo.

Atakaeiokoa nchi hii ni Rais kutoka upinzani na sio kutoka CCM. Kwahivyo, badala ya kupeyana nambari za simu ili tumshawishi mtu fulani wa CCM agombee urais mwakani, ni bora tutumie nguvu zetu kuvishawishi vyama vya upinzani nchini vikubaliane kumuweka mtu mmoja kugombea urais. Wapinzani wakiungana CCM itaanguka na hapo ndipo tutakapopata muokozi wa kweli wa hili Taifa. Kutegemea fulani ni waziri machachari na hodari wa kazi yake kutoka CCM na atakuja kuliokoa Taifa ni sawa na kutokutumia akili zetu vizuri, kwani katika chaguzi zetu za Rais hapa Tanzania tunakichagua chama na sio mtu. Kwahivyo, CCM ikishinda urais na Rais mpya akawa anafanyakazi zake kinyume na system ya kubebana ya CCM ilivyo, definitely watamuweka upande na badala yake fisadi atawekwa kuwa Rais na mambo yataenda kama yalivyo hivi sasa!

Mkuu naukubali sana mtazamo wako, hasa kwa kipindi hiki cha pili ambacho muungwana anakitaka. Watanzania wenzangu, mimi naamini kuwa mtandao wa CCM unaweza kutuletea maendeleo kama tu sisi wananchi tutaonyesha tupo serious na tunamaanisha maendeleo. Tanzania inaweza kuendelea kwa kas ya ajabu na ikawa mfano, ili hili litokee, tunapaswa kuiweka CCM benchi kwa muda waonje radha ya kuwa wapinzani na wajue tumechukizwa na russhwa za aina zote! na hatutaki ujinga. Weka chama chochote cha upinzani (of course kwa kufuata ubora wao na potentials), wakirudi 2015 CCM kuomba kura nidhamu juu, na nchi itaendelea.

hata kama hao wapinzani wataonyesha kutusukuma mbele then we just forget CCM, and go ahead. lakini kwa staili ya kupeana vijiti kama relay CCM hawatupi maendeleo, watabinafsisha kila kitu na kuhakikisha watoto wao ndo wanabaki kwenye system na sisi wana JF na wengine tabaka la kati tutajikuta mmojammoja tunaondoka kujiunga na mafisadi at different levels individually! thats the death cause of our development route!
 
Wakuu,

Muokozi wa Tanzania ni sisi wenyewe, hakika kama tukikaa na kutafakari yote ambayo yametupita, tutaona kuwa ni sisi wenyewe "Watanzania" tumejifikisha mahali tulipo

Tunaweza kudai kuwa kuna walaghai, wala rushwa, watoa rushwa, na wengine wote walioturudisha nyuma, lakini wote hao bado tu, ni "Watanzania"

Hivyo basi kama "Watanzania" tujitutumue kwa njia zote tuweze kulinusuru taifa letu kutoka kwa wale miongoni mwetu ambao sifa zao haziendani na uzalendo au matakwa ya Wananchi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Itakuwa vizuri kuona tunampata Raisi ambaye hayumbishwi na mwenye msimamo madhubuti-ikiambatanishwa na ujasiri na maadili mazuri ya kazi. Huyu Raisi anaweza kupatikana pale sisi "Watanzania" tutakapo tumia mda wetu kuchagua kiongozi kwa uangalifu na siyo kwa kulaghawia na kanga na kofia.

Muokozi wa Tanzania ni wewe- ni sisi wote regardless of our indifferences!

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika
 
Lipumba anaweza kutuokoa tumuunge mkono, ni muadilifu, msomi na mkali atawadhibiti hawa mafisadi bila kuogopa.
 
Lampart,
Kama maneno yako yametoka moyoni, Mungu akubariki. Napata shida sana kuelewa jinsi nchi inavyoendeswa.
1. Sitaki kukili kuwa raisi mzuri hawezi kutoka CCM, ila napenda kusema tunahitaji kujua shida ya nchi hii ni Raisi.
2. Bahati mbaya sina chama, lakini naipenda sana Tanzania, na najihurimia na kuwahurumia watanzania hasa wanyonge.
3. Ni kweli kabisa kwamba solution ya tatizo hili iko mikononi mwa watanzania, je wanajua? kama hawajui watajuaje?
 
Lampart,
Kama maneno yako yametoka moyoni, Mungu akubariki.

Nd. Mtanzania,
Maneno hayo hapo juu yametoka deep from the bottom of my heart na ninakushukuru kwa baraka zako.
Mungu atubariki sote Watanzania!
 
Tanzania haita okolewa na siasa bali watu wenyewe kubadilika.

Watanzania tumebadilika vya kutosha!tulikuwa tunasomeshewa watoto wetu chuo kikuu bure kwa kodi zetu leo tunatoa mamilioni ili waende sekondari!

we have done our part candidly,sema hiki kiji-system(maana hakistahili hata kuitwa system-mwenye kinyume cha system anisaidie) kinatupoteza siku nenda rudi.

hakuna mtu anayeniudhi,personally kama yule anayewaambia watanzania maendeleo watajiletea wenyewe!ebo,ofcourse kila binadamu ana-struggle to be better,in vipi tutajieletea maendeleo wakati njia kuu za uchumi ziko taabani?

kuna faida gani kulima kahawa wakati utaiuza for 20% of the world market,the remaining 80% inaenda kwa madalali wanaosaidiwa na hii system mbovu?and you actually spent 19% of its total cost to produce it?

tunajitahidi "out of our skin" watanzania,sema tumekuwa kama abiria tunaoendeshwa na dereva mlevi.siku atakapongolewa dereva mlevi(raisi) na vibaraka wake,akaletwa yule muadilifu na mwenye nia ya dhati y akuwasaidia wananchi kuendelea,ndio siku Watanzania tutapata uhuru wetu wa kiuchumi,na kimaendeleo.
Until then our future is doomed.
 
Mimi nafikiri tusubiri mpaka watakao jitokeza ndipo tuweze kusema huyu ni bora zaidi ya mwingine, kwa sasa hivi tutaishia kuwataja hao hao mafisadi. tunao wajua kwa viwango tofauti au katika ile hali ya kusema afadhali ya huyu.
 
Raisi bora atatokea UWANJA WA FISI KINONDONI
Huyo ataweza kuiendesha nchi bila Tatizo
akija Raisi atakaeleta siasa nchi itamshinda, hapa tupate raisi kichaa pekeee ndie tutaondoka tulipo tuzame au tuokoke lakini ukileta za kuleta kata kichwa
 
Nakubaliana na wewe ndugu!!!
 
Back
Top Bottom