Jamani jamani nani atasaidia wanafunzi ktk chuo kikuu cha Tumaini kampasi ya Kurasini? Tusikimbilie neno UDINI. Mazingira ya kusomea ni mabaya sana hasa jioni. Ni vurugu mechi, kuna kwaya ya kanisa vyombo juu, wanamaombi nao sauti juu. Lakini la ajabu ni kuwa wanafunzi wanalipa ada 2.5M/= kwa mwaka. Walipojaribu kujitetea kwa kuhainisha mazingira yao mabovu, haraka chuo kikafungwa. Serikali ipo na wakaguzi wapo, iweje wanaridhia mazingira kama hayo? Au ndo fasheni ya ufisadi? Eloi utusaidie