G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Ukipita barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam baada ya mataa ya barabara inayoelekea Masaki pembeni ya bahari ya Hindi utakuta kuna kadaraja fulani hivi kanaunganisha kona moja na nyingine ambako kako mita chache sana kutoka barabara hiyo na kapo kando kidogo mwa bahari ya Hindi. Hili ndilo daraja la coco beach ambalo limenyanyuka mita chache sana kutoka usawa wa bahari.
Ukiangalia kwa umakini daraja hili basi unajikuta ukijiuliza maswali mengi sana na kama una hasira basi utaishia kutoa lugha za kuudhi kimawazo na hata kwa mdomo.
Unajiuliza ni nini hasa umuhimu wa daraja hili? Unakosa jibu! Unajiuliza ni nani hasa anagharamia? Unaishia kuomba Mungu zisiwe kodi zetu!
Daraja limejengwa pembeni kidogo mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi na hivi karibuni Rais Magufuli na ikulu yake watahamia Dodoma, balozi za Umoja wa Ulaya Canada, China na nyingine zote ambazo labda wao ndiyo hasa walengwa wa daraja hili hawatakuwepo tena.
Unajiuliza kama daraja litatumika kama kivutio cha utalii unarudi unaangalia jinsi ujenzi wake ulivyo, lilivyonyanyuliwa kutoka usawa wa bahari, umbali kutoka daraja hilo na nchi kavu ulivyokaribiana unajikuta ukikasirika tena.
Any way naona sasa tumekuwa "Dona Kantre" kiasi kwamba tunaweza kutumia fedha jinsi tunavyotaka maana zipo nyingi.
Wabunge pingeni na kataeni kujengwa kwa Daraja la Juu ya Bahari kutoka Coco Beach to Agakhan