Nani anayegharamia ujenzi wa daraja la Coco Beach? Kama taifa tumewekwa kwenye kapu la akili ndogo?

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,874
Ukipita barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam baada ya mataa ya barabara inayoelekea Masaki pembeni ya bahari ya Hindi utakuta kuna kadaraja fulani hivi kanaunganisha kona moja na nyingine ambako kako mita chache sana kutoka barabara hiyo na kapo kando kidogo mwa bahari ya Hindi. Hili ndilo daraja la coco beach ambalo limenyanyuka mita chache sana kutoka usawa wa bahari.

Ukiangalia kwa umakini daraja hili basi unajikuta ukijiuliza maswali mengi sana na kama una hasira basi utaishia kutoa lugha za kuudhi kimawazo na hata kwa mdomo.

Unajiuliza ni nini hasa umuhimu wa daraja hili? Unakosa jibu! Unajiuliza ni nani hasa anagharamia? Unaishia kuomba Mungu zisiwe kodi zetu!

Daraja limejengwa pembeni kidogo mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi na hivi karibuni Rais Magufuli na ikulu yake watahamia Dodoma, balozi za Umoja wa Ulaya Canada, China na nyingine zote ambazo labda wao ndiyo hasa walengwa wa daraja hili hawatakuwepo tena.

Unajiuliza kama daraja litatumika kama kivutio cha utalii unarudi unaangalia jinsi ujenzi wake ulivyo, lilivyonyanyuliwa kutoka usawa wa bahari, umbali kutoka daraja hilo na nchi kavu ulivyokaribiana unajikuta ukikasirika tena.

Any way naona sasa tumekuwa "Dona Kantre" kiasi kwamba tunaweza kutumia fedha jinsi tunavyotaka maana zipo nyingi.

Wabunge pingeni na kataeni kujengwa kwa Daraja la Juu ya Bahari kutoka Coco Beach to Agakhan
 
Nadhani umekurupuka, kwanza hilo daraja ni juhudi za Mh JK Kipenzi cha Watanzania, aliondoka akiwa tayari ameshaweka misingi na makubaliano kama lilivyo daraja la Mfugale.

Pili Unasema daraja liko liko chini au unaliita kidaraja.. nIkwambie tu kwamba yale ni matayarisho ya ujenzi tu na lile daraja unaloliona likiwekwa lile sio daraja halisi, ni njia tu ya wakandarasi kupitisha materials na nyenzo vilevile litatumika kama support wakati wa ujenzi wa daraja halisi

Tatu.. Unaijua foleni ya kutoka na kuingia mjini wakati wa asubuhi na jioni hapo selander na stanbic? Daraja hili ni muhimu sana kama tunataka kupunguza foleni ali Hassan Mwinyi Road.

Nne; Jiji la Dar es Salaam litaendelea kukua kwa kasi licha ya Serikali kuhamia Dodoma hivyo daraja hili bado ni muhimu sana
 
Ndo umeandika nini ndugu? Kama huoni umuhimu wa hilo daraja basi utakuwa ni taahira
Mimi pia taahira, lakini mwenye subira maana ya Mungu mengi.

Kilipotangazwa kikokotoo cha 25% napo nilikuwa taahira, lakini kama nilivyosema, Ya Mungu Mengi...juu ya kikokotoo mimi si taahira tena.

Hii awamu imejaa matumaini yenye kuthibitika kabla ya jua kupambazuka, maana hata Ubungo pambazuko limeonekana. Mkandarasi kaweka round about ili atujengee flyover...mashallah! Foleni imeondoka na round hata kabla flyover haijaonesha dalili.

Waarabu wanasema: Inna allahu maaswabirinah...acha leo niwe taahira :D:D:D
 
Brother Kuna vitu vinakera Sana kwenye nchi hii ukivifuatilia sana utapata BP, KISUKARU na magonjwa mengine ya hatari wacha wafanye yao tu linchi liende ende hivyo hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kunamuda watukama nyny na wenyeakili kamazenu mnahitaji kupuuzwa.

Kabla ujaandika mada jaribu kutafuta undani wa hiyo mada au hoja yako..na sio kuanza kulialia kijinga.

Nakusaidia: tafuta taharifa ya huo mradi wa daraja utapata majibu yote kisha jifunze
 
Kwa kweli sielewi mantiki ya kujenga lile daraja pale hata kama ni sababu ya utalii na kupendezesha jiji hapana kwanza eneo ni chafu na kunanuka, hapokuwa ninatambua jitihada za serikali kuboresha miundo mbinu ya jiji ndani ya miaka kumi ijayo dar es salaam itakuwa kama Seoul, Korea
 
Nadhani umekurupuka, kwanza hilo daraja ni juhudi za Mh JK..Kipenzi cha watanzania, aliondoka akiwa tayari ameshaweka misingi na makubaliano kama lilivyo daraja la Mfugale...

Pili Unasema daraja liko liko chini au unaliita kidaraja.. nIkwambie tu kwamba yale ni matayarisho ya ujenzi tu na lile daraja unaloliona likiwekwa lile sio daraja halisi, ni njia tu ya wakandarasi kupitisha materials na nyenzo vilevile litatumika kama support wakati wa ujenzi wa daraja halisi

Tatu.. Unaijua foleni ya kutoka na kuingia mjini wakati wa asubuhi na jioni hapo selander na stanbic? Daraja hili ni muhimu sana kama tunataka kupunguza foleni ali Hassan mwinyi road.

Nne; Jiji la Dar es salaam litaendelea kukua kwa kasi licha ya Serikali kuhamia Dodoma hivyo daraja hili bado ni muhimu sana
Daraja hili halina umuhimu wowote, gharama zake bora wangevunja police surrender na kupanunua lililopo kwani ndio kikwazo. Magari yatokayo oceans yakiungana na mhimbili tayari foleni. Bora wangejenga interchange mchezo ungeisha
 
Mh. Rais JPM mtukufu tukumbuke kutuwekea barabara ya rami kakipande kaa kkk ikuti ileje isongole nasi ni watanzania pia japo hatupo Dar.
 
Mimi pia taahira, lakini mwenye subira maana ya Mungu mengi.

Kilipotangazwa kikokotoo cha 25% napo nilikuwa taahira, lakini kama nilivyosema, Ya Mungu Mengi...juu ya kikokotoo mimi si taahira tena.

Hii awamu imejaa matumaini yenye kuthibitika kabla ya jua kupambazuka, maana hata Ubungo pambazuko limeonekana. Mkandarasi kaweka round about ili atujengee flyover...mashallah! Foleni imeondoka na round hata kabla flyover haijaonesha dalili.

Waarabu wanasema: Inna allahu maaswabirinah...acha leo niwe taahira :D:D:D
Hata ziliponunuliwa ndege mlisema hazina maana. leo hii ndio mnazitumia. tulipojenga barabara za mwendokasi mlibeza. leo hii mnafurahia. tunafanya maendeleo kwa wapenda maendeleo na si ninyi msio na mwelekeo
 
Hata Mimi huwa sipati picha watawala wetu wanawaza nini? Hivi Kuipanua Ally Hassani Mwinyi kuwa njia nne kila upande si ingekuwa option nzuri zaidi kuliko kujenga hili Daraja uchwara? Tena daraja lenyewe ni two lanes
 
Hata ziliponunuliwa ndege mlisema hazina maana. leo hii ndio mnazitumia. tulipojenga barabara za mwendokasi mlibeza. leo hii mnafurahia. tunafanya maendeleo kwa wapenda maendeleo na si ninyi msio na mwelekeo
Hapo sawa, nilidhani unataka kusema zimeingiza faida.
 
Hata ziliponunuliwa ndege mlisema hazina maana. leo hii ndio mnazitumia. tulipojenga barabara za mwendokasi mlibeza. leo hii mnafurahia. tunafanya maendeleo kwa wapenda maendeleo na si ninyi msio na mwelekeo
Watu wengine mnapaswa kuhurumiwa tu-Watu kuzitumia hizo ndege au mwendokasi haimanishi maamuzi za kuzinunua hayakuwa ya Kipuuzi? Kwangu mimi Ujenzi wa aina ile wa Mwendo kasi ilikuwa ni Upuuzi. Hivi Ukiacha Joberg-SA tena maeneo machache-Kuna nchi nyingine Duniani imejenga barabara kama kwetu?
 
Ukipita barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam baada ya mataa ya barabara inayoelekea Masaki pembeni ya bahari ya Hindi utakuta kuna kadaraja fulani hivi kanaunganisha kona moja na nyingine ambako kako mita chache sana kutoka barabara hiyo na kapo kando kidogo mwa bahari ya Hindi. Hili ndilo daraja la coco beach ambalo limenyanyuka mita chache sana kutoka usawa wa bahari.

Ukiangalia kwa umakini daraja hili basi unajikuta ukijiuliza maswali mengi sana na kama una hasira basi utaishia kutoa lugha za kuudhi kimawazo na hata kwa mdomo.

Unajiuliza ni nini hasa umuhimu wa daraja hili? Unakosa jibu! Unajiuliza ni nani hasa anagharamia? Unaishia kuomba Mungu zisiwe kodi zetu!

Daraja limejengwa pembeni kidogo mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi na hivi karibuni Rais Magufuli na ikulu yake watahamia Dodoma, balozi za Umoja wa Ulaya Canada, China na nyingine zote ambazo labda wao ndiyo hasa walengwa wa daraja hili hawatakuwepo tena.

Unajiuliza kama daraja litatumika kama kivutio cha utalii unarudi unaangalia jinsi ujenzi wake ulivyo, lilivyonyanyuliwa kutoka usawa wa bahari, umbali kutoka daraja hilo na nchi kavu ulivyokaribiana unajikuta ukikasirika tena.

Any way naona sasa tumekuwa "Dona Kantre" kiasi kwamba tunaweza kutumia fedha jinsi tunavyotaka maana zipo nyingi.
Katika miradi ya kipumbavu iliyowahi kufanyika hapa nchini ni daraaja ya Cocbeach.

Halin tofauti naa darja la miti. Binafai sitaki kuamiji kuwa kile ninachokiona ndio darja analoshabikia Magufuli.

Ni afadhali ingepnuliwa lile la Seranda kuliko kihenga kidarha kingine kidogo karibu na daraja la zamani.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom