Ujenzi wa Daraja la Berega wafikia asilimia 68 kukamilika

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
UJENZI WA DARAJA LA BEREGA WAFIKIA ASILIMIA 68 KUKAMILIKA

Na. Geofrey A. Kazaula, Morogoro.

Ujenzi wa Daraja la Berega katika barabara ya Berega-Dumbalume Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro unaotekelezwa chini ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umefikia asilimia 68 kukamilika.

Ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa mita 140 na upana wa mita 11 linalounganisha Wilaya ya Kilosa, Gairo, Kiteto na Wilaya ya Kilindi linakusudia kuondoa kero ya muda mrefu ya usafiri na usafirishaji na kuwezesha wananchi kuendesha shughuli za kijamii na kiuchumi.

Akizungumza katika mahojiano maalum, Meneja wa TARURA Mkoa wa Morogoro Mhandisi Benjamin Maziku ameeleza kuwa mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 68 ya utekelezaji na watahakikisha wanamsimamia Mkandarasi kumaliza ujenzi wa daraja hilo Kwa wakati.

‘‘Tunaendelea kumsimamia mkandarasi ili kazi hii ikamilike kwa muda ili wananchi waweze kupata huduma kama yalivyo malengo ya Serikali”, alisema Mhandisi Maziku.

Aidha, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga shilingi bilioni 8 ili kuwezesha mradi huo kutekelezwa ambapo mradi huo pia umetoa ajira kwa wananchi takribani 150.

‘‘Mradi huu ni muhimu sana kwani ukikamilika utawezesha wananchi kufikia hospitali ya Berega katika kupindi chote cha mwaka na utarahisisha shughuli za kiuchumi kufanyika, hizi ni jitihada za serikali ya awamu ya sita baada ya kutafuta fedha na kuona umuhimu wa Daraja hili kwa wananchi.’’ alisema Mhandisi Maziku.

Naye Mkazi wa kijiji cha Berega, Ndugu Tina Muhumba ameishukuru Serikali kupitia TARURA kwa ujenzi wa daraja jipya la Berega ambalo litawasaidia wakulima kusafirisha mazao yao kuelekea kwenye masoko mbalimbali.

“Wakati wa mvua daraja hili hujaa maji na kukata mawasiliano baina ya wananchi wa Wilaya nne ambapo wengi wetu ni wakulima na tunatumia daraja hili kusafirisha mazao yetu hasa mbaazi ambazo tunalima sana huku, hivyo tumefurahi kuletewa daraja jipya kwani litakapoisha litatusaidia kusafirisha mazao yetu sokoni kwa urahisi”, alisema Tina.

Ndugu Sylvester Anderson, Mkazi wa Kijiji cha Berega ameipongeza Serikali kwa ujenzi wa daraja hilo ambalo litawasaidia wananchi wa Kata ya Berega, Kiegeya na maeneo jirani kuvuka kwa urahisi na kufikia huduma za kijamii na pia kupitia ujenzi wa daraja hilo ajira zimeweza kupatikana kwa wananchi wa maeneo hayo.

Ujenzi wa Daraja la Berega unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Juni 2023 na kuondoa kero ya muda mrefu kwa wakazi wa maeneo hayo hasa katika kipindi cha masika ambapo wananchi walikosa mawasiliano na kushindwa kupata huduma za kijamii.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA unaendelea kutekeleza miradi katika maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha wananchi wanafika kusiko fikika na wanafanya shughuli zao za kiuchumi kwa urahisi.

IMG-20221220-WA0079.jpg
IMG-20221220-WA0080.jpg
 
View attachment 2452608View attachment 2452609
Hapo tutaambiwa daraja la Tillion mbili na linajikunja na kukunjuka.
 
Back
Top Bottom