Nani anavikumbuka na alisoma hivi vitabu?

Nani anavikumbuka na alisoma hivi vitabu?

Wakuu nani anaukumbuka ule wa kingereza wa I wrote a letter to my darling. Nimeusahau unavyoendelea.
 
Wakuu nani anaukumbuka ule wa kingereza wa I wrote a letter to my darling. Nimeusahau unavyoendelea.

Nakumbuka kuna mchezo wa kuigiza waliimba hivi. .

I wrote a letter to my father, but he did not answer me. ..
I don't know what is the matter?
Who is knocking the door,
Sister is knocking the door
Brother is knocking the door always. ..
 
Mwenzenu nimemkumbuka jamaa yangu ni muhusika anaitwa...ANDUNJE.!
 
Kibibi jitu...pazi na jogoo..hekaya za esopo..hadithi za kikwetu...safari ya bulicheka
 
vingine ni simu ya kifo, alfu lela ulela, adili na nduguze, pinnochio, safari za sindbad, kisiwa cha hazina, nk
 
Lindi amuokoa Kapilima.

Chilunda apambana na chui

......Ilikua usiku wa mawingu ya mvua chilunda alipopambana na chui. Alikua akitoka kijijini kwao...
 
KAMA UNATAKA MALI...
karudi baba mmoja toka safari ya mbal
kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili....

juma na uledi..
awafu mwenye nguvu..
jogoo wa ajabu..
fikiri kabla ya kutenda...
 
Ila tuache masiala enzi hizo au enzi zetu elimu ilikuwa juu sana. Hebu jiulize wangetuwekea ufaulu wa hadi jumla ya alama ziwe 70 ufaulu ungekuwaje enzi zetu?
 
Wakuu nani anaukumbuka ule wa kingereza wa I wrote a letter to my darling. Nimeusahau unavyoendelea.

I wrote a letter to my darling, but she didn't answer me*2 I don't know what is the matter matter*2 Who is knocking the door,sister knocking the door*2 Brother knocking the door always*2
Mhh! Nilikuwa la kwanza miaka hiyo.
 
Wakuu nani anaukumbuka ule wa kingereza wa I wrote a to my darling. Nimeusahau unavyoendelea.

I wrote a latter to my darling but she didn't answer me
I don't know what is the matter matter
Who is knocking at the door*2 Marry is knocking at the door welcom
!????!?
 
Dah! Mi mwenzenu shuleni nilikuwa kiraza, yaani ninavyosoma hapa ndio napata picha kwa sababu picha ndio ilikuwa staili yangu ya kusoma.
Nilikuwa na uwezo wa kusoma kile kitabu cha TUJIFUNZE LUGHA YETU kwa mtindo wa picha kuanzia heading ya kwanza hadi mwisho. Yaani nikiiona title tu, najua hii imeandikwa hivi kwa mfano MSEMAKWELI ACHAGULIWA KUWA DIWANI, SAFARI YENYE MKOSI, CHILUNDA ASHAMBULIWA NA FISI nk.
Kuna muda nilikuwa nawapungia mkono wanaojua kusoma, mm nikiona tu ule muundo wa yale maandishi, basi najua hapa pameandikwa hivi kwa hiyo natamka tu bila kubabaika na wanafunzi wanapiga tu makofi huku wengine wakisoma kwa kurudia rudia.
Na kweli ni slow learner,yaani hadi la tatu hujui kusoma,leo uko mtandaoni. Historia yako inafaa kuifahamu,
 
Back
Top Bottom