Nkerebhuke
JF-Expert Member
- Nov 1, 2021
- 796
- 2,027
Kwa heshima na taadhima naomba kuwakaribisha wanazuoni wa mambo ya vita, watafiti na wajuvi wa siasa za kimataifa kutoa elimu kuhusu nani anashinda kwenye uwanja wa medani ndani ya ukraine. Kama wewe sio mjuzi wa mambo ya medani yanayojumuisha, silaha, askari, uchumi, propaganda, mbinu na mipango ya vita tafadhari usilete ushabiki ukaharibu uzi.
Ushindi ndani ya uwanja wa vita (medani) ni jambo tata sana pale vita inapokabiliwa na propaganda nyingi sana kuliko kuupata ukweli wenyewe kutoka mstari wa mbele. Russia ni taifa kubwa sana kijeshi kulinganisha na mataifa mengi ulimwenguni hivyo kampeni yake ya kijeshi ndani ya ukraine kumeibua hisia za watu wengi sana mpaka huku kwetu Tanzania. Je jeshi la Russia limefanikiwa kuharibu na kuvunja nguvu ya jeshi la ukraine?, Je ukaraine wamefanikiwa kiasi gani kulinda nchi yao dhi ya invaders?
Pia naomba wajuzi wa mambo ya vita watoe elimu kuhusu utofauti wa na propaganda na fake news kwani wengi inaonekana hawajui maana ya propaganda ndani na nje ya uwanja wa medani.