Nani anasema CHADEMA ni Imara kiasi Hicho !?

Nani anasema CHADEMA ni Imara kiasi Hicho !?

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,198
Reaction score
7,539
CHADEMA iko imara maana yake nini?

Hivi kwanza CHADEMA ni nini hasa?

Hivi tunajua CHADEMA ni wazo tu!? Na wazo huwa ndani ya watu, hivyo wazo hilo huonekana kupitia matendo ya wale ambao wazo lipo ndani yao? Hivi tunajua CHADEMA ni mimi na wewe?

Chama cha siasa ni wazo tu na sio kitu yabisi ambacho kimewekwa mahali. Inashangaza sana mimi na wewe tukiwa tunasema mara kwa mara kwamba CHADEMA ni imara hali mimi na wewe hatujafanya wala hatufanyi chochote cha maana kuuweka uimara huo. Tunazungumza kana kwamba CHADEMA ni kitu "Concreate" ambacho kipo mahala na kipo "Constant".

Yatupasa tufahamu kwamba CHADEMA ni mimi na wewe, na matendo yetu ndio yanayotoa taswira ya kwamba CHADEMA ni nini, CHADEMA ni imara au ni dhaifu n.k. Kusema tu CHADEMA ni imara wakati mimi na wewe hatuna kitu chochote cha maana tunachokifanya ili kuleta au kuhakikisha uimara huo unadumu, si sahihi hata kidogo.

Jiulize hapo ulipo mpaka sasa ni nini umefanya ili kudhihirisha au kuchangia huo uimara wa CHADEMA? Kama hamna ulichofanya na hamna unachofanya, basi badilika haraka na chukua hatua 2014. Elewa CHADEMA ndio wewe! Na kuwajibika na kujituma kwako, ndio kutaifanya CHADEMA iwe imara na kinyume chake!

Elewa! Mimi na wewe tukiwa na mshikamano kwenye mambo ya msingi huo ndio uimara na taswira ya CHADEMA na tukiwa tunagawanyika gawanyika ndio udhaifu wa CHADEMA, na matendo huzungumza zaidi ya maneno.

Elewa! Tukiwa tunaonesha uwezo wetu katika kudhibiti na kutatua migogoro ndani na nje yetu huo ndio uimara wetu na tukiwa tunashindwa kufanya hivyo ndio udhaifu wetu, na matendo yanaongeea zaidi ya maneno.

Elewa! Tukiwa tunaongea hoja za msingi kila mara ndio uimara wetu na tukiwa tunaongea mambo tu ili mradi ndio udhaifu wetu, na matendo huzungumza zaidi ya maneno!.

Elewa! Tukionesha jazba (udhaifu) ndio tunaonesha taswira ya chama na tukionesha hekima (uimara)ndio tunaonesha taswira ya chama na matendo huzungumza zaidi ya maneno!

Elewa! Tukionesha chuki na visasi katika jamii yetu ndio tunaonesha taswira ya chama (udhaifu) na tukionesha busara na ustaarabu (uimara) tunaonesha taswira ya chama vile vile!

Elewa! Tukiwa tunatenda uadilifu katika jamii zetu tunatoa taswira ya chama chetu katika muelekeo huo na kinyume chake.

Haiingii akilini na wala haina maana kusikia mke na mume wanapigishana kelele mara kwa mara ndani ya nyumba mara chupa zinarushwa halafu wakitoka nje wanasema "ndoa yetu imara ati" matendo yanaongea zaidi ya maneno! (ni mfano tu jamani). Na mimi na wewe ndio tunaamua tufanye nini ili tutoe taswira gani!

Wakati tunafunga mwaka, wewe unayesema CHADEMA ni imara, jiulize, umetoa mchango gani katika uimara huo au wewe mwenyewe ni imara kiasi gani na katika jambo gani! Kwa sababu CHADEMA ni mimi na wewe. Zaidi ya hapo mimi niseme CHADEMA si imara kama ambavyo tunazungumza. Tunatakiwa tuiimarishe 2014 vilivyo kwa matendo, na ni mimi na wewe na wala sio fulani na fulani!.

Uimara wako +uimara wangu + uimara wa jamaa= uimara wa chama

Udhaifu wako+ Udhaifu wangu+ Udhaifu wa jamaa = udhaifu wa chama.

CHADEMA ni chama kimeanzishwa kisheria na kinakuwa kwa maana kinapata wanachama wapya wengi hadi vivjijini, ila kinaandamwa sana na mamluki,wanafiki wengi wamejiunga wakati akilizao bado ziko CCM, CCM wenywewe wamekikaba koo kweli kweli chama chetu wanakihujumu usiku na mchana akina Ngulu Nchemba, Chris Lukosi kutwa kucha ni kukihujumu tu chama chetu hadi kuonekana kama vile siyo chama madhubuti

Mimi nilichofanya ni kukata kadi, kushona NGUO za chama pair nyingi na kutoa usafiri pikipiki yangu XL Japan kwenda vijijini kuratibu uhai wa chama ngazi za kaya na kuyazomea Ma-CCM kiasi yakivaa manguo yao yanaonekana kama yamejipaka mavi.
 
chadema ni hawa apa,yan hali hii

kutoka
Z
kwenda
images
hadi apa
2Q==

sasa usaliti wa namna hii alafu nikusikilize unachoniambia,Je nitajuwa ninaakili timamu?
Tuamke waTZ tunadanganywa tu na izi siasa,hakuna aliye uchungu na nchi hii bali wanatafuta namna ya kuuza i nchi
 
CCM imeipaisha CDM kwa njia zifuatazo:
1. Kwa kuwapiga mabomu mara kwa mara.
2. Kwa kukitamka kila mkutano au matamko ya CCM,
3. Kwa kufanya mauaji ya mara kwa mara (CDM inapata public sympthy),
4. Kwa kuonesha hofu kuwa CDM inaweza kuchukua madaraka,
5. Kwa kutoa utabiri kuwa CDM itakufa huku hakuna lolote linalotokea,,
6. Kwa kupiga propaganda za udini, ukabila na ukanda (hii strategy ilifanikiwa sana kwa upande wa CUF lakini kwa CDM hali ni tofauti sana),
7. Kwa kuwatumia masalia na wasaliti ndani ya CDM ambao hugundulika kirahisi!
8.....
 
uadilifu ni kutembea na wake za watu?
Msikamano ni kutaka kuanzisha taifa la kaskazini?
Hoja za msingi ni kuhalalisha gongo?
Unazungumzia cdm hii nayoifaham au labda sijakuelewa?
 
betlehem umekusanya maneno meeeengi mpaka naogopa, point yako hapo ni hii, unataka tuimiliki chadema, hili ni kosa kubwa kuwahi kutokea.

Ni kweli kwamba "ni wazo"
ikiwa wazo hili ni zuri na lina manufaa kwa jamii na linatekelezeka basi wajibu wetu ni kuliunga mkono "hili wazo" kulieneza "hili wazo" kulilinda "hili wazo" lakini zaidi sana kuwa tayari kulitekeleza "hili wazo"

Ni kosa kubwa kufikiria kulimiliki "hili wazo"
 
Last edited by a moderator:
CCM imeipaisha CDM kwa njia zifuatazo:
1. Kwa kuwapiga mabomu mara kwa mara.
2. Kwa kukitamka kila mkutano au matamko ya CCM,
3. Kwa kufanya mauaji ya mara kwa mara (CDM inapata public sympthy),
4. Kwa kuonesha hofu kuwa CDM inaweza kuchukua madaraka,
5. Kwa kutoa utabiri kuwa CDM itakufa huku hakuna lolote linalotokea,,
6. Kwa kupiga propaganda za udini, ukabila na ukanda (hii strategy ilifanikiwa sana kwa upande wa CUF lakini kwa CDM hali ni tofauti sana),
7. Kwa kuwatumia masalia na wasaliti ndani ya CDM ambao hugundulika kirahisi!
8.....
Wewe binafsi umefanya nini?
 
Ni kweli kwamba "ni wazo"
ikiwa wazo hili ni zuri na lina manufaa kwa jamii na linatekelezeka basi wajibu wetu ni kuliunga mkono "hili wazo" kulieneza "hili wazo" kulilinda "hili wazo" lakini zaidi sana kuwa tayari kulitekeleza "hili wazo"

Ni kosa kubwa kufikiria kulimiliki "hili wazo"
Nijuavyo mimi chama kinamilikiwa na wanachama na hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa.Au mmiliki wa chama anatakiwa kuwa nani kwa uelewa wako? hayo unayoyazungumzia hapo juu inaonesha wazi kwamba tuko pamoja.Kila mtu akiyafanya uliyoyataja hapo juu sasa ndio tunaweza kusema chama ni imara hasa!
 
Hivi nani alichagua wabunge wa viti maalum Chadema.
 
chadema ni hawa apa,yan hali hii

kutoka
Z
kwenda
images
hadi apa
2Q==

sasa usaliti wa namna hii alafu nikusikilize unachoniambia,Je nitajuwa ninaakili timamu?
Tuamke waTZ tunadanganywa tu na izi siasa,hakuna aliye uchungu na nchi hii bali wanatafuta namna ya kuuza i nchi

Ccm wameiba mpaka leo hatuna nafuu, tuwape na wengine hata kama watakuwa vile vile fain la msingi ni kugawana umasikini au utajiri wa nchi yetu....sio kila siku ccm wananenepeana kiasi kwamba wanataka kupasuka
 
Hivi nani alichagua wabunge wa viti maalum Chadema.
Kesho ni mwaka mpya.Tunaangalia mbele.Yanyuma yatakusaidia nini! wewe jiulize unaanza je mwaka mpya kwa kufanya mambo mazuri zaidi ya yale yaliyopita sio kurudi kinyume nyume.Wakati wazungu walitengeneza computer kubwa, wakaboresha wakapata desk top,muda ulivyoenda wakaibuka na laptop na wanazidi kuporesha kila mwaka, sisi tunawaza tu hivi computer ya kwanza ilikuwa je vile!!
 
pole sana chadema ndio maisha yako lakini bado unaimba melody zenye tune tofauti utashangaa na maisha yako
 
betlehem
Kama wewe hauko Imara sisi wenzio tuko imarq na tunazidi kujenga chama.
Tunashukuru kwa kukiri kwako kuwa wewe ni dhaifu na goi goi na huwezi kuwa na thaman yeyote ndani ya CHADEMA.
inshort haujawahi kuwa Mwanachama wa CHADEMA aisee.
Utahangaika sana na 2013 ndo hiyo inaoishia zake.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Nijuavyo mimi chama kinamilikiwa na wanachama na hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa.Au mmiliki wa chama anatakiwa kuwa nani kwa uelewa wako? hayo unayoyazungumzia hapo juu inaonesha wazi kwamba tuko pamoja.Kila mtu akiyafanya uliyoyataja hapo juu sasa ndio tunaweza kusema chama ni imara hasa!

Ukitaka kumiliki chama, unakianzisha wewe kwa gharama zako mwenyewe, unatushawishi tukuunge mkono kupitia katiba ya chama chako na sera zako. Tukikuunga mkono unapewa usajili kuendesha michakato ya siasa, ukituzingua hatukupokonyi chama chako, tunaondoa mkono tuliokuunga, ukikuta mtu anataka kumuondoa aliyekianzisha chama kwenye chama chake ujue huyo ni mjinga hata kama ana degree ya uzamivu.
 
Back
Top Bottom