Nani anasema CHADEMA ni Imara kiasi Hicho !?

Nani anasema CHADEMA ni Imara kiasi Hicho !?

CHAMA CHA MOB POLITICS? uimara utatoka wap????.... chama chenye mfumo wa anachy?????..... kamwe hatutafika 2angalie chama chenye mfumo wa DEVELOPMENTAL DEMOCRATIC STATE..... hakuna chama imara kama CCM, huo upepo2 utavuma na utapita... NCCR leo hi wako wap????
 
CHADEMA iko imara maana yake nini?

Hivi kwanza CHADEMA ni nini hasa?

Hivi tunajua CHADEMA ni wazo tu!? Na wazo huwa ndani ya watu, hivyo wazo hilo huonekana kupitia matendo ya wale ambao wazo lipo ndani yao? Hivi tunajua CHADEMA ni mimi na wewe?

Chama cha siasa ni wazo tu na sio kitu yabisi ambacho kimewekwa mahali. Inashangaza sana mimi na wewe tukiwa tunasema mara kwa mara kwamba CHADEMA ni imara hali mimi na wewe hatujafanya wala hatufanyi chochote cha maana kuuweka uimara huo. Tunazungumza kana kwamba CHADEMA ni kitu "Concreate" ambacho kipo mahala na kipo "Constant".

Yatupasa tufahamu kwamba CHADEMA ni mimi na wewe, na matendo yetu ndio yanayotoa taswira ya kwamba CHADEMA ni nini, CHADEMA ni imara au ni dhaifu n.k. Kusema tu CHADEMA ni imara wakati mimi na wewe hatuna kitu chochote cha maana tunachokifanya ili kuleta au kuhakikisha uimara huo unadumu, si sahihi hata kidogo.

Jiulize hapo ulipo mpaka sasa ni nini umefanya ili kudhihirisha au kuchangia huo uimara wa CHADEMA? Kama hamna ulichofanya na hamna unachofanya, basi badilika haraka na chukua hatua 2014. Elewa CHADEMA ndio wewe! Na kuwajibika na kujituma kwako, ndio kutaifanya CHADEMA iwe imara na kinyume chake!

Elewa! Mimi na wewe tukiwa na mshikamano kwenye mambo ya msingi huo ndio uimara na taswira ya CHADEMA na tukiwa tunagawanyika gawanyika ndio udhaifu wa CHADEMA, na matendo huzungumza zaidi ya maneno.

Elewa! Tukiwa tunaonesha uwezo wetu katika kudhibiti na kutatua migogoro ndani na nje yetu huo ndio uimara wetu na tukiwa tunashindwa kufanya hivyo ndio udhaifu wetu, na matendo yanaongeea zaidi ya maneno.

Elewa! Tukiwa tunaongea hoja za msingi kila mara ndio uimara wetu na tukiwa tunaongea mambo tu ili mradi ndio udhaifu wetu, na matendo huzungumza zaidi ya maneno!.

Elewa! Tukionesha jazba (udhaifu) ndio tunaonesha taswira ya chama na tukionesha hekima (uimara)ndio tunaonesha taswira ya chama na matendo huzungumza zaidi ya maneno!

Elewa! Tukionesha chuki na visasi katika jamii yetu ndio tunaonesha taswira ya chama (udhaifu) na tukionesha busara na ustaarabu (uimara) tunaonesha taswira ya chama vile vile!

Elewa! Tukiwa tunatenda uadilifu katika jamii zetu tunatoa taswira ya chama chetu katika muelekeo huo na kinyume chake.

Haiingii akilini na wala haina maana kusikia mke na mume wanapigishana kelele mara kwa mara ndani ya nyumba mara chupa zinarushwa halafu wakitoka nje wanasema "ndoa yetu imara ati" matendo yanaongea zaidi ya maneno! (ni mfano tu jamani). Na mimi na wewe ndio tunaamua tufanye nini ili tutoe taswira gani!

Wakati tunafunga mwaka, wewe unayesema CHADEMA ni imara, jiulize, umetoa mchango gani katika uimara huo au wewe mwenyewe ni imara kiasi gani na katika jambo gani! Kwa sababu CHADEMA ni mimi na wewe. Zaidi ya hapo mimi niseme CHADEMA si imara kama ambavyo tunazungumza. Tunatakiwa tuiimarishe 2014 vilivyo kwa matendo, na ni mimi na wewe na wala sio fulani na fulani!.

Uimara wako +uimara wangu + uimara wa jamaa= uimara wa chama

Udhaifu wako+ Udhaifu wangu+ Udhaifu wa jamaa = udhaifu wa chama.


IJ UKAINGNISHA KMWE CHADEMA NA saccos YA wama YA KIKWETES TERRITORY FOR MONEY MOBILISATIN TAFADHARI BE NFORED KWMA mWGULU NAWENYEKITI WA HAMA CHAKE WATPATAAJIU YATAKAYO WAHUNT FOR LIFE BAADO MIEZI CHINI YA 24 THEY WILL BE NOTHING WHAT SO EVER LEGACY YO NI DHULUMA
 
Back
Top Bottom