Nani analipia hizi kesi za akina Lema?

Nani analipia hizi kesi za akina Lema?

Ni kwamba hizi gharama ambazo wabunge au madiwani haswa wa CHADEMA, wanapotumia midomo yao kuropoka na kwenda kinyume cha sheria na kukamatwa na polisi na kuswekwa ndani, baadae wanakuja mawakili wa chama, kushughulikia kesi zao;

Swali
(a). Hizi gharama huwa zinalipwa na CHADEMAau wao wenyewe watuhumiwa
(b). Kama kinalipa chama ina maana ndo huwa kinawatuma?

Tuchukulie kesi ya Lema na Tundu Lisu hizi gharama zinagharamiwa na CHADEMA?
hivyo ndivyo wajanja wanavyokula hela ya ruzuku cdm. kesi za kujitakia halafu kampuni za kina lissu na wenzake zinaingia kazini. ingekua wanalipa wenyewe lema asingejilipua ovyo kila siku. ni mtazamo wangu its very likely ndio hivyo.
 
kesi ya jinai inafunguliwa na jamhuri hivyo jamhuri ndo inalipia gharama zake. mtuhumiwa analipia gharama za wakili wake na kama hana uwezo basi anapewa na mahakama na hiyo gharama inalipwa na jamhuri
ok kesi za chadema zote zinagharamikiwa nao. kwanza watasema hawana imani na wakilu wa serikali.
 
wewe ndo upo vinywani mwao? achana na ubishi wa kisiasa, kuwa mwepesi kujifunza ufahamu wako upanuke zaidi
 
NARUDIA

kesi ya jinai inafunguliwa na jamhuri hivyo jamhuri ndo inalipia gharama zake. mtuhumiwa analipia gharama za wakili wake na kama hana uwezo basi anapewa na mahakama na hiyo gharama inalipwa na jamhuri
 
The same question applied to u, "Hivi hawa wanaowakamata hao watu uliowata kisha wanashindwa kuthibitisha makosa yao mahakamani hivi huwa wanatumia fedha za walipakodi wa Tz au kuna chama au kikundi fulani kinawatuma kufanya hivyo?
Kama ni zetu walipa kodi huwa zinaidhinishwa na bunge?
Mfano, mtuhumiwa anakamatwa Singinda anasafirishwa kwa helkopita hadi dar kwa gharama za nani?
 
Hpana mkuu hapa hatuongelei mtu kuuawa ila personal issue au private issue zishughulikiwe kibinafsi lkn cyo chama kugharamia..
Naona umeshajibu kuwa chama ndio kinalipa bila ushahidi.
Unataka kujua? Jiunge na Chadema kisha gombea uongozi ili ushiriki vikao vitakavyo kupa nafasi ya kujua au kuhoji mambo ya ndani.
Ila naomba nikufahamishe wewe na wengine, mawakili wale wa chama ni mawakili binafsi na wana ofisi zao hivyo sio kila ukimuona mahakamani basi anashughulikia chama hata wewe ukimuhitaji unampata tuu.
Na wakili yeyote anao uhuru wa kutetea kesi hata kwa kujitolea kulingana na maslahi yake.
Jee wewe ulitegemea Lema akiwa na kesi amtumie Lamwai?
 
Ni kwamba hizi gharama ambazo wabunge au madiwani haswa wa CHADEMA, wanapotumia midomo yao kuropoka na kwenda kinyume cha sheria na kukamatwa na polisi na kuswekwa ndani, baadae wanakuja mawakili wa chama, kushughulikia kesi zao;

Swali
(a). Hizi gharama huwa zinalipwa na CHADEMAau wao wenyewe watuhumiwa
(b). Kama kinalipa chama ina maana ndo huwa kinawatuma?

Tuchukulie kesi ya Lema na Tundu Lisu hizi gharama zinagharamiwa na CHADEMA?
|Hebu uliza maana ingekuwa Chama kingine kinafanya hivi UKUTA ungekwishajengwa. ndio maana watu wanakuwa na viburi wanatukana watu hovyo wakijua chama kitawabeba!
 
Naona umeshajibu kuwa chama ndio kinalipa bila ushahidi.
Unataka kujua? Jiunge na Chadema kisha gombea uongozi ili ushiriki vikao vitakavyo kupa nafasi ya kujua au kuhoji mambo ya ndani.
Ila naomba nikufahamishe wewe na wengine, mawakili wale wa chama ni mawakili binafsi na wana ofisi zao hivyo sio kila ukimuona mahakamani basi anashughulikia chama hata wewe ukimuhitaji unampata tuu.
Na wakili yeyote anao uhuru wa kutetea kesi hata kwa kujitolea kulingana na maslahi yake.
Jee wewe ulitegemea Lema akiwa na kesi amtumie Lamwai?
Kila Mtanzania ana haki ya kuhoji si lazima kuwa ndani ya Chama kwani pesa wanayotumia ni Ruzuku inayotokana na kodi tunazokatwa!!!
 
Ndio maana kuna msajili wa vyama ambaye vitabu vilivyokaguliwa copies zinapekekwa kwake, unaweza kwenda kuangalia huko.
Hivi kila mtu miongoni mwa Watanzania milioni 50 akija JF akihoji abajibiwa, ajiwa FB au mtandao wowote ajibiwe na mikutano ya hadhara wajibiwe sii hesabu za mwaka mmoja zitachukua miaka mitano kuwajibu wote?
 
Kila Mtanzania ana haki ya kuhoji si lazima kuwa ndani ya Chama kwani pesa wanayotumia ni Ruzuku inayotokana na kodi tunazokatwa!!!
Ahsante Mwana na mimi hapa nimeuliza bila kuegemea chama ni swali in general kwa sbu ruzuku ni kodi za kila mtanzania bila kujali chama...na sijasita kuuliza pia wanapokamatwa hao viongozi bdye serikali inashindwa kesi hii hasara ni ya nani? Na kma kesi hazina msingi wwte kwa nini wanawakamata na wengine hata kusafirishwa?
 
Back
Top Bottom