Nani anakumbuka chupi za VIP?

Mmenikumbusha yolanda,ledygey! Na purfume zake!Zilikuwa zinabamba!
 
wandugu mi kwa kuanzia tu
nimevutiwa na kamsemo haka " mficha
moto kwenye msitu lazima moshi
utamuumbua" announcing the birth of New
World Order...
 
Nakumbuka vyote mkuu je wewe unakumbuka mashati tunaweka lebo ya soda ya Double cola???unapiga pasi inabaki picha ya chupa za Double cola au shati za ndege,Jeans za Zico,Maradona,Michel Jackson??Raba petty

Yeah! Kakakiiza nakumbuka, mjomba wangu alikuwa anafanya kazi kampuni moja ilikuwa inaitwa handico, (handcraft corporation nadhani) pale walukuwa wanafanya kazi za sanaa za mikono kama uchongaji na mengineyo ikiwemo screen printing, nimekumbuka hii baada ya kunigusia kuhusu, lebo za double cola na mashati ya ndege, basi mimi pale nilitengeneza shati langu mwenyewe kwa mikono yangu, kama la juliana lakini langu lilikuwa na picha ya tausi, I was mbele picha ndogo na nyuma mgongoni picha kubwa,

Bila shaka hujasahau suruali za mchemchele, mocasin, kwenye raba kulikuwa pia na DH Double Happines kutoka china, kweli zamani raha, usisahau bia za primus kutoka burundi chupa kubwa, bia moja mnashea.
 
Vipi kuhusu matukio mbalimbali ya kustajabisha eti mtu kageuka chatu buguruni!hivi hii ilikuwa kweli?mtujuze mlioweza shuhudia tukio
 
Jamani msisahau Walkman, radio cassette za Memory Q (National) stove za kujaza upepo za sweden, mabasi ya ikarus, milango yake ya upepo ilikuwa inawabana watu, na pale kwenye maungio likikata kona kama umeweka mgongo unafinywa vilevile, makonda wa uda walikuwa wanakata ticket kwa kutumia mashine za kuzungusha kwa mkono, enzi ukimiliki tv na deki yake unakuwa na registration card kama gari vile. Tuendelee kukumbushana.
 
kaka Kiiza umevuta hisia tamu na zenye burudani ukumbakapo, mi nakumbuka perfume za yolanda, na mafuta ya mikebe ka ile wanayowekea ugolo akina bibi. Shule ya msingi kulikuwa kuna kutumia vijiti badala ya vifungo unaiingiza ktk shate then unaingiza katika tundu la kifungo na kutokezea upande wa pili na kukiweka usawa hapo shati halifunguki wala kuchomoka. ..
 
Fantastic ... stove za kujaza upepo rangi ya shaba ikiwashwa ndani hakuna kusikilizana kama ni kuongea lazima uongee kwa sauti ka vile mko baa dah old is gold
 
Mmenikumbusha yolanda,ledygey! Na purfume zake!Zilikuwa zinabamba!

Hahaaaa..umeninikumbusha mbaaali..mafuta ya shanti, ayu nk..zile chupi za vip ilitokea jamaa mmoja anacheza mpira alafu anatakiwa to be substituted! Kumbe ile chupi ya vip imeshakatika na imeshapanda mpaka kifuani..kama unakumbuka wakati huo jezi zinakuwa kumi na moja tu kwa hiyo inabidi umwachie jezi ya juu yule anayeingia..pata picha ilikuwaje mkuu afu nje kuna akina dada wanaimba usiniumizieeee!!hahaaa kazi kweli kweli!
 
Nakumbuka vyote mkuu je wewe unakumbuka mashati tunaweka lebo ya soda ya Double cola???unapiga pasi inabaki picha ya chupa za Double cola au shati za ndege,Jeans za Zico,Maradona,Michel Jackson??Raba petty

Kweli hamna cha mtumba wala nini..nakumbuka shati langu la shule jeupe nikalibandika yale mastika ya'take me'nikawnda nalo shule..kibano nilichokipata ctasahau..sababu nilichapwa shule na mzee akaitwa shule akanichapa mbele ya walimu..duh tuliosoma zamani tulifaidi shule..
 
Haaah...haaaaa,umenikumbusha mbali sana,siku moja nikiwa kijijini kwetu pale mugana, nilihudhuria mechi moja kati ya kijiji chetu na cha jirani,sasa mshkaji mmoja alikuwa ameitiga VIP na KIPINDI HICHO HAPAKUWEPO NA JEZI ZAIDI YA UPANDE MMOJA KUVUA MASHATI KUBAKI KIFUA WAZI,Sasa kutokana na mshikaji alivyokuwa anahaha uwanja mzima....eeh bwanae ......si ilishamfika kifuani bila yeye kujua?Sasa uwanja mzima ukawa unashangilia (mashabiki)yeye ndio kwanza sifa zinamjaa na akaongeza kasi ya kupiga chenga, mashabiki hasa mademu nao wakazidisha makelele kushangilia.Sa,jamaa alipokuja kushtuka anaikuta VIP imejikita vizuri kifuani ka sidiria vile heeee....hiiiiiiiii!!
 
Sitaki kusikia habari ya VIP ilishaniumbua mbele ya Mama, Wanafunzi na Walimu, yaani kakisha katika tu kanakimbilia kifuani, kanapanda mdogo mdogo mwisho unahisi kaupepo maeneo flani, mara kameshatokeza kifuani!!!

Niliamua kununua chupi nyekundu za kike nitumie ila nazo ikawa noma maana enzi zetu tulikua tunaogea mtoni pale Magamba Sec now SECUCO. Sitaki hata kuzisikia!
 
tulikuwa mazoezini. mimi beki na tumevaa fulana/jezi. akaja striker wa waliokuwa vifua wazi. anafaint na kunipiga chenga. akawa anaelekea golini. mi nikaanza kumfukuza nyuma yake kidogo. kudadadeki. ghafla naona VIP inatoka kwenye bukta inapanda juu kwa kasi. halafu basi bukta yake nayo mpira wa kiunoni ukawa umelegea. so **** zote nje....mimi c kicheko hicho mpaka nilishindwa kuendelea kumfukuza. jamaa akamchambua kipa na kujifungia goli kiulainiii huku anashikilia bukta isiendelee kumdondoka. mshkaji alikuwa anaitwa SUnday na hapo ilikuwa Kibaha secondari enzi zile za kambi za umiseta kanda ya mashariki!!!! enzi za east pressure!!!
 
Nikiwa mdogo nililiaga mpaka nikanunuliwa, bila kujali za wanaume hahaa, sijui zile rangi ndo zilikua zinanizingua ha haa haa.
 
Back
Top Bottom