Nani anakumbuka chupi za VIP?

Aise bado kabisaa sijategemewa kuwepo kwenye huu ulimwengu. Heshima yako mkuu.
Hapana shaka. Mimi mwenyewe hivyo ndio vilikuwa vyupi vyangu.Lakini siku moja "VIP" iliniumbua sana nikiwa nasoma Jamhuri Primary school pale Moshi mjini, siku hiyo ilikuwa J'3 tuko mstarini kila mwanafunzi yuko smart tayari kwa ukaguzi. Enzi hizo Mwl alikuwa anakagua kwelikweli kuanzia mavazi na usafi wa mwili kwa ujumla. Siku hiyo nimetinga VIP yangu sina wasiwasi kumbe kile kikamba cha chini kimeshachoka! ile kuambiwa mguu pande! Mguu sawa! Tulia. Sasa Mwl anaanza kupita kwa mwanafunzi mmoja mmoja kwa ajili ya ukaguzi, Mmh! Mwl akiwa kwa mwanafunzi wa nne ili kunifikia mimi nikaanza kusikia kijibaridi fulani nikaona labda ni hali ya kawaida tu,Mwl kafika kwangu anaanza kunikagua kacheki viatu safari boot zile za (BORA) ziko freshi,kakagua kucha ziko safi kipindi hicho walikuwa wakikagua pia kuanzia kifuani kwenda mpaka shingoni kuona kama kuna ukurutu. Basi bana Teacher akaniamuru nifungue kishikizo cha juu cha shati, ile kufungua tu nashangaa Mwl anacheka na kuniambia wee! umevaa nini kifuani? kucheki aaah! VIP imeshapanda hadi kifuani siku nyingi! Mwl alijua ni mnyama VIP akaniambia hebu nenda katoe hicho ulichovaa,wanafunzi wenzangu waliojua ni kitu kimekwea wakaanza kunicheka.Nilikimbia nyumbani Police line na kubadilisha na kuvaa dizaini nyingine. Kiukweli vyupi vya VIP vilikuwa noma enzi hizo.
 
Wale wa enzi za kale mnakumbuka hii?
FB_IMG_15816852159154021.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
🤣🤣🤣 dah! Mkuu hizi chupi zilkuaje ad zikikatika znapanda kifuani?????
 
Back
Top Bottom