Nani anakumbuka chupi za VIP?

Nimekumbuka kitu kimoja nikiwa katika baa moja nimeletewa chupi na chinga!Chupi za kichina! Mwisho wake nikakumbuka vyupi vya VIP nilifurahishwa na ufungaji wake katika boks (Prkg) ila nakumbuka kadhia yake kukatika ktk maungio!! Kamkanda kachi!! Hapo nazungumzia 80's)[/QUOTEn

Kaka nimecheka hadi mbavu sina, VYUPI vya VIP vilikuwa noma, si unajua mashindano ya umiseta, Tukiwa F3 mwanangu, mashindano ya madarasa, kuna mwanafunzi mmoja, alikuwa kwenye mbio, basi akiwa katika motion na amewatangulia wenzake yale maungio ya VIP yakakatika, basi ikachomoza juu ya pensi ile hadi kifuani huku akiwa kifua wazi, umati wa wanafunzi uliokuwepo kuiona wakaaanza kumshangilia, mabinti kwa wavulana, basi jamaa akadhani wanamshangilia kwa kuwa amewatoka wenzie, jamaa akaongeza speed hadi akawa wa kwanza huku akishangiliwa vilivyo na mabinti wakimfuata hadi mwisho.


Ile kufika mwisho akipumua pumua akaona iko kifuani, Jamaa kidogo azimie aliona aibu na akajitoa kwenye mashindani. Hakurudi kwenye mbio tena pamoja na juhudi za walimu kumbebembeleza.

Hizo CHUPI NUKSI ndugu yangu.
 
daah...mimi nakumbuka wakati naoga mtoni iliwahi kukatika katikati ikashuka chini ikasombwa na maji.. ila baada ya hapo nikawa naikagua nikiona inataka kukatika tu nainganisha kwa kuishona na sindano ya mkono...
 
Freddie, Bila kuisahau hilo shati la shule mgongoni limepigwa pasi kwa mikunjo inakuwa kama kashata hivi, unakumbuka?
Yap nakumbuka ile mikunjo inakuwa kama utando wa buibui..afu unapiga mstari mmoja toka bega moja hadi lingine..hahaa safi sana..what a memory!!
 
Jamani msisahau Walkman, radio cassette za Memory Q (National) stove za kujaza upepo za sweden, mabasi ya ikarus, milango yake ya upepo ilikuwa inawabana watu, na pale kwenye maungio likikata kona kama umeweka mgongo unafinywa vilevile, makonda wa uda walikuwa wanakata ticket kwa kutumia mashine za kuzungusha kwa mkono, enzi ukimiliki tv na deki yake unakuwa na registration card kama gari vile. Tuendelee kukumbushana.

Nauli za basi Dar ilikuwa sh tana enzi hizo ikiitwa dala. Ndio mwanzo wa mabasi Dar kuitwa Daladala. Kulikuwa na mabasi ya Uda,kupanda wote sharti mkae foleni. Mabasi binafsi yalikuwa machache. Nakumbuka njia ya Ubungo posta kulikuwa na Torino(fiat)Shella Beach(scania) Matumbi(Leyland) na mabasi ya Mzee Casian Lucas (fiats) wa Ubungo Maziwa.
 
Ha ha ha! kakakiiza umenisababisha nimrimembe mwl wangu
enzi hizo alikuwa anatoa demo ya kucheza basketball wakati wa umiseta
Njombe akawa amevua shati,alikuwa na mikwara kibao na alikuwa kifua wazi
mara chupi ikapanda yeye hakushituka mpaka ikafika kifuani,halafu ilikuwa chafu ile
ile mbaya,simnakumbuka zilivyokuwa zinaonesha uchafu!!!

Nakwakuwa alikuwa mpenda sifa wanafunzi hawakmshtua
wakawa wanapiga kelele ticha! ticha!yeye akadhani wanamshangilia,
Hamadi kujiangalia kitu kipo kwapani,aliondoka hakurudi mpaka mashindano
ya umiseta yakaisha.:pound::pound::pound::pound::pound::pound:
 
Kwenye mashindano ya awali ya UMMISETA jamaa yetu mkimbia mita 100 alivaa VIP; ikakatika akiwa anakaribia finisshing line..Taabu aliyekuwa ameshika stop watch alikuwa Mwalimu wetu wa phyisics wa KIKE; alitupa stop watch kwa yale aliyoona.=VIP ilikuwa kifuani kama KANCHIRI (sidiria) na huku chini mambo yalikuwa kama mtu anatumia KOMBEO kurusha jiwe...Haahahaaaaaahhhhaaa!! VIP....Kukatika kwake ilikuwa ni kitu hatari hasa kama unakimbia na KUNA WATAZAMAJI..
Hahah..dah imebidi niitafute tena hii thread!weekend yangu ndo imeshaanza namna hii
 
Ha ha ha! kakakiiza umenisababisha nimrimembe mwl wangu
enzi hizo alikuwa anatoa demo ya kucheza basketball wakati wa umiseta
Njombe akawa amevua shati,alikuwa na mikwara kibao na alikuwa kifua wazi
mara chupi ikapanda yeye hakushituka mpaka ikafika kifuani,halafu ilikuwa chafu ile
ile mbaya,simnakumbuka zilivyokuwa zinaonesha uchafu!!!

Nakwakuwa alikuwa mpenda sifa wanafunzi hawakmshtua
wakawa wanapiga kelele ticha! ticha!yeye akadhani wanamshangilia,
Hamadi kujiangalia kitu kipo kwapani,aliondoka hakurudi mpaka mashindano
ya umiseta yakaisha.:pound::pound::pound::pound::pound::pound:

Hii ndiyo dawa ya mijitu inayopenda sifa za kijinga na kupiga piga wanafunzi ovyo
 
Duuh ! zile ukijifanya unacheza mpira umeivaa inageuka kuwa vest
 
Nimekumbuka kitu kimoja nikiwa katika baa moja nimeletewa chupi na chinga!Chupi za kichina! Mwisho wake nikakumbuka vyupi vya VIP nilifurahishwa na ufungaji wake katika boks (Prkg) ila nakumbuka kadhia yake kukatika ktk maungio!! Kamkanda kachi!! Hapo nazungumzia 80's)[/QUOTEnKaka nimecheka hadi mbavu sina, VYUPI vya VIP vilikuwa noma, si unajua mashindano ya umiseta, Tukiwa F3 mwanangu, mashindano ya madarasa, kuna mwanafunzi mmoja, alikuwa kwenye mbio, basi akiwa katika motion na amewatangulia wenzake yale maungio ya VIP yakakatika, basi ikachomoza juu ya pensi ile hadi kifuani huku akiwa kifua wazi, umati wa wanafunzi uliokuwepo kuiona wakaaanza kumshangilia, mabinti kwa wavulana, basi jamaa akadhani wanamshangilia kwa kuwa amewatoka wenzie, jamaa akaongeza speed hadi akawa wa kwanza huku akishangiliwa vilivyo na mabinti wakimfuata hadi mwisho.Ile kufika mwisho akipumua pumua akaona iko kifuani, Jamaa kidogo azimie aliona aibu na akajitoa kwenye mashindani. Hakurudi kwenye mbio tena pamoja na juhudi za walimu kumbebembeleza.Hizo CHUPI NUKSI ndugu yangu.
Ha ha haa haaa haaaa hahaaaaa
 
Nimekumbuka kitu kimoja nikiwa katika baa moja nimeletewa chupi na chinga!Chupi za kichina! Mwisho wake nikakumbuka vyupi vya VIP nilifurahishwa na ufungaji wake katika boks (Prkg) ila nakumbuka kadhia yake kukatika ktk maungio!! Kamkanda kachi!! Hapo nazungumzia 80's)
haha hahaaaa mkuu umenifanya nicheke. Tene zile chupi ni kama kiwanda cha chawa. Mana chawa na chupi za vip ni kama mbuz na chumvi. Afu zikikatika huwa zinapanda juu hadi tumboni.
 
Duuh ! zile ukijifanya unacheza mpira umeivaa inageuka kuwa vest
hahaha hahaaa jamani hii thread imepotea njia. Nadhan kule kwenye jokes ndo pahala pake. Mi nlikua serious natfuta newz ona sasa nimeishia kucheka....haha haaa. U made my day.
 
Ha ha ha! kakakiiza umenisababisha nimrimembe mwl wanguenzi hizo alikuwa anatoa demo ya kucheza basketball wakati wa umisetaNjombe akawa amevua shati,alikuwa na mikwara kibao na alikuwa kifua wazimara chupi ikapanda yeye hakushituka mpaka ikafika kifuani,halafu ilikuwa chafu ileile mbaya,simnakumbuka zilivyokuwa zinaonesha uchafu!!! Nakwakuwa alikuwa mpenda sifa wanafunzi hawakmshtuawakawa wanapiga kelele ticha! ticha!yeye akadhani wanamshangilia,Hamadi kujiangalia kitu kipo kwapani,aliondoka hakurudi mpaka mashindanoya umiseta yakaisha.:pound::pound::pound::pound::pound::pound:
Ayaaaaaaaaaaah!
 
...Bila kusahau kama ni wewe ni mvulana ndio uko std VII (LY) unachomekea shati kwa nyuma then mbele unaliachia halafu kama una nywele nyingi kidogo ili uonekane gangwe unaziweka katika mtindo matuta, chini umepiga chachacha au safari buti iliyoanza kuchakaa shuleni kwetu tulikuwa tunaita ubuyu!!
Hahaaaaaaa umenkumbusha mbali sana Ubuyu...kuna jamaa yangu mpaka leo 2namwita Ubuyu...tukiwa Seminarini...uwez amin mpaka leo ni Padri uko Catania(sicily-Italy) na adi leo 2namwta Fr.UBUYU...duh JF bana
 
nakumbuka wanawake tulikuwa na chupi flani zimechorwa moyo na mkuki unapenya kati unatokeze upande wa pili zimeandikwa express mid night.. ukiwa nayo hiyo hata sketi ikifunuka hadi kichwani huna wasiwasi.. otherwise nakumbuka waschana wengine hata chupi walikuwa hawavai na ikifika jumatatu na alhamisi tunafanyiwa ukaguzi eti tunachunguliwa hadi chupi... wengine wana za jinja wengine hawana kbs.. na kale ka mtindo ka wavulana kuweka kakioo chini ya miguu ya waschana ili watuchunguliee. jamani leo nimecheka sana mmenikumbusha mbaali sana
 
enzi hizo cream zinaitwa ambi na cleartone wanaopaka hzo wanaonekana matajiri kweeli wengine ilikuwa nimwendo wa shanti mafuta yanavitu vinametameta hivi na ukikosa perfume unatumia tu sabuni rexona unaogea mbunju au sabuniz a magadi halafu unajipaka rexona ili unukie basi unameremereta utadhani umepigwa polish. halafu kulikuwa na mitindo ya nywele akina yomboo na zazuuu... hizo nilikuwa naona mama wadogo na dada zangu wakipaka.. eh tumetoka mbali jamani acheni tu
 
Yap nakumbuka ile mikunjo inakuwa kama utando wa buibui..afu unapiga mstari mmoja toka bega moja hadi lingine..hahaa safi sana..what a memory!!
tena shurti upige pasi ya mkaa kwa kutumia wanga ili lishike vizuri mikunjo ya buibui.. halafu nakumbuka kuna kipindi kile cha miezi 18 ililazimu wanafunzi kuvaa vitambaa vya 'marekani' au 'marudufu' ambavyo pia vilitumika sana kutengenezea sanda za kuzikia.. raba fulani zilikuwa zikiuzwa BORA zikiitwa ikarus zina kinundu hapo mbele cha mpira... na viatu vile 'rise-on' za rangi ya mende (brown) ndefuuuuu enzi hizo tulikuwa tunaziita 'mfaume waniliza' au 'teremka tuzoze' huku mtu katinga kaunda suti imechanwa hapa nyuma kama mabawa ya mende na zinga la buga luu... mapatano na fundi ni kiunoni tu huku chini achia hadi kitambaa kiishe... duh aaah hii safi sana
 
Back
Top Bottom