Nani anaikumbuka hii AC Milan yamoto?

CARIFONIA

JF-Expert Member
Aug 17, 2013
518
901
Kwenu wahenga nani ana kumbukumbu na hawa miamba wa Italy AC Milan, ilikua ya moto kweli kweli.

PSX_20201223_201036.jpg
 
2005, Atatürk stadium..
Usiku wa istanbul miracle
Wanastaajabishwa na vijukuu vya bill shankly..

Ika hii milan ilikuwa balaa,
seedorf kwangu ndio alikuwa mchezaji kipenzi katika kikosi hiki, ni shujaa asiyeimbwa ila alikuwa fundi mnoo.. Kabeba ndoo hii akiwa na ajax 95 km sikosei, akaibeba akiwa na madrid 96, enzi hizo wanapika uzi chata teka.

Kisha akabeba na ac milan mara hii mara 2, ya kwanza 2003 wanamfunga kibibi kizee cha turin kwa matuta, ya pili 2007 wanalipa kisasi wanachukua ndoo mbele ya Liverpool fc

Ricardo Ernesto almangungule kaka kibraza, fundi wa kibrazil, mtaalam wa ku'curve, vidi na teja rio wanamkumbuka vizuri, aliwafanya km jackie chan anavyowatenda maadui katika movie zake. Anakimbia kama anaanguka sasa hivi.

Pirlo, sijui nisemaje, huyu ndio alikuwa backbone wa 4-4-2 diamond formation, akili nyingi, mipango mingi..

Nafasi haitoshi kuwazungumzia woote kika mtu na sifa zake..

Cafu namba 2 bora toka kuuanza kwa ulimwengu wa soka.

Jaap stam
Nesta
Kibabu maldini
Ukrainian andriy shevchenko
Muuaji hernan crespo
Gattuso roho ya paka.

Hapo bado costacuta
Kibabu inzaghi kosa moja goli moja, mzee wa offside trick, sio wale wa albata..
N.k n.k
 
Walichowafanyia Liverpool mwaka 2005 kwenye dimba la Ataturk jijini Istanbul Uturuki watakikumbuka daima.
Hakitasahaulika kwa siku za hivi karibuni.
Hata hivyo walikuwa na kikosi kikali sana kama inavyoonekana pichani.
Beki yao chini ya Maldin ilikuwa kizingiti tosha
 
Kabla ya hapo ilikuwepo ya 1992 mpaka 1995 ambayo mwaka 94 ilimpiga Barcelona 4 bila ikiwemo na wachezaji watatu waliokuwa wakipokezana uchezaji bora ulaya Frank Rijcard, Van basten na Rud Guilt huku ikiwa na ukuta wa chuma
Hao waholanzi wa3 walikuwa moto wa kuotea mbali ,, sema Marco van basten majeruhi yaliwahi kumuondoa lkn dunia ingeshuhudia mengi kwa mwamba huyo.
IMG_20201223_215301.jpg
 
Back
Top Bottom