Nani anabisha kuwa Kikwete na CCM yake si 'dhaifu'?

katika hotuba yake Jk hakuwahi kutaja majina ya Lowassa na chenge kama ndio magamba. Lowassa na chenge walitajwa kwenye list of shame kama mafisadi na Dr Slaa pale mwembeyanga. Hii ni moja ya sababu kubwa chadema wanageuka na kusema ni msimamo wa JK wakati ukweli ni msimamo wao juu ya lowassa na chenge
 
Nape alikuwa anatumia dhana ya chadema kwa kugeuza msimamo wa ccm kuwa wa chadema na ndipo safari hii kule Dodoma kaambiwa asichanganye msimamo wake binafsi na wa chama kuhusu agenda ya kujivua gamba.
 
wameamua kuchagua kaburi wao wenyewe baadae wataaanza kutafuta nani mchawi wao
 
Ulikuwa hujui? Tuna Rais kilaza na historia inatuhukumu kwa chaguzi zote!! Hata ile nepi ya cameroon imekana kauli ya kuvua gamba!


ulikuwa hujui cameron ni mshirika wa karibu wa chadema kwa upande wa mahusiano kisiasa kuliko ccm. kwa maana hii vilaza watakuwa ni wewe na waliokutuma. ndio maana tunasema Jk hakuwa na sababu ya kusoma barua yenu ya kumwomba kukutana na nyinyi angewaacha muandamane nchi nzima
 
amekuwa goigoi, mwoga, mnafiki anajifanya anatawala kwa mujibu wa sheria, sheria zipi mbovu haziwezi hata kuwafunga mafisadi yaani mimi simuelewagi kazi kuchekacheka tu kama mwanamke anatongozwa

kama ana udhaifu huo mmeomba kwenda Ikulu kutafuta nini basi mtakuwa wanafiki wakubwa kuliko JK. Mnakwenda kujadili maslahi gani ya taifa na JK? Bora tu mungeendelea na maandamano yenu.
 
chadema ni kama hamna akili mnasema ccm wote sio wasafi lakini mnaandika barua ya kuzungumza na wachafu. Jk alishasema msimamo wake mnakwenda kuonana naye kwa lipi jipya?
 
katika hotuba yake Jk hakuwahi kutaja majina ya Lowassa na chenge kama ndio magamba. Lowassa na chenge walitajwa kwenye list of shame kama mafisadi na Dr Slaa pale mwembeyanga. Hii ni moja ya sababu kubwa chadema wanageuka na kusema ni msimamo wa JK wakati ukweli ni msimamo wao juu ya lowassa na chenge

Wabara, Nafikiri una matatizo binafsi na CDM. List of shame haikumsema Lowassa na Chenge tu iliwasema wengi akiwemo Kikwete mwenyewe. Lowassa, Chenge na Rostam ingawaje walikuwa kwenye list of shame, walitajwa na CCM yenyewe chini ya uongozi wa Nape kwamba ndio mapacha watatu wanaopashwa kujivua gamba. Sasa hapa CDM inabebewaje bango tena?

Tiba
 
Sasa kuondolewa mikononi mwa NEC
Ni mkakati wa kudhibiti watuhumiwa

Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), imependekeza kwa Halmashauri Kuu (Nec), irejeshewe suala la kuvua magamba linalowahusu viongozi wa juu wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi. Pendekezo hilo limetolewa na CC iliyokutana chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete kwa siku mbili na kumaliza kikao chake juzi usiku.

Kwa mujibu wa taarifa zilizovuja kutoka ndani ya chama hicho, wajumbe hao walipendekeza suala hilo lirejeshwe kwenye CC ili hatua za kushughulikiwa ziweze kuchukuliwa na ngazi hiyo. Suala la uadilifu ndani ya chama likiwa ni moja ya mpango wa mageuzi ndani ya chama (kuvua magamba), liliamuliwa na Nec wakati wa mkutano wa Aprili, mwaka huu ambapo lilitoka azimio namba 15 likiwataka wanachama na viongozi waliokosa sifa hiyo kujiengua wenyewe kabla ya kuenguliwa.

Habari hizo zinasema kuwa hatua ya kurejesha utekelezaji wa maamuzi hayo kwa CC, imeelezwa kuwa ni furaha kwa kundi linalotuhumiwa kwa ufisadi huku mahasimu wao wakiona ni njia ya kulipa kundi hilo haueni. Kundi linalopinga ufisadi ndani ya chama hicho linataka suala hilo limalizike katika kikao cha Nec kilichoanza jana mjini hapa. "Sisi tunataka mambo haya yamalizike hapa hapa kwenye kikao cha Nec kama watu kufukuzwa basi wafukuzwe, kama kusimamishwa basi na iwe hivyo hivyo," alisema mmoja wa wanachama wa kundi linalojipambanua kwa kupinga ufisadi. Hata hivyo, tangu kuanza kwa vikao hivyo, makundi hayo hasimu yalikuwa yakihangaika kila moja likitafuta kuungwa mkono na wajumbe wa Nec.

Hata hivyo, hadi kufikia jana jioni, bado hoja hiyo ilikuwa haijatua katika kikao hicho na baadhi ya wajumbe walisema inategemea uamuzi wa Mwenyekiti, Rais Kikwete.

Source: Nipashe
 
amekuwa goigoi, mwoga, mnafiki anajifanya anatawala kwa mujibu wa sheria, sheria zipi mbovu haziwezi hata kuwafunga mafisadi yaani mimi simuelewagi kazi kuchekacheka tu kama mwanamke anatongozwa

msamehe Mungu ana maana yake kuleta duniani wavivu,wanafiki,wezi,mabwabwa, taahir...,nk
 
Endapo Lowassa na Chenge watafukuzwa faida kubwa itakuwa upande wa chadema na hasara kwa CCM kwani hatua hiyo itaigawa CCM na ndio maana chadema wanapiga debe wafukuzwe.
Hivi Nape ni katibu mwenezi wa CDM? Maana ndiye aliyekuwa mpiga debe mkuu juu ya mapacha watatu!
 
Kiongozi imara ana sifa moja kuu. Lazima awe na uwezo wa kufanya maamuzi na kusimamia kutetea maamuzi hata kama kutamgharimu. Kiongozi imara harudi nyuma.

JK alifanya maamuzi kuhusu kuwavua gamba mapacha watatu. Huo ndio ulikuwa uamuzi wa chama na ili chama kulinda heshima yake lazima kuutekeleza. Sasa JK anaonekana ku retreat, hii ni kwa sababu ni dhaifu na hawezi kutekeleza hata yale maazimio aliyoahidi kutekeleza.

Madhara ya kuacha kuchukua hatua dhidi ya Lowassa na Chenge ni kwamba CCM itapuuzwa na kuonekana ni chama cha mafisadi ambacho kimejaa uoga kuchukua hatua.

Ilikuwa hakuna sababu kuanzisha dhana ya kujivua gamba lakini kwa kiongozi mwenye nguvu kwa vile dhana hiyo imeshaanzishwa kwa ajili ya kukinusuru chama lazima itekelezwe.

Bila kutekelezwa wananchi watakuwa na mtazamo hasi zaidi dhidi ya ccm maana ni chama hicho chenyewe kilisema hawa ni mafisadi na wakapewa muda wajiondoe la sivyo wataondolewa
Wamekaa wamefikiria wameona ni heri waonekane ni wadhaifu kuliko kung'ang'ania kuwavua gamba akina Lowassa chama kipalanganyike unategemea nani ndani ya CCM ana nguvu ya kumtoa Lowasa?
 
Back
Top Bottom