Nani anabisha kuwa Kikwete na CCM yake si 'dhaifu'?

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Kiongozi imara ana sifa moja kuu. Lazima awe na uwezo wa kufanya maamuzi na kusimamia kutetea maamuzi hata kama kutamgharimu. Kiongozi imara harudi nyuma.

JK alifanya maamuzi kuhusu kuwavua gamba mapacha watatu. Huo ndio ulikuwa uamuzi wa chama na ili chama kulinda heshima yake lazima kuutekeleza. Sasa JK anaonekana ku retreat, hii ni kwa sababu ni dhaifu na hawezi kutekeleza hata yale maazimio aliyoahidi kutekeleza.

Madhara ya kuacha kuchukua hatua dhidi ya Lowassa na Chenge ni kwamba CCM itapuuzwa na kuonekana ni chama cha mafisadi ambacho kimejaa uoga kuchukua hatua.

Ilikuwa hakuna sababu kuanzisha dhana ya kujivua gamba lakini kwa kiongozi mwenye nguvu kwa vile dhana hiyo imeshaanzishwa kwa ajili ya kukinusuru chama lazima itekelezwe.

Bila kutekelezwa wananchi watakuwa na mtazamo hasi zaidi dhidi ya ccm maana ni chama hicho chenyewe kilisema hawa ni mafisadi na wakapewa muda wajiondoe la sivyo wataondolewa
 
Tunataka Nape aje hapa jamvini atueleze bila kumung'unya maneno, walipokuwa wanasema kujivua gamba, walituambia kwamba wamewataka pia Magamba kujiondoa wenyewe, vinginevyo watawaondoa kwa aibu. Pia alikwenda mbele zaidi na kutuambia kwamba kuna barua zao zimeandaliwa tayari kwa kuja kuwakabidhi.

Je mbona hatujaona hata moja kutekelezwa? Au aje aseme tu alikuwa anaongea Utani tu ispokuwa watu hatukumwelewa. Otherwise atuambie kwamba je bado anajiona kweli yeye ni mtu wa kuaminika kwenye jamii makini?

Najua kwamba ni mwanachama wa hili jukwaa japo siku hizi hachangii toka alipokataa ukweli kwamba amekuwa akija humu jukwaani na kujaribu kuelezea mambo yake ikiwamo matokeo ya uchaguzi wa Igunga.
 
Ulikuwa hujui? Tuna Rais kilaza na historia inatuhukumu kwa chaguzi zote!! Hata ile nepi ya cameroon imekana kauli ya kuvua gamba!
 
amekuwa goigoi, mwoga, mnafiki anajifanya anatawala kwa mujibu wa sheria, sheria zipi mbovu haziwezi hata kuwafunga mafisadi yaani mimi simuelewagi kazi kuchekacheka tu kama mwanamke anatongozwa
 
Narudia kusema tena humu jukwaani,Kwa CCM ya leo hakuna mwenye uwezo wa kumfukuza Lowasa.na hii ni kwa sababu nani ni MSAFI ndani ya chama,jamani semeni ukweli ni nani msafi ndani ya CCM, ni kwa ufisadi, ni kwa kupitisha miswaada kwa ushabiki, ni kwa kuunga mkono hoja kandamizi kwa wananchi, ni kwa rushwa ndogo na kubwa,ni kwa namna gani atoke mtu aseme EL toka humu eti wewe ni mchafu, Vijisenti-Chenge toka ccm wewe ni mchafu.

Hiyo kujivua gamba walikulupuka bila kujipanga tu kwa sababu ya kuwalaghai wananchi baada ya kuona hawakubaliki kwa sababu ya ufisadi wao,ni vile jamii imeshatambua CCM ni chama cha mafisadi. Walipashwa kutafuta namna nyingine ya kukisafisha chama lakini sio kuwanyoshea kidole baadhi yao.sas leo kauli yao itawagharimu maana itabidi waje waupotoshe umma kwa lugha zingine ambazo bado hazitawajenga.

HAKUNA WA KUWAFUKUZA EL NA MZEE WA VIJISENTI
 
Tunataka Nape aje hapa jamvini atueleze bila kumung'unya maneno, walipokuwa wanasema kujivua gamba, walituambia kwamba wamewataka pia Magamba kujiondoa wenyewe, vinginevyo watawaondoa kwa aibu. Pia alikwenda mbele zaidi na kutuambia kwamba kuna barua zao zimeandaliwa tayari kwa kuja kuwakabidhi.

Je mbona hatujaona hata moja kutekelezwa? Au aje aseme tu alikuwa anaongea Utani tu ispokuwa watu hatukumwelewa. Otherwise atuambie kwamba je bado anajiona kweli yeye ni mtu wa kuaminika kwenye jamii makini?

Najua kwamba ni mwanachama wa hili jukwaa japo siku hizi hachangii toka alipokataa ukweli kwamba amekuwa akija humu jukwaani na kujaribu kuelezea mambo yake ikiwamo matokeo ya uchaguzi wa Igunga.
Atakuja na jibu la kuwa hamkuelewa dhana zima ya kujivua gamba. Ni aibu kwa nchi kuongozwa na chama kisicho na msimamo!
 
Kungelikuwa na utekelezaji wa sera na ahadi mbalimbali ndani ya CCM, walau kwa asilimia 40% tu, katika kipindi cha miaka 10 iliyopita NCHI hii ingeshaondokana na umasikini wa kujitakia na mapokeo yetu ya miaka 50 ya uhuru yangelijawa na shangwe za kweli!!!

CCM ya leo ndani ya Taifa letu ni sawa na sanamu ya simba nyikani!!
 
Rais aliyeshindwa kuwavua gamba wanachama katika chama chake anataka kusimamia utungaji wa katiba mpya! Atawezeje kusimamia utungaji wa katiba mpya kama suala la gamba limemshinda? Watanzania tunapaswa kujiuliza sana kwa ujinga wetu wa kukubali kuendelea kuongozwa na JK. Anashindwa kuongoza chama chake halafu awe na uwezo wa kuongoza nchi!
 
Topic: Nani Anabisha kuwa
JK si Dhaifu?
Hapo hakuna ubishi, JK si dhaifu. Ni strong coz kuongoza nji yenye mafisadi wengi namna hii si kazi rahisi na si wote wanaweza!
 
Unaweza kunitajia makosa mawili2 ya lowasa ambayo unaweza kumtia hatiani?, na ufahamu kuwa unamtia mti hatiani kwa ushahidi.
 
Acha uongo dhana ya kujivua gamba haikuwa uamuzi wa chama cha ccm na ndiyo maana NEC haijapitisha kufukuza unaodai ni mafisadi. Dhana ya kujivua gamba ilijitokeza kwenye hotuba ya JK wakati wa kuazimisha miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM.
 
Hii dhana ya kujivua gamba haina tofauti na dhana ya kupunguza posho ya Mbowe na Dr Slaa ambayo inapata upinzani ndani ya chadema. John shibuba, Joseph selasini na wabunge wengine wa chadema wamepinga dhana hiyo. Haina mantiki na sio sahihi kusema kwamba kila wakati kauli ya mwenyekiti wa chama ni uamuzi wa chama.

Kuna wakati kauli ya mwenyekiti inaweza kujadiliwa ndani ya vikao vya chama kama maagizo lakini kauli inaweza kupata tafsiri pana na kutoka na azimio tofauti.
 
dhana ya kujivua gamba imetekwa na wapinzani wa JK ili kuitumika kisiasa. Jk kashtuka baada ya kupima upepo ndani ya chama chake kwa kupima faida na hasara za maamuzi ya pupa
 
Endapo Lowassa na Chenge watafukuzwa faida kubwa itakuwa upande wa chadema na hasara kwa CCM kwani hatua hiyo itaigawa CCM na ndio maana chadema wanapiga debe wafukuzwe.
 
CCM ikipuuzwa inakuwashia nini? hamia chama kingine ndio maana ya mfumo wa vyama vingi?
 
Unaweza kunitajia makosa mawili2 ya lowasa ambayo unaweza kumtia hatiani?, na ufahamu kuwa unamtia mti hatiani kwa ushahidi.
Kwamba Lowassa ana makosa au la si issue, issue ni kwanini waliazisha hivyo vita vya kumng'oa kama wanajua hawawezi? Lowasssa ataibuka kuwa na nguvu zaidi baada ya vikao hivi. Na ukweli dhana ya kujivua gamba imemjenga Lowassa na kumdhoofisha JK maana watu wataona Lowassa hakuna anayeweza kupambana nae hata kumzuia kugombea urais na JK hana nguvu yeyote ndani ya chama
 
Back
Top Bottom