Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Kwa maoni yangu, kama kuna eneo rais ameonyesha mapungufu makubwa, ni katika kulinganisha gharama iliyotumiwa na faida iliyopatikana (value for money). Kwa mfano, hivi majuzi wakati akifungua semina elekezi kwa viongozi waandamizi serikalini pamoja na mambo mengine rais alisikika akiwahimiza viongozi hao kutotumia mda wao mwingi maofisini, bali wafanya ziara huko vijijini ili kuyajua matatizo ya wananchi. Kuna watu wengi hapa nchini na mimi nikiwemo, tunao ziona hizi ziara za viongozi huko mikoani kuwa ni mzigo mkubwa kwa uchumi wetu. Kwa hesabu za haraka haraka, inasemekana msafara wa viongozi wa juu serikalini ughalimu kati ya shs, 300-500 milioni kila siku. Kiasi hicho cha fedha kinatosha kujenga zahanati angalau mbili. Hii ina maana kiongozi huyo akifanya ziara ya siku 10 mikoani anakwamisha ujenzi wa zahanati siyo chini ya 20. Na faida inayotokana na ziara hizo ni kama hakuna, kwa sababu huko mikoani serikali ipo, na kama isingelikuwa inatimiza wajibu wake angalau baada ya ziara kama hizo tungelisikia wakuu hao wanachukuliwa hatua, jambo ambalo ni nadra kulisikia. Sasa ikiwa kila kiongozi na watendaji waandamizi serikalini wote watafanya ziara vijijini hiyio gharama ambayo hakuna uwezekano wa kuzaa matunda yeyote nani aikabili!