Nani amewahi kuexperience hiki kitu?

Nani amewahi kuexperience hiki kitu?

Maisha ni kupanga na kujiwekea malengo hata kama itachukua muda.hiyo ya kutoroka na kutusua zilipendwa.
 
Hayo mawazo mgando aga nyumban hata kama kuna vita nyumban ni nyumban tu , thaman ya ndugu ni kubwa kuliko rafiki
 
Hii kitu alifanya mtu wangu tunayetoka tumbo moja, alienda huko akapata tabu sanaaaaa, alirudi akawadondokea wazazi miguuni akaomba msamaha wakamsamehe, ndani ya mwaka moja yuko mbali sana kimaisha leo ninavyoongea, ila alikuja na mtoto huko atokapo na shule alikataa, ujanja ni kuaga utafanikiwa usitoroke
 
Dah hadith yako kama ya uncle wangu nae alitoroka na alikuwa na akili tu shulen coz alimaliza form six, matokeo yake karudi mlevi matokeo yake wazazi wake na ndugu ndo wanakazi ya kumrudisha kwenye mstari na wameshindwa.

Yani hata leo akifa(siombei) hana hata suruali ya maana ya anko zake sie turithi.
Hahaaa sasa sisi alikua yupo form three , wenzake wakamdanganya akakimbilia mererani, ndugu walitafta sanaaa ikabahtika kujua alipo kwa kupitia rafiki yake mkubwa, mana tulijua amekufa mana mgodi aliokua akipiga kaz kuna kipindi ulifumuka ukaua karibu nusu ya watu. Basi rafk yake akatumwa akamdanganye kama Mama yako yu mahututi hospital washamrudisha nyumbani wanasema hamalizi week. Baaada ya siku mbili asubuh tunamuona anko. Alikua anakijibeg tuu eti kumbe bado ana mawazo ya kurud akishamsalimia mama, ukatumika ubabe kumzuia asiondoke mpk leo ndo Mwangalizi wa mali za familia kijijini. Baraka za wazazi ni muhimu sana kwenye kuchomoa kimaisha.
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] If bana mtu anasema niliaga wazazi halaf nikatoroka, sasa wewe si msafiri tuu. Duu kweli ulipo tupo kama Nisan patrol
 
washkaji na wana wanaokujaza upepo utoroke hom ukishasepa tu wote wanakukataa washkaj wanakuchekea ukiwa na kitu lakini hawataki uwabebeshe mzigo(mtaa ni mgumu sana)...asikwambie mtu kitu babu...we kaza hapo hapo home au aga halafu ndo usebenze...la sivyo utasanda ukashindwa kurud hom....usiharibu hom babu...
 
Movie za kihindi bana! We jaribu kutoroka uone....
 
Mi niliwahi kutoroka kurudi home nikarudi home na mawe ya kutosha lakini nilienda Somalia
 
Back
Top Bottom