Nani aliyemwapisha Spika na kwanini?

Tukikubaliana na anayosema Companero.. yawezekana kumbe Spika Sitta alikuwa anajipa nguvu ambazo hana (nadhani niliwahi kuliandika hili huko nyuma) kwa kujaribu kujiweka at par na Jaji Mkuu, na Rais? kwa kujiona yeye ni kiongozi wa Mhimili wa Serikali? Yawezekana sasa Spika Makinda atarudisha kwenye kuwa mratibu wa vikao na siyo mkuu wa mhimili na hivyo kuwa chini ya Rais. Kwa sababu ni kweli kuna matatizo ya mtiririko wa Mantiki:

a. Kuna mhimili mitatu ya Serikali - Utendaji (Rais), Mahakama (Jaji Mkuu) na Bunge (???)
b. Bunge lina sehemu mbili ambayo moja ni Rais na pili ni Wabunge.
c. Kama (b) ni kweli Spika hawezi kuwa Mkuu wa Mhimili wa Bunge kwani atakuwa ni Mkuu wa Rais (ambaye ni sehemu ya Bunge) vile vile kwani Rais ni Mkuu wa Mhimili mwingine na tunaambiwa mihimili hii haiingiliani (iko huru).
d. Kama a-c yote ni kweli kwa kiwango chake ina maana kuwa Bunge liko chini ya Rais na hapa ndiyo sababu kuna watu waliona kuwa kwa wabunge wa Chadema kutoka Bungeni wamemdhalilisha Mkuu wa Bunge ambaye ni Rais ...

well.. me so confused!
 
Mwanakijiji hili ni moja ya mapungufu mengi sana ya Katiba yetu. Ukweli ni kwamba hata wale wengi walio ndani ya uongozi wa serikali wanaona umuhimu wa kubadilisha hii katiba inayo tufanya wote tuonekane hamnazo.

Kwenye nchi kama US, spika huapishwa na Dean of the House, ambae ni muwakilishi wa muda mrefu katika baraza la wawakilishi. Ukweli ni kwamba ipo siku hii katiba either itamfunga mmoja wa watetezi au itatumaliza tulio wengi. Tunaitaji katiba mpya, JK anajua hilo, CCM wanajua hilo.
 
Nadhani spika kuapishwa na jaji mkuu rais sio sahihi kwa mtazamo wangu sababu Spika kama walivyo wabunge wanatakiwa kuwa na uhuru mpana zaidi wa kuchallenge katiba.
Sasa wabunge na spiker watachellenge vipi katiba na kuirekebisha kama wakiapishwa kwa misingi ya kuilinda?

Nahisi speaker kuapishwa na jaji Mkuu au hata Rias itakuwa ni ukiukwaji wa katiba vile vile.

Je kuna mtu anaweza kuteletea maneno yanyotamkwa na watu hawa wakiwa wanaapa?
Rais
Jaji Mkuu
Wabunge
Spika
 
Tukikubaliana na anayosema Companero.. yawezekana kumbe Spika Sitta alikuwa anajipa nguvu ambazo hana (nadhani niliwahi kuliandika hili huko nyuma) kwa kujaribu kujiweka at par na Jaji Mkuu, na Rais? kwa kujiona yeye ni kiongozi wa Mhimili wa Serikali? Yawezekana sasa Spika Makinda atarudisha kwenye kuwa mratibu wa vikao na siyo mkuu wa mhimili na hivyo kuwa chini ya Rais. Kwa sababu ni kweli kuna matatizo ya mtiririko wa Mantiki:

a. Kuna mhimili mitatu ya Serikali - Utendaji (Rais), Mahakama (Jaji Mkuu) na Bunge (???)
b. Bunge lina sehemu mbili ambayo moja ni Rais na pili ni Wabunge.
c. Kama (b) ni kweli Spika hawezi kuwa Mkuu wa Mhimili wa Bunge kwani atakuwa ni Mkuu wa Rais (ambaye ni sehemu ya Bunge) vile vile kwani Rais ni Mkuu wa Mhimili mwingine na tunaambiwa mihimili hii haiingiliani (iko huru).
d. Kama a-c yote ni kweli kwa kiwango chake ina maana kuwa Bunge liko chini ya Rais na hapa ndiyo sababu kuna watu waliona kuwa kwa wabunge wa Chadema kutoka Bungeni wamemdhalilisha Mkuu wa Bunge ambaye ni Rais ...

well.. me so confused!

Kweli hili swala linachanganya, ni wazi kabisa sehemu yakwanza kabisa inayochambua bunge inasema wazi bunge lina sehemu mbili na moja ya sehemu hizo raisi wa serikali ya Tanzania ni sehemu ya Bunge hilo. Jee hapa swala zima la bunge kuwa muhimili mkuu linatoka wapi?

Mwaka 2007 niliandikaga kuhusu Bunge nikasema Bunge letu ni la Vikaragosi, nikiweka wazi kabisa kwamba halina makali. Bunge halijapewa nguvu, bunge linaitwa kama mshauri wa serikali. Hapo hapo katiba inaweka wazi raisi ana haki ya kukataa ushauri wa mtu yoyote.

Siku mmoja niliongea na Bunge mmoja wa pwani tukijadili mambo mbali mbali ya Bunge, nikamuuliza jee ni kwa kiasi gani mbunge anaweza kuinfluance maendeleo jimboni kwake? Akanijibu ya kwamba Mbunge hana nguvu yoyote ya kuchagua either barabara ijengwe au isijengwe jimboni kwake, bali serikali kuu ndio muamuzi wa mwisho. Serikali ya Tanzania inanguvu kushinda bunge, na inauwezo wa kufanya itakalo pasipo uangalizi. dawa ni katiba mpya.
 
I read, read and read and the more I do it, the more I get confused. I can see everything is mixed up but sufficiently to say Something is missing in our Laws and regulations. Katiba Mpya, only KM can redress such imbalances
 
Hivi kwa nini tunataka kumshirikisha mungu katika sehemu ambayo tunalazimika kufuata sheria za kibinaadamu?

What if katiba anayoapa kuitekeleza inapingana na sheria za mungu wake anaemuamini?

Ukiapa kwa msahafu mathalan, kipi kinakuwa na nguvu ya maamuzi yako, katiba au msahafu? Ulichoapa au ulichoapia?

Na kwa wale wasioamini mungu jee?

Sheria za viapo katika nchi za kidemokrasia kama ya kwetu zinataka utumia vitabu vya dini yako. Ukitumia katiba kuapa kuwa utailinda katiba hiyo hiyo ni kiapo cyclic ambacho hakina maana yoyote kwa sababu ukiamua kuivunja katiba basi unahalaisha kuvunja kiapo chako moja kwa moja.
 
Nashawishika kukubaliana na wewe, lakini kwa kuwa mtu ambaye unaapa mbele yake ni wa muhimu, tunachoongelea ni kilekile labda tutafute neno jingine. hoja itarudi kuwa nani aape mbele ya nani? angalia hapa kwa mujibu wa katiba:

42(5) Kila Rais mteule na kila mtu atakayeshikilia kiti cha Rais,
kabla ya kushika madaraka ya Rais, ataapa mbele ya Jaji Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano, kiapo cha uaminifu na kiapo kingine
chochote …

49. Makamu wa Rais, kabla ya kushika madaraka yake
ataapishwa mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, kiapo
cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote …

51.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii na
ambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais
kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa
na Bunge.
56. Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka
awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia
kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake
kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

Kwa mujibu wa katiba, Rais na makamu wake wote wanaapa mbele ya Jaji mkuu! kwa hiyo suala linakuwa kwa nini Spika asiape mbele ya Jaji mkuu pia? especially kama ikiwa anaweza wakati fulani kuvaa viatu vya Rais, na pia kwa kuwa ni mmoja wa mihimili mikuu ya mamlaka ya Dola?

Hakuna wakati ambapo CJ anakaimu nafasi ya urais, soma tena Katiba uliyonayo!
 
Halafu tunakosea jambo moja. Rais haapishwi na Jaji Mkuu. Anaapa mbele ya Jaji Mkuu (42.5 ya Katiba ya JMT)
nilikuwa nafikiri hivyo pia, kwamba hapa kinachofanyika ni kuapa mbele ya fulani lakini si kwamba fulani anamuapisha fulani. kwanza tujiulize kwenye hati ya kiapo ni nani anayetia saini, anayeapa, au aliye mbele ya anayeapa au wote?. ubongo wangu unaniambia kwamba mtu anaapa siyo kuapiishwa.
 
Sheria za viapo katika nchi za kidemokrasia kama ya kwetu zinataka utumia vitabu vya dini yako. Ukitumia katiba kuapa kuwa utailinda katiba hiyo hiyo ni kiapo cyclic ambacho unaweza hakina maana ayoyote kwa sababu ukiamua kuivunja katiba basi unahalaisha kuvunja kiapo chako moja kwa moja.

Kwa kuongezea. Katiba ya Tanzania ina urithi wa taratibu za uingereza. Hivyo utaratibu wa kuapa ulikuwa na wa kutumikia ufalme. Hivyo tulipopata uhuru, tumebadilisha maneno yanayosemwa lakini vitendo vimeendelea kuwa vilevile.

Miaka ya zamani uingereza ilikuwa ni nchi ya dini moja na watu wote waliamini ufalme. Hivyo kiapo kilikuwa cha aina moja na mtu ilibidi atumie Biblia. Lakini kutokana na mabadiliko yaliopo sasa nchini uingereza, wabunge wanaruhusiwa kuapa kwa kutumia taratibu mbalimbali.

Kwa Tanzania inabidi taratibu zingine zitizamwe. Kama mtu anaweza kuapa kwa kisukuma, kichagga au kivyake let it go.
 
Hizi mihili mnazosema ni mbwembwe tu , hakuna kitu hapo.

Kwa katiba yetu tuna mhimili mmoja tu ambao unaongozwa na RAIS . Full stop. Hebu niulize kidogo je RAIS ana mamlaka ya kum-fire JAJI MKUU?
 
Tukikubaliana na anayosema Companero.. yawezekana kumbe Spika Sitta alikuwa anajipa nguvu ambazo hana (nadhani niliwahi kuliandika hili huko nyuma) kwa kujaribu kujiweka at par na Jaji Mkuu, na Rais? kwa kujiona yeye ni kiongozi wa Mhimili wa Serikali? Yawezekana sasa Spika Makinda atarudisha kwenye kuwa mratibu wa vikao na siyo mkuu wa mhimili na hivyo kuwa chini ya Rais. Kwa sababu ni kweli kuna matatizo ya mtiririko wa Mantiki:

a. Kuna mhimili mitatu ya Serikali - Utendaji (Rais), Mahakama (Jaji Mkuu) na Bunge (???)
b. Bunge lina sehemu mbili ambayo moja ni Rais na pili ni Wabunge.
c. Kama (b) ni kweli Spika hawezi kuwa Mkuu wa Mhimili wa Bunge kwani atakuwa ni Mkuu wa Rais (ambaye ni sehemu ya Bunge) vile vile kwani Rais ni Mkuu wa Mhimili mwingine na tunaambiwa mihimili hii haiingiliani (iko huru).
d. Kama a-c yote ni kweli kwa kiwango chake ina maana kuwa Bunge liko chini ya Rais na hapa ndiyo sababu kuna watu waliona kuwa kwa wabunge wa Chadema kutoka Bungeni wamemdhalilisha Mkuu wa Bunge ambaye ni Rais ...

well.. me so confused!

Rais ni sehemu ya Bunge lakini sio mkuu wa Bunge. Mkuu wa Bunge ni Spika, don't be confused!
 
Rais ni sehemu ya Bunge lakini sio mkuu wa Bunge. Mkuu wa Bunge ni Spika, don't be confused!

lakini Bunge lina sehemu mbili mojawa ni Rais na pili ni Wabunge - sasa Spika ni mkuu wa Wabunge au Mkuu wa Bunge lenye sehemu mbili? ambayo mojawapo ni Rais?
 
Back
Top Bottom