Nani aliyemwapisha Spika na kwanini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani aliyemwapisha Spika na kwanini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 22, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa nazungumza na mzalendo mmoja mwishoni mwa juma na akaniuliza maswali fulani yakitu ambacho labda hatukukiangalia kilipotokea.

  a. Rais akitangazwa kuwa Rais anaapishwa na Jaji Mkuu - Mkuu wa Mhimili
  b. Jaji Mkuu akiteuliwa anaapishwa na Rais - Mkuu wa Mhimili
  c. Spika akitangazwa kuwa Spika anaapishwa na Katibu wa Bunge - mtumishi wa Umma (Civil servant).

  Katika mazungumzo yangu na mkulu huyo mmoja jingine likajitokeza:

  a) Wabunge wanakuwa Wabunge wakati gani? - Wanapotangazwa na RO kuwa wameshinda na hasa inaposemwa "Namtangaza X,Y kuwa ni Mbunge halali wa Jimbo la M" au
  b) Anapokuja Bungeni na kula kiapo cha Ubunge?

  Kama jawabu ni (a) kwanini Mbunge huyo asiapishwa hapo hapo kuwa Mbunge na anasubiri kuja Bungeni kuapishwa wakati tayari ametangazwa kuwa ni Mbunge?

  Kama jawabu ni (b) kwanini RO anamtangaza mtu kuwa Mbunge badala ya kumtangaza tu kuwa ameshinda kura za Ubunge na anakuwa "Mbunge Mteule" hadi pale atakapoapishwa?

  Tulipoliangalia hilo tukajikuta tunaingia kwenye tatizo jingine:

  Wabunge "wateule" wanapopiga kura kumchagua Spika wanapata wapi hizo nguvu hizo wakati hawajaapa kuilinda na kuitetea Katiba? Aidha ni wabunge au siyo kama ni wabunge kwanini wakishamchagua Spika huyo Spika ndio anawaapisha wao kuwa wabunge?

  Well.. I'm confused enough.. and talk about "no need for a new constitution"...
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Nov 22, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Yote uliyoongea ni sehemu ya mapungufu ya Katiba yetu. Hata hivyo kuhusu mbunge, ninadhani kuwa anakuwa mbunge mara tu baada ya kuchaguliwa na watu wake na kutangazwa na returning officer. Kuapishwa bungeni hufanyika ili kumruhusu kushiriki mijadala ya bunge; asipoapishwa na bunge hawezi kukosa ubunge wake lakini nadhani hataruhusiwa kushiriki mijadala ya bungeni.

  katiba na sheria zetu zina mapungufu mengi sana ikiwa na pale waapaji wanapoamua kwa makusudi kutokutumia misahafu ya dini zao.
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mwakei,

  Mbona wewe unaleta vurugu na kuchokonoa ilhali bado hatujajua kura za Urais tunazitatua vipi? Nawe umezidi ubundi!
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hivi kwa nini tunataka kumshirikisha mungu katika sehemu ambayo tunalazimika kufuata sheria za kibinaadamu?

  What if katiba anayoapa kuitekeleza inapingana na sheria za mungu wake anaemuamini?

  Ukiapa kwa msahafu mathalan, kipi kinakuwa na nguvu ya maamuzi yako, katiba au msahafu? Ulichoapa au ulichoapia?

  Na kwa wale wasioamini mungu jee?
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji, if you were a teacher... (or if you are a teacher as i write) you students must be very lucky, though lazy ones would complain, umepembua hadi ukakuta mchele una ngano kidogo

  big up! najifunza everyday namna ya kuangalia issues zinazohusu haki za raia na wajibu wao
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkjj umeanza uchochezi eti??? hahah ahaha ahaha! muda si mrefu Wazee wa DSM wataandamana kushutumu uchochezi wako! Hahaha ahaha.

  Anyways, Good one bro! najiuliza kwa nini miaka yoote hii hili jambo halikuwahi kuongelewa. Au ndiyo ule utaratibu kwamba serikali ikisema, ikipanga, ikifikiri haikosei.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  kwa kweli hili hata mimi sikulifikiria hadi nilipozungumza na huyu ndugu Ijumaa ambaye ni mtumishi kigogo tu wa serikali hii; kuna maswali mengine ambayo aliniuliza na naona hata woga kuyauliza maana wasije kunifanyia press conference bure.. I mean kina Chiligati au Waziri ajaye wa Habari na Utamaduni..
   
 8. M

  Mindi JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2010
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Kwanza nakushukuru sana mkuu kwa kuitendea haki JF - kweli ni "home of great thinkers", kwa hoja kama hizi. sasa nilipitisha macho haraka kwenye katiba yetu, angalau nakala niliyonayo inaeleza yafuatayo
  1. Mbunge aliyechaguliwa na wananchi katika uchaguzi atakuwa mbunge baada ya kutangazwa na Tume ya uchaguzi, kwa kuwa ndiyo yenye mamlaka kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya katiba, ibara ndogo 6(b). RO anafanya kazi kwa maagizo ya Tume ya uchaguzi, lakini ni Tume yenyewe yenye mamlaka ya kutangaza. aidha katika ibara hiyohiyo, ibara ndogo ya 12 inasema:

  "Hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya
  kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika​
  kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii."

  kwa hiyo hata kama Tume imechakachua, haiwezekani kuihoji uchakachuaji wake.

  2. Ibara ya 68 ya katiba inasema:
  "Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha
  uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini
  Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla​
  hajaapishwa."

  Maana yake huyu ni mbunge tayari, ila ili aweze kushiriki shughuli za Bunge, imempasa kula kiapo cha uaminifu. naona watunga katiba waliliona hili unalolisema na ndio maana wakaweka hiyo "provision" ya kumchagua Spika kabla ya wao wenyewe kuapishwa.

  Kimsingi nakubaliana kwamba katiba hii haitufai kwa sasa na tunahitaji katiba mpya. naona ndio msingi wa hoja yako
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mindi asante sana.. lakini hujajaribu kugusia nani anamwapisha Spika na kwa nini? Najua sheria na Katiba inasema nini.. ninaulizia something deeper kidogo.. kwanini SPIKA haapishwi na Jaji MKUu kama Rais anavyoapishwa?
   
 10. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Hili la kuaapa kuna jambo! inamaana bunge lina hadhi ndogo kiasi hiki? kwamba Mkuu wake anaapisha hovyo hovyo tu?sikuwahi fikiria
   
 11. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #11
  Nov 22, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  mwanakijiji,tunashukuru kwa hoja nzuri,ni kweli bado kunatatizo ktk katiba ya hii nchi,haiwezekani katibu wa bunge kumwapisha spika wa bunge ambe anaongoza mhimili wa 3 wa serikali,lakini pia tutambuwe kuwa mwakilishi aliyechaguliwa na wapigakura ni mbunge tosha na anaitwa mteule kwa kuwa bado hajapata baraka za spika,ila hilo halimzuii yeye kuwa mbunge,haya mengine ya wabunge kumchaguwa spika then huyo spika kuwaapisha wabunge ni utaratibu tu ambao hauna msingi wowote ule

  mapinduziiiii daimaaaaaa
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Labda tuanzie hapa: KATIBU wa BUNGE anateuliwaje? Sifa zake ni zipi? Ana hadhi sawa na JAJI wa Mahakama kuu? ROs ambao karibu wote ni WAKURUGENZI wa Halmashauri/Manispaa/miji wanao uwezo KIKATIBA kumtangaza mtu kuwa ni DIWANI/MBUNGE? Viapo hivi vya kushika vitabu vitakatifu badala ya KATIBA ya NCHI sio UDINI kweli wakati tunasema kila mara NCHI yetu haina DINI?
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Nov 22, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Halafu tunakosea jambo moja. Rais haapishwi na Jaji Mkuu. Anaapa mbele ya Jaji Mkuu (42.5 ya Katiba ya JMT)
   
 14. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  MMK,
  Usihofu kuyauliza,kwani ndo twajifunza kupia kwayo.
   
 15. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #15
  Nov 22, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  kuna tofauti gani hapo mkuu?
  basi kama ni hivyo hata Jaji mkuu haapishwi na rais bali anaapa mbele ya rais.
  Mi naona ni lugha tu hapo ndugu yangu.
   
 16. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #16
  Nov 22, 2010
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Thats why i like JF, unapata upembuzi yakinifu! ila wakija wanasihasa wataharibu sasa hivi badala ya kujenga hoja. Ahsanteni sana
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Nov 22, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Jaji Mkuu ni SHAHIDI kwa niaba yetu na KATIBA ya JMT.
   
 18. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #18
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  nimebaki kucheka tu

  kwel tunahitaji katiba mpya
   
 19. Companero

  Companero Platinum Member

  #19
  Nov 22, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji kwa mujibu wa Mwanasheria wa Katiba aliyebobea nchini, katika muundo wa Tanzania, Spika sio Kiongozi wa Mhimili wowote wa Uongozi. Inabidi ufikiri sana uelewe hoja hii - walinganishe Rais, Jaji Mkuu na Spika wa Bunge utaona kuwa hao wawili wa kwanza ndio wana madaraka katika mihimili yao, yaani Serikali na Mahakama. Kwa maana nyingine, Spika sio Kiongozi wa Bunge - ni muendeshaji/mratibu (modereta) tu!
   
 20. Mpenda Kwao

  Mpenda Kwao Senior Member

  #20
  Nov 22, 2010
  Joined: Apr 29, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii nimeipenda kwani umeutendea vema mtandao " The Home of Great Thinkers" Big up MKJJ. Kama msemo wa Entrepreneurs unaosema " When others see darkness good entrepreneurs see light".

   
Loading...