Nani aliyemwapisha Spika na kwanini?

Nilikuwa nazungumza na mzalendo mmoja mwishoni mwa juma na akaniuliza maswali fulani yakitu ambacho labda hatukukiangalia kilipotokea.

a. Rais akitangazwa kuwa Rais anaapishwa na Jaji Mkuu - Mkuu wa Mhimili
b. Jaji Mkuu akiteuliwa anaapishwa na Rais - Mkuu wa Mhimili
c. Spika akitangazwa kuwa Spika anaapishwa na Katibu wa Bunge - mtumishi wa Umma (Civil servant).

Katika mazungumzo yangu na mkulu huyo mmoja jingine likajitokeza:

a) Wabunge wanakuwa Wabunge wakati gani? - Wanapotangazwa na RO kuwa wameshinda na hasa inaposemwa "Namtangaza X,Y kuwa ni Mbunge halali wa Jimbo la M" au
b) Anapokuja Bungeni na kula kiapo cha Ubunge?

Kama jawabu ni (a) kwanini Mbunge huyo asiapishwa hapo hapo kuwa Mbunge na anasubiri kuja Bungeni kuapishwa wakati tayari ametangazwa kuwa ni Mbunge?

Kama jawabu ni (b) kwanini RO anamtangaza mtu kuwa Mbunge badala ya kumtangaza tu kuwa ameshinda kura za Ubunge na anakuwa "Mbunge Mteule" hadi pale atakapoapishwa?

Tulipoliangalia hilo tukajikuta tunaingia kwenye tatizo jingine:

Wabunge "wateule" wanapopiga kura kumchagua Spika wanapata wapi hizo nguvu hizo wakati hawajaapa kuilinda na kuitetea Katiba? Aidha ni wabunge au siyo kama ni wabunge kwanini wakishamchagua Spika huyo Spika ndio anawaapisha wao kuwa wabunge?

Well.. I'm confused enough.. and talk about "no need for a new constitution"...
sasa mkuu tujaribu kuangalia hili swala kiundani kama RO anaweza kumtangaza na kumdhibitisha Mbunge papo kwa hapo hilo ni bao laweza kuwa bao lingine kwa demokrasia maana Mkulu amepewa urais kwa namuna hiyo sasa nathani kuapa Bungeni ni muhimu kumdhibitisha Mbunge na RO abaki akitangaza Mshindi tu...
 
Kisoda na Nyambala tuendelee: Ibara ya ya 62(3)(a) inasema hivi:

Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza: Kumuuliza Waziri yeyote swali lolote kuhusu mambo ya Umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;

Sasa, je, huyu Spika ambaye watu wanamuona ana madaraka katika mhimili wake mithili ya Rais na Jaji Mkuu katika mihimili yao, anaweza kumuuliza Waziri yeyote wa Serikali swali lolote au anaratibu tu Wabunge na Kamati zao ambao wao ndio wanaweza kuuliza hivyo? Kumbuka hapo juu tumeona tafsiri mbili za Bunge - yaani:

Bunge = Rais + Wabunge
Bunge = Sehemu ya Pili ya Bunge = Wabunge

Narudia kusisitiza: Spika ni Mratibu/Modereta tu wa Wabunge - zaidi ya hapo hana meno!

Nafurahi sana kupata hizi data mkuu, ila hii imekaaje pale tunapo ambiwa kuwa rais na makamu wake wasipokuwepo nchini spika anachukua madaraka ya urais kwanza kabla ya jaji mkuu?
je huu sinimchuzi mix hapa katika katiba hiyo hiyo?
Na kama katiba inampa uwezo huo wa kushika madaraka makubwa hivyo iweje asiape mbele ya jaji mkuu?
 
Mwanakijiji ameshalijibu hili swali hapo juu - anasema siku hizi hakaimu.

Hivyo Spika hana madaraka makubwa hivyo - madaraka yake ni haya tu:

"...atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge" - Ibara 84(1)

Zingatia kuwa kuwakilisha huko ndio kwenye sherehe za kuapishana, kwenye mikutano ya mabunge mbalimbali duniani n.k.

Tena Spika aliyepita hata hakustahili kujibishana na Jaji Mkuu kama alivyofanya - madaraka yake ni kuratibu (Wa)Bunge.

Swali: Nini hasa maana ya kuwa "kiongozi wa Bunge"?
 
Mindi asante sana.. lakini hujajaribu kugusia nani anamwapisha Spika na kwa nini? Najua sheria na Katiba inasema nini.. ninaulizia something deeper kidogo.. kwanini SPIKA haapishwi na Jaji MKUu kama Rais anavyoapishwa?

Ipo siku mkuu wa wilaya atamwapisha mkuu wa mkoa! MMKJ kwani unafikiri hawajui utata wa katiba! la muhimu tumo mbele taifa baadaye. Tumeweka viraka hadi tunashuhudia haya.
Kuongezea hoja yako, Mwanasheria mkuu ambaye pia ni mbunge anaapishwa na rais. Spika na katibu wake.
 
Companero... kiongozi wa Bunge maana yake wabunge wakipanga mstari yeye anakuwa wa kwanza wao. Au wanapokaa kwenye mikutano yeye ndiye prominent member. Na anamadaraka juu ya wabunge na mambo yao na jinsi wanavyozungumza Bungeni na masuala ya wabunge tu. Nadhani hapa ndipo watu watamkumbuka Sitta kwa sababu yeye alijaribu kulipa Bunge nguvu kidogo japo bila kuwa na singi wa Kikatiba. Mama Makinda yeye anataka kuwa ni Spika wa taratibu na kanuni za Bunge kwa hiyo hana mpango wa kuliinua Bunge kuwa ni Mhimili wa Serikali.
 
Tena hapa kuna tatizo jingine Mwanasheria Mkuu anakula kiapo cha Ubunge vile vile?
 
Mkuu tutumie mifano halisi kuelezea hili suala tata na tete la madaraka ya Spika wa Bunge - tuanze na swala la Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge kuhusu Kampuni ya Richmond; enhe Spika alikuwa Kiongozi wa Bunge kivipi hapa katika kusimamia Serikali itekeleze maazimio hayo?
 
Ndio maana nimesema inahitaji kufikiri sana kuelewa hili suala. Ni hivi: Bunge kweli ni Mhimili mmojawapo. Ila Spika sio Mkuu wa Mhimili huo. Kama huamini soma kwa makini Ibara hii ya 62 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kama ilivyorekebishwa 2005:

Ndiyo Bunge ni Muhimili mmojawapo hali sioni tatizo hapa.

Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge.

Sasa, je, Spika ni Kiongozi/Mkuu wa 'Rais na Wabunge', yaani, Kiongozi/Mkuu wa Bunge lenye sehemu mbili?

Hapa sasa ndipo rais amepewa nguvu ya kuwa juu ya Bunge na Spika kubakia kama Kiranja wa shule ya Chekechea.

Nimeshasisitiza hapo juu kuwa kiukweli hakuna Kiongozi wa Bunge, tuna mratibu/muendeshaji tu wa mijadala ya kufikia maamuzi wa Wabunge - rejea kwa makini Ibara hizi za 62 (1), 62 (3) na 84(4) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kama ilivyorekebishwa 2005 uone huo utata.

Ibara ya 62 (1) inasema Bunge lina sehemu mbili, "yaani Rais na Wabunge"
Ibara ya 62 (3) inasisitiza Rais na Wabunge ni "sehemu zote mbili za Bunge"
Ibara ya 84(4) inadai kuwa "Spika ndio Kiongozi wa Bunge..."

Swali la msingi hapa ni: Je, ni Kiongozi wa 'Bunge' au 'Wabunge'?

Swali la nyongeza ni: Je, anaongoza Bunge au Wabunge?

Rejea: "Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kusimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano..." ( Ibara ya 62 (2) ya Katiba)

Je, kweli Spika ndiye Kiongozi mwenye madaraka haya ya kusimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano?

Red: Ukiangali kwa makini Spika ni Mbunge hivyo anakuwa na madaraka ya Ubunge wa kusimamia na kuishauri serikali ya jamhuri ya Muungano kama mbunge siyo kama Spika.

Kisoda na Nyambala tuendelee: Ibara ya ya 62(3)(a) inasema hivi:

Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza: Kumuuliza Waziri yeyote swali lolote kuhusu mambo ya Umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;

Sasa, je, huyu Spika ambaye watu wanamuona ana madaraka katika mhimili wake mithili ya Rais na Jaji Mkuu katika mihimili yao, anaweza kumuuliza Waziri yeyote wa Serikali swali lolote au anaratibu tu Wabunge na Kamati zao ambao wao ndio wanaweza kuuliza hivyo? Kumbuka hapo juu tumeona tafsiri mbili za Bunge - yaani:

Bunge = Rais + Wabunge
Bunge = Sehemu ya Pili ya Bunge = Wabunge

Narudia kusisitiza: Spika ni Mratibu/Modereta tu wa Wabunge - zaidi ya hapo hana meno!

Kimsingi naye anapaswa kuwauliza sawa na wabunge lakini nadhani kuwana mazoea kwamba Spika hawezi kuuliza yeye pia ni mbunge, tatizo itikadi za vyama (U-CCM) anaogopa kuwauliza mawaziri ila ni haki yake naye kuuliza swali.

Tukikubaliana na anayosema Companero.. yawezekana kumbe Spika Sitta alikuwa anajipa nguvu ambazo hana (nadhani niliwahi kuliandika hili huko nyuma) kwa kujaribu kujiweka at par na Jaji Mkuu, na Rais? kwa kujiona yeye ni kiongozi wa Mhimili wa Serikali? Yawezekana sasa Spika Makinda atarudisha kwenye kuwa mratibu wa vikao na siyo mkuu wa mhimili na hivyo kuwa chini ya Rais. Kwa sababu ni kweli kuna matatizo ya mtiririko wa Mantiki:

a. Kuna mhimili mitatu ya Serikali - Utendaji (Rais), Mahakama (Jaji Mkuu) na Bunge (???)
b. Bunge lina sehemu mbili ambayo moja ni Rais na pili ni Wabunge.
c. Kama (b) ni kweli Spika hawezi kuwa Mkuu wa Mhimili wa Bunge kwani atakuwa ni Mkuu wa Rais (ambaye ni sehemu ya Bunge) vile vile kwani Rais ni Mkuu wa Mhimili mwingine na tunaambiwa mihimili hii haiingiliani (iko huru).
d. Kama a-c yote ni kweli kwa kiwango chake ina maana kuwa Bunge liko chini ya Rais na hapa ndiyo sababu kuna watu waliona kuwa kwa wabunge wa Chadema kutoka Bungeni wamemdhalilisha Mkuu wa Bunge ambaye ni Rais ...

well.. me so confused!

RED; Mhimili wa tatu ni Bunge ambaye anayesimama kama alama yake ni Mbunge na kiongozi wao ni Spika, lakini amepokwa nguvu kijanja hajijui.

Mwanakijiji hili ni moja ya mapungufu mengi sana ya Katiba yetu. Ukweli ni kwamba hata wale wengi walio ndani ya uongozi wa serikali wanaona umuhimu wa kubadilisha hii katiba inayo tufanya wote tuonekane hamnazo.

Kwenye nchi kama US, spika huapishwa na Dean of the House, ambae ni muwakilishi wa muda mrefu katika baraza la wawakilishi. Ukweli ni kwamba ipo siku hii katiba either itamfunga mmoja wa watetezi au itatumaliza tulio wengi. Tunaitaji katiba mpya, JK anajua hilo, CCM wanajua hilo.

Hapa nami nakubaliana na mabadiliko ya katiba haraka lakini kabla ya hayo mabadiliko kuna haja ya kuangalia kwa makini kwa mijadala wai kama hii vipengele vingi sana.
 
Jamani hebu tuelemishane kidogo, kwa katiba yetu ilivyo, mfano katika uchaguzi wa juzi, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi NEC Jaji Lewis Makame angeamua tu kumtangaza Dr. Wilbroad Slaa hata kama idadi ya kura inaonyesha yuko chini, kisheria kungetokea nini?

I mean kama namna matokeo yalivyotangazwa Zanzibar
 
Tena hapa kuna tatizo jingine Mwanasheria Mkuu anakula kiapo cha Ubunge vile vile?

Ndio. Jaji FM Werema alikuwa wa kwanza kula kiapo hiki. Sikumwona Spika wa sasa akila kiapo hiki ingawa kile cha Uspika aliapa. Viapo vyenyewe vina maana basi? Wakishaapa wanaendelea na madili yao kama kawa. Viapo hivi kama vile vya NDOA kwa WATANZANIA ni MAIGIZO tu. Nilimuuliza rafiki yangu mmoja ile pete ya ndoa akienda "gesti" anaiweka wapi? Alicheka tu.
 
Jamani hebu tuelemishane kidogo, kwa katiba yetu ilivyo, mfano katika uchaguzi wa juzi, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi NEC Jaji Lewis Makame angeamua tu kumtangaza Dr. Wilbroad Slaa hata kama idadi ya kura inaonyesha yuko chini, kisheria kungetokea nini?

I mean kama namna matokeo yalivyotangazwa Zanzibar

Anatangazwa MSHINDI tu.
 
Back
Top Bottom