Lini haswa tulianza kuwahesabu wanawake na watoto kwenye mambo ya Mungu na mengineo ya msingi? Tukirudi nyuma hata idadi ya waliolishwa mikate na Yesu, watoto na wanawake hawakuwepo kwenye ile idadi, na kuna mifano mingine mingi. Wachungaji wanawake ni wengi sana siku hizi sasa hivi utasikia Azana za wanawake misikitini any way.
Nani haswa aliwaingiza wanawake kwenye idadi ya watu? Maana hii dhambi/ au niseme huu udhaifu wa wanaume unaanza kututafuna wanadamu kimya kimya ikianzia na Ujerumani, Uingereza na hata taifa kubwa duniani Marekani soon linaingia kwenye mtego wa wanawake.
Najua kuna mtakao shindwa kuona hoja yangu, pole yenu.
Kwa mlioiona tafadhali athari yake nini hii kitu?
Baadhi ya wanawake walioshamiri kwenye agano la kale
1.Debora -Huyu alikuwa Muamuzi na Nabii -soma habari zake Waamuzi 4-5
Waamuzi 4:4Wakati huo, kulikuwa na nabii mwanamke aliyeitwa Debora, mke wa Lapidothi, aliyekuwa mwamuzi wa Waisraeli wakati huo. 5Debora alikuwa na mazoea ya kuketi chini ya mtende uliokuwa kati ya mji wa Rama na mji wa Betheli katika nchi ya milima ya Efraimu. Watu wa Israeli walimjia ili awaamulie mashauri yao. 6Siku moja alimwita Baraki mwana wa Abinoamu wa Kedeshi katika nchi ya Naftali. Alipokuja alimwambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anakuamuru hivi: ‘Nenda ukusanye watu wako mlimani Tabori, uchague watu 10,000 kutoka makabila ya Naftali na Zebuluni. 7Mimi nitamchochea Sisera, jemadari wa jeshi la Yabini, aje na majeshi na magari yake kupigana nawe kwenye mto Kishoni, na kumtia mikononi mwako.’
2.Huldah -nabii 2WAFALME 22:14, 2Mambo ya nyakati 34:22
3.Noahdiah-Nehemiah 6:14
4.Isaya 8:3 3Nililala na mke wangu ambaye pia ni
nabii, akapata mimba, akajifungua mtoto wa kiume. Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Mpe mtoto huyo jina ‘Teka-haraka-pokonya-upesi.’ 4Maana kabla mtoto huyu hajafikia umri wa kuweza kutamka: ‘Baba’ au ‘Mama,’ utajiri wa Damasko na nyara walizoteka huko Samaria zitapelekwa kwa mfalme wa Ashuru.”