Nani alisema TBS wanapima bidhaa kabla ya kuingia sokoni!

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,652
22,250
Kwenye taarifa ya habari ITV leo saa mbili usiku TBS wamesema wataiondoa sokoni juisi ya Ceres Apple yenye sumu! Kuondoa huku kinafuatia TBS kusikia nchi nyingine zikiondoa juisi hiyo ya toleo husika na si matoleo mengine. Baada ya kusikia!

TBS ilienda kwenye godauni ya muagizaji ambaye kwa bahati nzuri ni mmoja tu nchini, tujielize kwanini hawapimi vyakula kabla ya kuingia sokoni? Je, wako bize kupima magari toka Japani?

Ni wakati muafaka kwa serikali kuunda mamlaka pekee itakayohusika na upimaji wa vyakula vyote vya nchini na viingiavyo nchini.
 
Mbona sidhani kama ni kazi ya TBS bali kazi ya TFDA, hiyo taarifa umeona TBS ndio wanatekeleza hili. Labda sijui utendaji kazi wanafanana vipi

Hata hivyo tupime au tusipime, tatizo linajulikana na hata wasingechukua hatua yoyote bado Ceres ya SA ime-recall batch nzima ya juice zenye shida. Shida yenyewe ndogo tu
 
Soma barua yao waliotoa inamelezo yote
Nimeandika kutokana na maelezo ya msemaji wa TBS kwenye taarifa ya habari ITV, amesema walikwenda kagua kwenye godauni kama zipo! Bahati nzuri ziko njiani zinakuja laki pia wamewataka wananchi wasinunue toleo husika! Haina ubishi kutokana na maelezo hayo hawapimi ziingiapo nchini.
 
Mbona sidhani kama ni kazi ya TBS bali kazi ya TFDA, hiyo taarifa umeona TBS ndio wanatekeleza hili. Labda sijui utendaji kazi wanafanana vipi

Hata hivyo tupime au tusipime, tatizo linajulikana na hata wasingechukua hatua yoyote bado Ceres ya SA ime-recall batch nzima ya juice zenye shida. Shida yenyewe ndogo tu
Ni TBS, utakuwa haukufuatilia Post iliyohusu unga wa mahindi na muhogo.
 
Hakuna wanachopima! TBS wanakamata na kuchoma kwa mujibu wa kilichoandikwa au kusemwa na wengine.

Tunaingiza betri nyingi sana za magari na mitambo mikubwa, zinapaswa kuishi kwa zaidi ya miaka 2 kwa mujibu wa mtengenezaji, ila hizi tunazonunua hapa, zikidumu kwa miezi 7 una bahati, zinaingiaje kwa wingi wake kama TBS wanapima?

Wanaenda kukamata bidhaa kwa mangi na si kwenye ports, wale watu wawili wanapimaje pale kwa mangi?

Waya za umeme zilizo kwenye soko letu, nyingi ni chuma, earth rod ni chuma/nondo, wao wanapima nini?

Extension cables mbovu na hatari kwa jamii, ziko madukani, zimepitishwaje na wao?

Vipi kuhusu walaji wa mwisho wanaonunua kuku wa kisasa, nyama mabuchani, mboga za majani n.k, kuna standards zozote walizozitoa na kufiatilia kuwa zinafikiwa?

Nimeagiza kifaa, TBS wakachukua kwenda kukipima ilhali nikijua hakuna watakachopima kwakuwa kiko nje ya uwezo wao, baada ya kukaa nacho wiki 3, wakakitoa kuwa kiko up to standard, ajabu ni kwamba, kilipofika eneo husika hakikufanya kazi na baada ya kukichunguza tukaona ni kibovu, tukakirudisha, tumeletea kingine, wakakichukua tena kwa ukaguzi!

Ni mengi, ila kimsingi jua wako busy kupeana safari za nje zisizo na tija kwa taifa kama TPDC wafanyavyo, wanaagiza sampuli kwa wingi, wanagawana sampuli hizo, wanachelewesha mambo kwa makusudi ku-buy sometime
 
Hii tabia ipo karibia kila sekta yan
 
Hii tabia ipo karibia kila sekta yan
TBS inaendeshwa kwa mtindo wa GURU ni kama dampo ambamo kila takataka imo! TBS wanapima viwango vya kondom, mazagazaga mengine mpaka vyakula! Katika hali ya kawaida hawawezi kuwa na ufanisi, inatakiwa iwepo mamlaka itakayohusika kupima viwango vya ubora na sumu kwenye vyakula na TBS kuthibitisha tu.
 
Mbona sidhani kama ni kazi ya TBS bali kazi ya TFDA, hiyo taarifa umeona TBS ndio wanatekeleza hili. Labda sijui utendaji kazi wanafanana vipi

Hata hivyo tupime au tusipime, tatizo linajulikana na hata wasingechukua hatua yoyote bado Ceres ya SA ime-recall batch nzima ya juice zenye shida. Shida yenyewe ndogo tu
Hivi sasa hakuna taasisi inaitwa TFDA ndani ya Jamuhuri yetu pendwa !
 
Mbona sidhani kama ni kazi ya TBS bali kazi ya TFDA, hiyo taarifa umeona TBS ndio wanatekeleza hili. Labda sijui utendaji kazi wanafanana vipi

Hata hivyo tupime au tusipime, tatizo linajulikana na hata wasingechukua hatua yoyote bado Ceres ya SA ime-recall batch nzima ya juice zenye shida. Shida yenyewe ndogo tu
TFDA waliondolewa ishu ya chakula wamebaki na mambo ya dawa tu muda mrefu kidogo...
 
Utafiti wa chombo gani ulipiga marufuku mafuta ya kula yatokanayo na mbegu za ubuyu?

Ni kweli yana madhara au ilikua mgongano wa maslahi na mambo ya biashara tu?
 
Nikiangalia vichaja vya kichina ambavyo hata wiki Moja huwa haiishi kabla havijaungua ukichajia simu,, hapo ndio naonaga TBS ni kama kikundi Fulani hivi kisichoeleweka
 
TBS walikua wanafanya kazi enzi za mkurugenzi aitwaye Mwakyembe. (Sio yule ma degree)
Kuna siku tuliingiza kondom za promotion, kwa kweli zilipimwa na kuonekana unfit. Tulijaribu kuhonga lkn mzee alisema hachezi na Maisha ya mtu.
Kipindi chake matairi, maji, beer na vyakula vingi lazima vilipimwa na kupewa usajili wa haki.
Alipokuja Ekelege ni maji ya kandoro tu ndio hayakupata usajili.
Siku hizi tumeenda chini zaidi ukwaju wa MO nao ulipata usajili.
Kesho utasikia kumeingizwa kinywaji kinaitwa Shit energy na kitasajiliwa.
 
Kupima vitu lazima uvijue, uwe na watu na vifaa vya kufanya hivyo.
Duniani vinazalishwa vitu vingi sana, na kwa vyovyote vile, TBS yenyewe haiwezi kuvipima vyote. Kunahitajika maabara nyingi sana za kupima kulingana na mahitaji ya walaji na wazalishaji ili TBS awe regulator tu.
Kwa sababu ya ukiritimba na ujinga kuanzia serikalini, wote tunaamini uwezo na ulinzi wa TBS ambao hauko hivyo.
 
Mbona sidhani kama ni kazi ya TBS bali kazi ya TFDA, hiyo taarifa umeona TBS ndio wanatekeleza hili. Labda sijui utendaji kazi wanafanana vipi

Hata hivyo tupime au tusipime, tatizo linajulikana na hata wasingechukua hatua yoyote bado Ceres ya SA ime-recall batch nzima ya juice zenye shida. Shida yenyewe ndogo tu

Hakuna TFDA kwa sasa ndugu! Ipo TMDA
Hebu kuwa updated japo kidogo!
Kwa sasa mamlaka inayohusika na vyakula ni TBS
 
Nikiangalia vichaja vya kichina ambavyo hata wiki Moja huwa haiishi kabla havijaungua ukichajia simu,, hapo ndio naonaga TBS ni kama kikundi Fulani hivi kisichoeleweka
Ndugu yangu hao TBS, muda mwingi utendaji wao ni kujaribu kuweza kupata ' hela ya brashi' ili waishi kadri itakavyowezekana....
 
Kwenye taarifa ya habari ITV leo saa mbili usiku TBS wamesema wataiondoa sokoni juisi ya Ceres Apple yenye sumu! Kuondoa huku kinafuatia TBS kusikia nchi nyingine zikiondoa juisi hiyo ya toleo husika na si matoleo mengine. Baada ya kusikia!

TBS ilienda kwenye godauni ya muagizaji ambaye kwa bahati nzuri ni mmoja tu nchini, tujielize kwanini hawapimi vyakula kabla ya kuingia sokoni? Je, wako bize kupima magari toka Japani?

Ni wakati muafaka kwa serikali kuunda mamlaka pekee itakayohusika na upimaji wa vyakula vyote vya nchini na viingiavyo nchini.
Achana na TBS mkuu, fanya mambo yako. Hiyo ni mamlaka ilishawekwa.
 
Back
Top Bottom