Dondoo 5 muhimu kabla hujanunua bidhaa ya chakula

Dondoo 5 muhimu kabla hujanunua bidhaa ya chakula

Mema Tanzania

Member
Joined
Feb 23, 2020
Posts
66
Reaction score
65
Umewahi nunua chocolate ile unaipiga paap! inapukutika kama biscuits? Ujue umenunua bidhaa ambayo imekwisha muda wake. Kabla hujanunua bidhaa za kula ni vyema ukazingatia dondoo zifuatazo.

Tips9.png


1. Jina halisi ya bidhaa

Vyema ukajiridhisha bidhaa unayonunua jina lake halisi ni lipi kwani sokoni kuna bidhaa nyingi fake.

Tips10.png


2. Muda wa matumizi

Kila bidhaa ina muda wake wa mwisho kwa matumizi. Tizama kwa umakini kufahamu, kuepusha kutumia bidhaa zilizopita muda wake.

Tips11.png


3. Alama ya ubora

TBS ndiyo yenye kuthibitisha ubora wa bidhaa zote nchini pia zikiwepo mamlaka za chakula na dawa na shirika la viwango vya kimataifa ISO. Tazama kama bidhaa unayo nunua imewekewa chapa ya ubora.

Tips12.png


4. Ufungaji wa bidhaa

Tazama kwa umakini bidhaa unayonunua kama haijafunguliwa. Vinywaji, nafaka na vyakula vya kusindika ni rahisi kuwa na upenyo kama hazikufungwa vizuri.

Tips13.png


5. Mzalishaji/Msambazaji wa bidhaa

Kagua kwa umakini kuona bidhaa unayo nunua ni kampuni gani inazalisha au/kusambaza. Hii itakusaidia unaponunua bidhaa isiyo na ubora kujua ni msambazaji au mzalishaji gani unapaswa kumfikishia malalamiko.

Tips14.png


Unapoenda kununua bidhaa huzingatia vitu gani vingine? Tiririka kwenye comment 👇

#MemaTips #Jiongeze

Tufuate! Facebook, Instagram, Twitter na Medium / Mema Tanzania
 
Back
Top Bottom