Expedito Mduda
JF-Expert Member
- Sep 22, 2009
- 522
- 240
hatuezi kuendelea bila elimu au kwa kutoa shahada za kujipendekeza kwa viongozi.maprof wawe makini na taruma zao...!!
Muda si mwingi tutaipata Tanganyika. Muhimu tukubali kuidai kwa nguvu zetu zote. Alilianzisha Mtikila, mkamuona mwehu, sasa mmeanza kujionea jinsi mke wetu Zanzibar alivyoanza kujibaraguza, anadai haki sawa kwa mke na mume. Enheheheheheheheeeeee
Nakwambia hapo wapemba hawawezi kukujibu jinsi walivyoolewa kwa ndoa ya mkeka na ccm. teh teh teh teh teh sasa hivi wasikilize wanavyojidai kwamba Zanzibar kuna amani. Iko wapi? kwa sababu rais na makamu wake wa kwanza ni wapemba. teh eh teh teh tehDuh!kaka nyi wapemba mmeshtuka sasa.
unajua kiuchumi mlikua juu kipindi tunaungana lakini sasa poleni.
ata ivyo muungano kwa wapemba ulikua na maana kwa wakati ule sio sasa kwani ulikua unatuliza hali ya amani kwa kua serekali iliyokuwepo ni ya mapinduzi so kama tusingekuja sisi watanganyika ambao kwa sasa hatulitaki hilo jina mngekue mpaka leo mnapinduana tu.
wapemba jipangeni tu na sisi tutaamka awa mafisadi kwetu wanakunyimeni hata hata haki zenu za msingi, hata rais wenu mafisadi ndi wanaamua nani awe rais wa wapemba?
lakini na nyie nani hasa alofanya kosa la kuunganisha chama?
unajua makonda ndo lugha zao za siku zote tumewazoea, so hata wakipata elimu awawezi kubadilika kwani nao wako kazini wanahitaji kujaza abiria wengi ili waweze kupata kipato
kuamsha (concietization) watu kuweza kujielewa wao wenyewe na kuwaelewa wenzao na hata taifa kwa ujumla ni mchakato (process). Hivyo, hakuna aliyelaniwa, ila watanzania wako kwenye mchakato wa kuelimika kutoka kwenye wimbi la mgando wa kifikra-unaoona uduni na umaskini wa watanzania kuwa ni mpango wa mungu. Watanzania wanazidi kuelevuka kuona kuwa mstakabari wa maendeleo yao unaletwa na jitihada za wao wenyewe (watu), ardhi au rasilimali nchi, na uongozi bora (siyo mapenzi ya Mungu). Hivyo tunatoka kwenye kuamini kuwa kila kitu ni mapenzi ya mungu-kuelekea kwenye-jitihada za watu, uongozi na rasilimali zilizopo. kadri tuelekeapo huko, ndo utaona watu wanazidi kuona ukweli wa DOWANS, Richmond, EPA, MEREMETA, TANGOLD, SHERATON/KEMPESKY ect. katika harakati zao za kulikomboa Taifa kutoka kwa wazungu weusi
Tulikuwa kwenye Basi lililo jazana hata pa kupumua hakuna konda anapanga watu kwa kuwasukuma kama ng'ombe kituo kilicho fuata konda anaongeza abiria kwa madai kuwa gari haijai kinachojaa ni ndoo ya maji Mwana nyii vipi î£ýù@ö
Kama sivyo kakodi taxi huku tupo kwenye foleni kubwa tukivuja jasho wote ndani ya basi tuliridhika na hali hiyo
Tulipo shuka mama mmoja akanikabili akasema Tanganyika tumelaaniwa na hizi alama/dalili si zake bali za M/MUNGU Akasema;
1-MUNGU atakutia woga hata ukiona unyasi utafikiri ni nyoka utatoka mbio.
2-Kondoo wako atachukuliwa kuchinjwa na kuliwa machoni kwako wewe hutii neno
3-Utaoa wewe mkeo atachukuliwa na wengine
4-Utajenga wewe wataishi wageni wewe hutakaa humo
5-Kutakuwa na mafarakano kama Babeli lete maji utapeleka moto lete mwiko utapeleka kalai jambo dogo utaliona kubwa utahaha jambo kubwa utalipuuza!
6-Kila kitu utasema nitafanya kesho na kutumainishwa upepo!
KWELI TUMELAANIWA?
KAMA KWELI TUFANYE NINI?
KAMA SIO KWELI TUMEJIKWAA WAPI?
KARIBUNI JAMVI HILOO!