Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
Nani adui wa CCM? CHADEMA au ufisadi?
Source: Msomaji Raia
Raia Mwema - Nani adui wa CCM? CHADEMA au ufisadi?
Toleo la 271
5 Dec 2012
HALI ya kisiasa nchini imetawaliwa na mijadala juu ya vyama viwili. Chama cha Mapinduzi (CCM) kinajitahidi kuuaminisha umma wa Watanzania kuwa adui wake mkuu ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Na kwamba, adui wa CCM ni adui wa Watanzania wote.
Kwa hiyo, kwa kuwa CHADEMA ni adui wa CCM, basi ni adui wa Watanzania wote. CCM inadai kuwa uadui wa CHADEMA kwa CCM unatokana na madai ya CHADEMA kuwa CCM hakijafanya kitu na kimedumaza maendeleo.
Kwa hiyo CCM kinawataka Watanzania waipuuze CHADEMA na waichukie kwa sababu inachochea vurugu kwa kusema uongo. Ukihudhuria mikutano ya ndani na ya wazi ya CCM, utasikia na kuona kuwa CCM inaamini kwa dhati kuwa adui wake namba moja ni CHADEMA.
Nyaraka za siri za chama zimejaa malalamiko na tahadhari kubwa juu ya hatari inayotokana na uchochezi wa CHADEMA. Viongozi wakuu wa serikali wameaminishwa hivyo na wao wakajiunga na wimbo huu unaofunika ukweli na hali halisi.
Baadhi ya makada wachache waliodiriki kuona na kuamua kwenda kinyume na mtizamo huu, wameonywa na kuchongewa ndani ya vikao. Wamesingiziwa kuwa ni mawakala wa CHADEMA na kuwa kama wamechoka kuwa ndani ya CCM, waondoke na kwenda huko CHADEMA ili wapambane na CCM wakiwa wa nje ya chama.
Maonyo haya, ndiyo kiini cha ukimya unaoelekea kutawala kutoka kwenye kambi ya waliowahi kujiita makamanda wa kupambana na ufisadi ndani ya CCM. Mtizamo wao kuwa CHADEMA siyo adui wa CCM bali ufisadi ndio adui wa CCM, haukubaliki kirahisi ndani ya CCM.
Wakati CCM wakishikilia msimamo huo, CHADEMA wanasema waziwazi kuwa adui yao namba moja ni CCM. Na kwamba adui wa CHADEMA ni adui wa maendeleo ya Watanzania wote.
Hata kama Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alituaminisha kuwa adui wetu wakubwa ni watatu yaani ujinga, umasikini na maradhi, lakini CHADEMA wanasema haya matatu maana yake ni CCM.
Kwamba ukizungumzia umasikini, unamaanisha CCM, ukizungumzia ujinga, unamaanisha CCM na ukizungumzia maradhi unamaanisha CCM. Wanahitimisha na kusisitiza kuwa nyenzo kuu ya kutekeleza hayo matatu ni ufisadi uliokithiri kila kona ya nchi.
Kwa maana nyingine, CHADEMA wanasema, ufisadi ndiye adui mkuu wa maendeleo ya nchi hii, na ufisadi huo ni CCM. Hii ndiyo sababu CHADEMA wanadai kuwa ukiuchukia ufisadi, umeichukia CCM na ukiichukia CCM umeuchukia ufisadi. Ujumla wa mahesabu ya hoja hii ni kuwa CCM ni sawasawa na ufisadi na ufisadi ni sawasawa na CCM.
Kwa nyakati fulani siku za karibuni CCM ilijikuta pia inaimba wimbo huu wa kupinga ufisadi bila kujua kuwa inajipinga yenyewe. Baadhi ya viongozi wake walipoamua kuwashikia bangowenzao ndani ya chama kwa kuwaita mafisadi lakini bila kuwachukulia hatua, waliisaidia sana CHADEMA kwa kuinadi sera yake ya kupinga ufisadi.
Kwa kuwa baadaye wameshituka na kuuacha huo wimbo, CCM ni kama imeamua kufa na ufisadi kwa sababu kuupinga ni kujipinga yenyewe.
Kwa ukimya huu wa CCM dhidi ya ufisadi, CCM imetangaza kuwa adui wake si ufisadi bali ni CHADEMA. Ni kosa la kimkakati ambalo kwa kawaida hufanywa na watu wenye tabia ya kutenda na baadaye kufikiri badala ya kufikiri na baadaye kutenda.
Urafiki wa CCM na ufisadi una mifano mingi sana ya wazi. Kwa takribani miaka sita sasa, CHADEMA imekuwa na kazi kubwa ya kupiga kelele kila inapobaini ufisadi. Na kazi ya CCM imekuwa ni kuunda tume. Matokeo ya tume hizo yamekuwa ama na kuficha zaidi ushahidi au kuzuia utekelezaji wa matokeo ya tume hizo.
Orodha ya tume hizo bungeni na nje ya Bunge ni nyingi sana. Kimsingi kutokutekeleza maazimio ya tume iliyochunguza ufisadi wa aina yoyote, ni kutangaza wazi kuwa kuna unasaba kati ya CCM na ufisadi huo. Tuchukue mifano michache:
Tume iliyochunguza Kashfa ya Richmond iliibua mambo mengi na orodha ndefu ya watendaji waliopaswa kuchukuliwa hatua. Lakini baada ya kumwondoa aloyekuwa waziri mkuu, waliobaki waliachwa na hata wengine kufikia wakati wa kustaafu na kuondoka kwa heshima.
Maazimio 23 ya Bunge kuhusiana na sakata hilo yalipigwa danadana kila kikao cha Bunge na mpaka sasa hata Spika mwenyewe hajui utekelezaji wa maazimio hayo uko hatua gani.
Mmoja wa watu muhimu katika serikali amesema, baada ya kumwondoa mlengwa mmoja, hapakuwa na haja ya kuendelea, vinginevyo tungegusa mahali pa hatari.
Kwangu mimi, mahali pa hatari ni kwenye kiini cha urafiki kati ya CCM na ufisadi.
Kamati ya Bunge iliyochunguza sakata la David Jairo; yule katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, ilibaini maovu mengi na kupendekeza hatua za kuchukuliwa. Mpaka sasa, Spika ameendelea kupiga danadana utekelezaji wa maazimio kwa kisingizio cha kuwa yeye binafsi hajaridhika kana kwamba David Jairo alimkosea yeye binafsi kama Spika!
Wajuzi wa mambo wa siasa za Tanzania, wanaamini kinachofanya maazimio hayo yasitekelezwe ni hofu ya kutibua uhusiano kati ya CCM na ufisadi. Kiongozi mstaafu mmoja amesema, ufisadi katika CCM ni kama tawi ililokaliwa na CCM na kamwe haiwezi kulikata ikawa salama.
Msururu wa tume na kamati ni mrefu sana. Kila suala mojawapo linapoibuliwa au kukumbushwa, inaelezwa kwamba hata Rais huwa anauliza wasaidizi wake, hivi hili bado lipo? Tulilifikisha wapi? Hapo ndipo mkakati mpya huwa unaundwa ili kuisaidia CCM na serikali kupata nafasi zaidi ya kuchelewa kutekeleza.
Tunaweza kujiuliza sakata na kashafa mbalimbali zimefikia wapi? Liko suala la EPA, fedha za stimulus package, Dowans, rushwa bungeni, utoroshaji wa nyara za Taifa, ujangili wa dola, teuzi tata za majaji, mauaji ya raia mikononi mwa polisi, utekaji wa Dk. Ulimboka, kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi, na mengine mengi.
Wakati msururu huu unahusu kashfa zilizo katika ngazi ya Taifa, iko misururu mingine mingi ya kashfa katika ngazi za mikoa, wilaya, kata na vijiji. Hivi sasa ni kawaida kwa wakuu wa wilaya na mikoa kusajili makampuni na kufanya biashara na serikali. Hali hiyo hiyo ni kawaida kwa mawaziri na wateule wengine kumiliki makampuni yanayofanya biashara na wizara wanazoziongoza. Madiwani wanamiliki shule za kata kwa maana ya ni wao wanaopewa tenda za kuzijenga, kuzilisha na hata kuziuzia vitabu.
Wakati haya yanafanyika, TAKUKURU ipo lakini haina uwezo wa kushughulikia kwa sababu ile ile ya kuhofia kutibua uhusiano mzuri kati ya CCM na ufisadi. Anayemteua kamanda mkuu wa TAKUKURU, ndiye anayekalia kiti cha kumteua Mkuu wa Wilaya, Mkoa na hata kupitisha jina la mgombea ubunge!
Mnyororo huu ndicho chanzo cha kulindana na kudumisha uhusiano mwema kati ya ufisadi na CCM. Pale TAKUKURU inapokamata ushahidi wa kutosha kumtia hatiani afisa wa serikali au mwanasiasa, kamanda mkuu wa takukuru sharti ajulishwe kabla ya kupeleka shtaka mahakamani.
Kwa kuwa naye ana kitanzi au kiporo cha kutuhumiwa na Bunge, huwa ni mwangalifu wa kuruhusu kesi iendelee mbele maana itaamsha madudu yanayoweza kuharibu uhusiano mwema kati ya CCM na ufisadi.
Wana CCM wenzangu wanaweza kuibeza simulizi hii na kuibatiza majina mabaya kama ni chuki ya kushindwa uchaguzi, lakini uhusiano mwema kati ya CCM yetu na ufisadi haukisaidii chama na juzi tu kwenye Mkutano Mkuu, nusura ufisadi umwangushe Mwenyekiti kutoka kwenye kiti.
Kwa bahati mbaya, demokrasia inayopatikana katika sanduku la kupigia kura haiwezi kuwa mwamuzi wa kweli katika mnyukano huu. Hii ni kwa sababu, ufisadi umepewa uhuru wa kuamua nani awe kiongozi katika Taifa hili na hata ndani ya CCM. Ni mpaka CCM itakapochukia ufisadi na kuufanya uwe adui namba moja, ndipo tutakapoanza safari yetu ya kuelekea katika maisha bora.