Nani adui wa CCM? CHADEMA au Ufisadi?

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,853
2,000
Nani adui wa CCM? CHADEMA au ufisadi?

Source: Msomaji Raia
Raia Mwema - Nani adui wa CCM? CHADEMA au ufisadi?

Toleo la 271
5 Dec 2012

HALI ya kisiasa nchini imetawaliwa na mijadala juu ya vyama viwili. Chama cha Mapinduzi (CCM) kinajitahidi kuuaminisha umma wa Watanzania kuwa adui wake mkuu ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Na kwamba, adui wa CCM ni adui wa Watanzania wote.

Kwa hiyo, kwa kuwa CHADEMA ni adui wa CCM, basi ni adui wa Watanzania wote. CCM inadai kuwa uadui wa CHADEMA kwa CCM unatokana na madai ya CHADEMA kuwa CCM hakijafanya kitu na kimedumaza maendeleo.

Kwa hiyo CCM kinawataka Watanzania waipuuze CHADEMA na waichukie kwa sababu inachochea vurugu kwa kusema uongo. Ukihudhuria mikutano ya ndani na ya wazi ya CCM, utasikia na kuona kuwa CCM inaamini kwa dhati kuwa adui wake namba moja ni CHADEMA.

Nyaraka za siri za chama zimejaa malalamiko na tahadhari kubwa juu ya hatari inayotokana na uchochezi wa CHADEMA. Viongozi wakuu wa serikali wameaminishwa hivyo na wao wakajiunga na wimbo huu unaofunika ukweli na hali halisi.

Baadhi ya makada wachache waliodiriki kuona na kuamua kwenda kinyume na mtizamo huu, wameonywa na kuchongewa ndani ya vikao. Wamesingiziwa kuwa ni mawakala wa CHADEMA na kuwa kama wamechoka kuwa ndani ya CCM, waondoke na kwenda huko CHADEMA ili “wapambane na CCM” wakiwa wa nje ya chama.

Maonyo haya, ndiyo kiini cha ukimya unaoelekea kutawala kutoka kwenye kambi ya waliowahi kujiita makamanda wa kupambana na ufisadi ndani ya CCM. Mtizamo wao kuwa CHADEMA siyo adui wa CCM bali ufisadi ndio adui wa CCM, haukubaliki kirahisi ndani ya CCM.

Wakati CCM wakishikilia msimamo huo, CHADEMA wanasema waziwazi kuwa adui yao namba moja ni CCM. Na kwamba adui wa CHADEMA ni adui wa maendeleo ya Watanzania wote.

Hata kama Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alituaminisha kuwa adui wetu wakubwa ni watatu yaani ujinga, umasikini na maradhi, lakini CHADEMA wanasema haya matatu maana yake ni CCM.

Kwamba ukizungumzia umasikini, unamaanisha CCM, ukizungumzia ujinga, unamaanisha CCM na ukizungumzia maradhi unamaanisha CCM. Wanahitimisha na kusisitiza kuwa nyenzo kuu ya kutekeleza hayo matatu ni ufisadi uliokithiri kila kona ya nchi.

Kwa maana nyingine, CHADEMA wanasema, ufisadi ndiye adui mkuu wa maendeleo ya nchi hii, na ufisadi huo ni CCM. Hii ndiyo sababu CHADEMA wanadai kuwa ukiuchukia ufisadi, umeichukia CCM na ukiichukia CCM umeuchukia ufisadi. Ujumla wa mahesabu ya hoja hii ni kuwa CCM ni sawasawa na ufisadi na ufisadi ni sawasawa na CCM.

Kwa nyakati fulani siku za karibuni CCM ilijikuta pia inaimba wimbo huu wa kupinga ufisadi bila kujua kuwa inajipinga yenyewe. Baadhi ya viongozi wake walipoamua kuwashikia “bango”wenzao ndani ya chama kwa kuwaita mafisadi lakini bila kuwachukulia hatua, waliisaidia sana CHADEMA kwa kuinadi sera yake ya kupinga ufisadi.

Kwa kuwa baadaye wameshituka na kuuacha huo wimbo, CCM ni kama imeamua kufa na ufisadi kwa sababu kuupinga ni kujipinga yenyewe.

Kwa ukimya huu wa CCM dhidi ya ufisadi, CCM imetangaza kuwa adui wake si ufisadi bali ni CHADEMA. Ni kosa la kimkakati ambalo kwa kawaida hufanywa na watu wenye tabia ya kutenda na baadaye kufikiri badala ya kufikiri na baadaye kutenda.

Urafiki wa CCM na ufisadi una mifano mingi sana ya wazi. Kwa takribani miaka sita sasa, CHADEMA imekuwa na kazi kubwa ya kupiga kelele kila inapobaini ufisadi. Na kazi ya CCM imekuwa ni kuunda tume. Matokeo ya tume hizo yamekuwa ama na kuficha zaidi ushahidi au kuzuia utekelezaji wa matokeo ya tume hizo.

Orodha ya tume hizo bungeni na nje ya Bunge ni nyingi sana. Kimsingi kutokutekeleza maazimio ya tume iliyochunguza ufisadi wa aina yoyote, ni kutangaza wazi kuwa kuna unasaba kati ya CCM na ufisadi huo. Tuchukue mifano michache:

Tume iliyochunguza Kashfa ya Richmond iliibua mambo mengi na orodha ndefu ya watendaji waliopaswa kuchukuliwa hatua. Lakini baada ya kumwondoa aloyekuwa waziri mkuu, waliobaki waliachwa na hata wengine kufikia wakati wa kustaafu na kuondoka kwa heshima.

Maazimio 23 ya Bunge kuhusiana na sakata hilo yalipigwa danadana kila kikao cha Bunge na mpaka sasa hata Spika mwenyewe hajui utekelezaji wa maazimio hayo uko hatua gani.

Mmoja wa watu muhimu katika serikali amesema, “baada ya kumwondoa mlengwa mmoja, hapakuwa na haja ya kuendelea, vinginevyo tungegusa mahali pa hatari”.

Kwangu mimi, “mahali pa hatari” ni kwenye kiini cha urafiki kati ya CCM na ufisadi.

Kamati ya Bunge iliyochunguza sakata la David Jairo; yule katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, ilibaini maovu mengi na kupendekeza hatua za kuchukuliwa. Mpaka sasa, Spika ameendelea kupiga danadana utekelezaji wa maazimio kwa kisingizio cha kuwa yeye binafsi hajaridhika kana kwamba David Jairo alimkosea yeye binafsi kama Spika!

Wajuzi wa mambo wa siasa za Tanzania, wanaamini kinachofanya maazimio hayo yasitekelezwe ni hofu ya kutibua uhusiano kati ya CCM na ufisadi. Kiongozi mstaafu mmoja amesema, ufisadi katika CCM ni kama tawi ililokaliwa na CCM na kamwe haiwezi kulikata ikawa salama.

Msururu wa tume na kamati ni mrefu sana. Kila suala mojawapo linapoibuliwa au kukumbushwa, inaelezwa kwamba hata Rais huwa anauliza wasaidizi wake, “hivi hili bado lipo? Tulilifikisha wapi?” Hapo ndipo mkakati mpya huwa unaundwa ili kuisaidia CCM na serikali kupata nafasi zaidi ya kuchelewa kutekeleza.

Tunaweza kujiuliza sakata na kashafa mbalimbali zimefikia wapi? Liko suala la EPA, fedha za “stimulus package”, Dowans, rushwa bungeni, utoroshaji wa nyara za Taifa, ujangili wa dola, teuzi tata za majaji, mauaji ya raia mikononi mwa polisi, utekaji wa Dk. Ulimboka, kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi, na mengine mengi.

Wakati msururu huu unahusu kashfa zilizo katika ngazi ya Taifa, iko misururu mingine mingi ya kashfa katika ngazi za mikoa, wilaya, kata na vijiji. Hivi sasa ni kawaida kwa wakuu wa wilaya na mikoa kusajili makampuni na kufanya biashara na serikali. Hali hiyo hiyo ni kawaida kwa mawaziri na wateule wengine kumiliki makampuni yanayofanya biashara na wizara wanazoziongoza. Madiwani wanamiliki shule za kata kwa maana ya ni wao wanaopewa tenda za kuzijenga, kuzilisha na hata kuziuzia vitabu.

Wakati haya yanafanyika, TAKUKURU ipo lakini haina uwezo wa kushughulikia kwa sababu ile ile ya kuhofia kutibua uhusiano mzuri kati ya CCM na ufisadi. Anayemteua kamanda mkuu wa TAKUKURU, ndiye anayekalia kiti cha kumteua Mkuu wa Wilaya, Mkoa na hata kupitisha jina la mgombea ubunge!

Mnyororo huu ndicho chanzo cha kulindana na kudumisha uhusiano mwema kati ya ufisadi na CCM. Pale TAKUKURU inapokamata ushahidi wa kutosha kumtia hatiani afisa wa serikali au mwanasiasa, kamanda mkuu wa takukuru sharti ajulishwe kabla ya kupeleka shtaka mahakamani.

Kwa kuwa naye ana kitanzi au kiporo cha kutuhumiwa na Bunge, huwa ni mwangalifu wa kuruhusu kesi iendelee mbele maana itaamsha madudu yanayoweza kuharibu uhusiano mwema kati ya CCM na ufisadi.

Wana CCM wenzangu wanaweza kuibeza simulizi hii na kuibatiza majina mabaya kama “ni chuki ya kushindwa uchaguzi”, lakini uhusiano mwema kati ya CCM yetu na ufisadi haukisaidii chama na juzi tu kwenye Mkutano Mkuu, nusura ufisadi umwangushe Mwenyekiti kutoka kwenye kiti.

Kwa bahati mbaya, demokrasia inayopatikana katika sanduku la kupigia kura haiwezi kuwa mwamuzi wa kweli katika mnyukano huu. Hii ni kwa sababu, ufisadi umepewa uhuru wa kuamua nani awe kiongozi katika Taifa hili na hata ndani ya CCM. Ni mpaka CCM itakapochukia ufisadi na kuufanya uwe adui namba moja, ndipo tutakapoanza safari yetu ya kuelekea katika maisha bora.
 

Kichuli

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
320
0
Adui wa ccm ni cdm maana yenye inapinga kila jema lilofanywa serikali ya ccm anaye pinga maendeleo yako ndiye adui yako namba moja.
 

andate

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
2,652
2,000
siamini ni wewe ume post hii kitu.
Adui mkubwa wa CCM ni Chadema na sio Mafisadi.
Vigogo wa CCM wapo ndani ya ufisadi na ufisadi upo ndani ya vigogo wa CCM, hauwezi kutenganisha .
Dawa ni kuwaondoa hao vigogo wote kitu ambacho hakitatokea leo wala kesho. Labda CCM ipigwe chini kwenye uchaguzi wa rais na wabunge wengi, hapo ndipo CCM wenye moyo wa kujenga nchi watabaki kwenye chama na wale wasiofaa wataondoka kwa sababu hawataona tena maslahi yao binafsi kwenye chama. Wengi wa vigogo hao wanazitumia nguvu za chama tawala kufanya ufisadi.
 

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
1,500
Ni kwa nini CCM wameshindwa mpaka sasa kutenganisha kofia ya uenyekiti na urais? Ni kwa nini kila rais anayeondoka madarakani mara moja hukabidhi kofia ya uenyekiti kwa rais anayeingia hata kabla ya kipindi chake hakijaisha? Haiwezi ikawa ni kwa sababu rais anaweza kutumia madaraka yake kuchota hela serikalini kukifadhili chama au anaweza akawalinda mafisadi wanaochota hela serikalini kwa ajili ya chama? Kama sababu ni hiyo, adui mkubwa wa CCM si ufisadi bali ni CHADEMA.
 

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,919
2,000
Magazeti yetu haya bwana, yaani yanachukua habari hapa jf bila kuweka chanzo kuwa ni jf bali wanasema eti "msomaji wetu"

Niliandika hii mada hapa jf ikiwa na kichwa

"JK na Lowasa ndio maadui wa ushindi wa ccm 2015 na sio Chadema"

Lakini wao wametoa baadhi ya maneno na kuiandika kwenye gazeti lao,

Kweli nimeamini siku JF ikienda likizo na vyombo vyetu vya habari nchini vitaenda likizo!
 

Fukuyama

Senior Member
Mar 15, 2012
121
195
Lakini huoni kama mada yako imeshika kasi? Hii ni changamoto kwako uwe unaandika makala nyinginyingi ili waandishi wa habari wawe wana kopy edit na kupaste kwenye magazeti yao, na baadae dunia nzima inasoma. Shukuru Mungu JF imekupa nafasi na ukautumia uwanja wake vyema.


Magazeti yetu haya bwana, yaani yanachukua habari hapa jf bila kuweka chanzo kuwa ni jf bali wanasema eti "msomaji wetu"

Niliandika hii mada hapa jf ikiwa na kichwa

"JK na Lowasa ndio maadui wa ushindi wa ccm 2015 na sio Chadema"

Lakini wao wametoa baadhi ya maneno na kuiandika kwenye gazeti lao,

Kweli nimeamini siku JF ikienda likizo na vyombo vyetu vya habari nchini vitaenda likizo!
 

Takalani Sesame

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
588
170
Msomaji Raia (au whoever that started this topic) niseme tu umejaribu kulieleza hili suala vizuri. Lakini, adui wa CCM ya sasa sio ufisadi na kwa kweli ni kinyume chake kabisa. Kwa hii CCM ya sasa, ufisadi ni swahiba wake mkubwa na wala sio adui hata kidogo. Na ndio maana any attempt ya kuwagombanisha inakumbana na vizingiti vizito toka ndani ya CCM kwenyewe.

Tungekuwa tuizungumzia ile CCM ya Mwalimu, you would have made your point very clear. However kwa sasa, tuseme tu kuwa CCM na ufisadi wana-coexist vizuri na Chadema ni kama mchonganishi wa hawa maswahiba wawili. Na naweza kwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa uhusiano huu wa CCM na ufisadi ni 'mutually beneficial'.
 

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,919
2,000
Lakini huoni kama mada yako imeshika kasi? Hii ni changamoto kwako uwe unaandika makala nyinginyingi ili waandishi wa habari wawe wana kopy edit na kupaste kwenye magazeti yao, na baadae dunia nzima inasoma. Shukuru Mungu JF imekupa nafasi na ukautumia uwanja wake vyema.

Wakikopi huku jf waseme wazi kuwa chanzo ni jf
 

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,431
2,000
Ccm wote ni vi-nape tu!

Hivi kujadili kadi ya mwana-ccm mfu, isiyolipiwa na mwana-chama mwenyenyewe alikwishahamia chama kingine ni tija kuliko kumkamata Mwizi wa EPA aliyekiri kuiba hela zinazolipwa na jasho la wananchi? Kuna matrix nimechora kama tathmini ya akili ya vi-nape, kila nikiitazama nahisi kama vile ni kweli kuna wanadamu wako katika hatua za mabadiliko ya kuwa wanyama na kurejea maporini! How comes stupid issues are tabled as national agenda?

IssueHatua zilizochukuliwa
Dr. SlaaKumiliki kadi ya ccm isiyolipiwaDr. Slaa amekiri kuwa anamiliki kadi kama ukumbusho bila kuilipia. ccm wanaona umiliki wa kadi hii indo kikwazo cha maendeleo ya Watanzania!
Wezi wa EPA na MafisadiKuiba pesa za ummaWezi wanafahamika na wamekiri ila serikali ya ccm inasema wakiguswa; nchi itayumba
 

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
2,000
Mkuu heshima yako!

Waswahili wana usemi ya kuwa 'Alalaye usimwamshe, ukimwamsha utalala wewe'.

Adui wa ccm ni ccm yenyewe. Hakuna haja hata ya kuwapa dawa wala ushauri nasaha.
Ni uamuzi mzuri sana kuwaacha hivyo walivyo na ndoto zao za 'Alinacha', wabaki na waendelee na viongozi wao wasio na upeo kama wakina Nape.
Waendelee na viongozi wao mafisadi na wahujumu wa nchi yetu kama akina Kinana.
Waendelee na wabunge wao wanaojua kutukana kama wakina 'Kudadeki'.
Waendelee na mawaziri wao ambao hawana hata sifa za kuwa 'monitor' darasani kama Naibu Waziri wa Elimu.
Waendelee na viongozi wao wengi tu wanaoitwa ma-Dr. ambao hawajaandika hata kitabu kimoja cha hadithi za paka na panya.
Waendelee kupiga kelele za nani ana kadi ya ccm na nani hana, kama vile hawajui ya kwamba enzi zetu sisi ilikuwa huwezi kuingia Chuo Kikuu kama wewe si mwanachama wa CCM. Tupo wengi sana tuliingia CCM kwa kulazimishwa. Wengine tumerudisha kadi, lakini hata walio na kadi wengi ni wanachama wafu, na haibadilishi kitu chochote maana kadi isiyolipiwa haikufanyi kuwa mwanachama.

Wamelala... tusiwaamshe!

Movement for Change iendelee na kazi... Mpaka kieleweke!
 

mwankuga

JF-Expert Member
Aug 30, 2010
334
225
CHADEMA NA CCM HEBU TUAMBIENI ADUI YENU NI NANI? Ukimwangalia na kumsikiliza Katibu Mwenezi wa Itikadi CCM,bwana Nape Nnauye,na kwa upande wa Chadema ukiwasikiliza akina Mnyika,Slaa,unaweza kuvutiwa nao,ukaa kitako na kufungua masikio. Katika maongezi yao,utagundua jambo moja tu "Kusambuliana".CCM wanawasema Chadema hasa kwa "mabaya" na wimbo wa Chadema ni "ufisadi" wa CCM na serikali yake.Kifupi CCM na CHADEMA ni "mahasimu","watani wa jadi"kama Simba na Yanga. Hebu nenda mbele kidogo.

Hivi maana ya siasa na vyama vya siasa inaishia hapo kwenye vijembe?Nani anafaidika na hivyo vijembe? Vipi kuhusu ilani,itikadi na falsafa za vyama hivyo,zinaelezwa wapi? Tangu zamani tunaambia adui yetu ni ujinga,njaa na magonjwa,vipi ukweli huu mebadilika?Sasa CCM adui yao mkubwa ni Chadema, nah ii inasemwa wazi,na wanajipanga kukabiliana na Chadema (sio matatizo ya watanzania),na Chadema ni kinyume chake.

Kama vyama hivi havisemi mikakati ya kuwakomboa Watanzania kwenye huu uchumi mbovu (unaendesha kwa nguvu ya Mungu), elimu iliyovurugika,Taifa kukosa maadili, nani atawasemea watanzania Kwa kuwa CCM ni Chama Tawala, wanaweza kujikita zaidi kwenye utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010-2015. Hili litakuwa jibu tosha kwa Watanzania,wala hakutakuwa na umuhimu wa akina Nape kuita waandishi wa habari kutoa ufafanuzi.Chema Chajiuza.

Lakini hata ndugu na rafiki zangu wa Chadema wajifunze.Waonyeshe kwamba wanaweza kuaminiwa na kupewa madaraka.Hoja yao ya ufisadi inavutia sana,ukiwasikiliza,lakini in long-run haitawasaidia. Maana ufisadi ni matokeo tu!Hebu watuambie sera zao mbadala kwenye masuala ya uchumi,siasa,afya,elimu n.k.

Haitoshi tu kusema utatoa elimu bora. Taratibu siasa zetu zinakosa mwelekeo,kwa sababu tunakosa watu wenye mtazamo na mwono wa mbali,ambao wanaweza kuzungumzia masuala ya Taifa kiundani na kiuweledi.Tunachokiona kwa sasa,ni wapiga debe wa siasa kuongezeka.Sera imekuwa kama uwanja wa fujo. Huko tuendako itatupa shida sana. Kama ujinga,magonjwa na njaa,sio maadui wetu wakumbwa,hebu tuambieni ukweli huu umebadilika? Je, adui yenu ni nani?
 

mwankuga

JF-Expert Member
Aug 30, 2010
334
225
CHADEMA NA CCM

HEBU TUAMBIENI ADUI YENU NI NANI?

Ukimwangalia na kumsikiliza Katibu Mwenezi wa Itikadi CCM,bwana Nape Nnauye,na kwa upande wa Chadema ukiwasikiliza akina Mnyika,Slaa,unaweza kuvutiwa nao,ukaa kitako na kufungua masikio.

Katika maongezi yao,utagundua jambo moja tu “Kusambuliana”.CCM wanawasema Chadema hasa kwa “mabaya” na wimbo wa Chadema ni “ufisadi” wa CCM na serikali yake.Kifupi CCM na CHADEMA ni “mahasimu”,”watani wa jadi”kama Simba na Yanga.

Hebu nenda mbele kidogo.Hivi maana ya siasa na vyama vya siasa inaishia hapo kwenye vijembe?Nani anafaidika na hivyo vijembe?Vipi kuhusu ilani,itikadi na falsafa za vyama hivyo,zinaelezwa wapi?

Tangu zamani tunaambia adui yetu ni ujinga,njaa na magonjwa,vipi ukweli huu mebadilika?Sasa CCM adui yao mkubwa ni Chadema,nah ii inasemwa wazi,na wanajipanga kukabiliana na Chadema (sio matatizo ya watanzania),na Chadema ni kinyume chake.Kama vyama hivi havisemi mikakati ya kuwakomboa Watanzania kwenye huu uchumi mbovu (unaendesha kwa nguvu ya Mungu),elimu iliyovurugika,Taifa kukosa maadili,nani atawasemea watanzania

Kwa kuwa CCM ni Chama Tawala,wanaweza kujikita zaidi kwenye utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010-2015.Hili litakuwa jibu tosha kwa Watanzania,wala hakutakuwa na umuhimu wa akina Nape kuita waandishi wa habari kutoa ufafanuzi.Chema Chajiuza.

Lakini hata ndugu na rafiki zangu wa Chadema wajifunze.Waonyeshe kwamba wanaweza kuaminiwa na kupewa madaraka.Hoja yao ya ufisadi inavutia sana,ukiwasikiliza,lakini in long-run haitawasaidia.Maana ufisadi ni matokeo tu!Hebu watuambie sera zao mbadala kwenye masuala ya uchumi,siasa,afya,elimu n.k.Haitoshi tu kusema utatoa elimu bora.

Taratibu siasa zetu zinakosa mwelekeo,kwa sababu tunakosa watu wenye mtazamo na mwono wa mbali,ambao wanaweza kuzungumzia masuala ya Taifa kiundani na kiuweledi.Tunachokiona kwa sasa,ni wapiga debe wa siasa kuongezeka.Sera imekuwa kama uwanja wa fujo.Huko tuendako itatupa shida sana.

Kama ujinga,magonjwa na njaa,sio maadui wetu wakumbwa,hebu tuambieni ukweli huu umebadilika?Je,adui yenu ni nani?
 

bily

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
8,032
2,000
Ccm ni adui wa watz wote kwani wamepandisha bei za vitu kiholela watt wa maskini wamekua na tabu awasomi mwisho wa elimu yao ni kidato cha 4, akinana mama wajazito wanakufa kila wakikaribia kujifungua akika ccm is aghost , mafuta hayapatkani kwa urahisi cyo ya taa wa petrol wala ya kula yote bei juu yote hayo ni results of ccm ,jiulize kama mafuta yanachakachuliwa masaki jiulize uko namtumbo, tandaimba, shirati, hali ikoje na yote ni kwa ajili ya ccm kwaio chadema iz brainstorming for tanzanians who are fed up with lumumba fm.
 

mzalendokweli

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
579
250
Vijembe vya CDM kwa mafisad vina maslah kwa raia mana bila wao ufisad mwingi tusingeujua tunajua uvundo mwingi sabab ya CDM. Vijembe vya CCM kwa CDM vina maslah pia kwa CDM mana vinawaweka kwe mstar.

Hata hvyo njia nzur ya CCM kurespond vijembe ni kuwafanyia wananchi maendeleo ya kweli sio ya kupromote kwe vyombo vya habar na maendeleo ya takwim hayo hayana maslah kwetu, pia iwachukulie hatua mafisad wote kuanzia wa juu kabisa ndio tuje wachini
 

mnyinda

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
277
0
Juzi wakati wa mapokezi ya Lema mjumbe mmoja wa CHADEMA toka mwanza alisema ninashangaa CCM wanatumia nguvu nyingi kupigana CHADEMA na huku adui wao akiwa ni CCM wenyewe alidai kuwa CCM wangegudua alama za nyakati kwasasa wangetatua matatizo ya watanzania.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom