🤣🤣🤣🥴Unamaanisha kufungua media station ni rahisi kama kukunua kiwanja mabwepande?
Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
We unafuatilia kweli muziki ? Au shabiki WA diamond tuMnadhan kuanzisha media ni kama kwenye kunya chooni? Wenye pesa na ushawishi mkubwa hizo media zao tu zimewahenyesha na bado wana hisa chache katika umiliki wa hizo media.
Tabia ya kichawi na kishirikina mliyojifunza huko Clouds mnataka kuwaambukiza na wasanii wengine ili mlete uhasama na chuki za kijinga.
Wasanii wenu hao mnaoona wamekua ni bora muwashauri watafute management bora ili wazidi kusonga mbele na sio kuanzisha medias au lebo za muziki ambazo nazo wanashindwa kuziendesha zinaishia kujifia, wapi King music label? Wapi konde music kabel? Wapi Next level music label? Takataka zote zishajifia,
Tatizo la wasanii wa Bongo sio media wala makundi ya muziki, bali Usimamizi mzuri na wenye Sheria kali zinazowafanya wasanii wawe na adabu ktk tasnia ya muziki, nje na hapo hakuna la maana.
Acha kumdanganya mtoto wa watu akaishia kula hasara. Mondi aliwekeza kwenye social media ndo katobolea huko so hata hizo media hakuna zilichomsaidia zaidi ya kutaka kumpoteza, na hata sasa hazitegemei kwa lolote zaidi ya wao tu kuanza kujipendekeza baada ya kumshindwa. Nandy dada jichanganye uoneNikimuangalia Nandy namuona kama mwanangu kwa umri wake. Ni msanii mwenye kipaji kikubwa sana na pia ndiye msanii pekee wa kike nchini mwenye Personality nzuri sana.
Ninatamani kuona siku moja akijikomboa kwa kuanzisha media station yake NA HAKIKA INGEBAMBA SANA kuliko Wasafi media.
Nimeshauri hivyo baada ya kuona jinsi Mond alivyofanikiwa hasa baada ya kuanzisha media stn yake. Mond kabla ya kuwa na media yake ilionekana kuminywa na kubaniwa sana na media kongwe hasa Cloud media enzi za Ruge.
Kwasasahivi Mond ana nguvu kubwa sana na ushawishi hata kwa media station zingine kwasababu wanaogopa kumbania wakijua anaweza kuwaajiri kwenye media zao. Wanahabari hawataki yawakute ya Mpoki ambaye alikuwa anamponda Mondi na kumkuza Harmonize.
Japo kwasasa naye Mond ameshageuka na kuwafanyia zengwe wasanii wenzake ili kubaniwa wasichanue kabisa, anatumia nguvu za chombo chake na hata alishalalamikiwa kuwahonga presenters wa media station zingine.
Ukombozi pekee ni kuanzisha media station na hapo ndipo itakuwa mwisho wa zengwe.
Ali Kiba na Harmonize ni wasanii wakubwa sana lakini ndio hivyo sio rahisi kupambana na Mond mwenye kituo cha radio na luninga na hii imemsaidia kumuongezea status Serikalini na kuchukuliwa kama mdau mkubwa wa vyombo vya habari.
Nandy wake up please
Ubunifu zero kabisaKuigana kwingi Africa, ndio mana hatufanikiwi [emoji23][emoji23][emoji23]