Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,886
- 938
MHE. NANCY NYALUSI AFANYA ZIARA YA KIKAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOLO - IRINGA
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Mhe. Nancy Nyalusi amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya Kilolo mkoani Iringa katika kijiji cha Ng'uruwe ambapo amachangia Shilingi Milioni 1 kwenye ujenzi matundu ya choo kwenye Shule ya Msingi Masege kama sehemu ya mkakati wake kusaidia juhudi za Serikali kuweka mazingira mazuri kwenye maeneo ya kujifunzia kama shule.
Ziara hiyo ni muendelezo wa Mbunge huyo kwenye maeneo mbalimbali mkoani Iringa ikiwa ni utekelezaji shughuli zake za kibunge.
"Nimekuja hapa wilayani Kilolo katika eneo hili na kwenye shule hii kujionea mwenyewe ni kwa jinsi gani nami kama Mbunge naweza kuwa na mchango katika kuboresha mambo hatimaye sote tukawa kwenye mazingira mazuri" - Mhe. Nancy Nyalusi alisema.
Katika hatua nyingine Mbunge huyo amewahimiza vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kuacha kubweteka na badala yake kuchangamkia fursa za mikopo ambazo Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeziweka kupitia mikopo inayopatikana kwenye Halmashauri zote nchini.
"Jamani Serikali yetu imeweka mikakati mizuri sana kusaidia makundi haya ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kupitia mikopo ya Halmashauri zetu, Rais wetu anatupenda sana tusiache bahati hii ndugu zangu" - Alisisitiza Mhe. Nyalusi.
#KaziIendelee
#CCMIringa