Mara nyingi hizo ni kauli za kujipa moyo haswa pale unapogundua kuna wanawake fulani utabaki kuwasikia na kuwaona kwenye medias tu..
Kama unataka asiyekunya kanunue dolls..
Mkuu,
Si kila mwanamme ana udhaifu wa kutaka wanawake wengi, wanawake wazuri wote.
Kuna wanaume wamejisoma, wamejielewa na wamejua kuwa huo ni udhaifu. Wameona kuwa wanaume wanapata matatizo mengi kwa kutoweza kushinda tamaa zao za wanawake.
Wameushinda udhaifu huo.
Sasa wewe unaongelea kitu ambacho wengine wanakiona kama udhaifu kama kitu kizuri.
Hatuwezi kuelewana kwa sababu hatuna falsafa zinazofanana za maisha.
Mimi najiona naepuka udhaifu wa wanaume wengi. Kwa sababu najiona mimi ni zaidi ya wanaume wengi.
Wewe unaniona najipa moyo.
Halafu sijasema nataka asiyekunya, hiyo tafsiri ni ya mtu mwenye tatizo la kusoma kwa ufahamu, anayefanya logical non sequitur fallacy.
Naweza ku deconstruct hoja nzima ya "demu huyu mzuri balaa" kwa kuonesha wote wana mapungufu, halafu nikawa na wangu mwenye mapungufu yake ambayo nimeyakubali.
Point kubwa hapa ni kwamba beauty is subjective, hakuna kizuri kisicho na kasoro na we are all human and fallible.
Mimi nishacheza na watoto wa kimataifa New York City mpaka sasa nashangaa cha ajabu ni kipi kwa huyo binti, yani hata tukiondoa masuala controversial ya hanyi au anakunya, sawa inawezekana mzuri kwa standards zenu, siwezi kusema ni mbaya, lakini uzuri wa kusumbua mtu mpaka kuanzisha thread maalum mbona sijauona bado? Huyo kuna sehemu nyingi akipita anaonekana average tu.
So, inawezekana hamuijui dunia tu, au inawezekana ana stories nyingine nyingi zilizowafikisha hapo ambazo mimi sizijui.
Labda mmemuona anavyobiduka sehemu sehemu na mimi sijaona kwa hiyo naweza kuwa simuelewi kama nyie 😂😂