Namuogopa dingi, mkali kama pilipili

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,968
Za siku wanajamvi,

leo nakuja na kisa cha Dingi yangu, ni mkali sana, enzi tunakua ukimuona kwa mbali tu unatafuta pa kutokea, unafurahia zaidi kutokuonana naye kwa kuwa ukionana naye tu lazima utakuwa na hatia ya kujibu, hivyo dawa ni kukwepana hadi akutafute yeye. Kwa sasa mimi ni mtu mzima, nina maisha yangu lakini bado namuogopa sana, siyo mimi tu bali hata ndugu zangu, tumekuwa tukipanga mambo mengi ya kuongea naye na yote yanaishia hewani na mkifanikiwa kwenda kumuona mkifika tu getini kwake mnaanza kupungua na hatimaye mnasmbaratika hata kabla ya kuonana naye.

Siku moja tukachukuana na ndugu zangu ili tukampatie ushauri, wengi wetu tukiwa na miaka zaidi ya 30 na wengine wamegonga 40, tukafanikiwa kuingia getini, akatukaribisha viti, tukasema tunahitaji kuongea naye, ile kuanza tu kuongea mmoja wetu, yakawa ni mawazo tofauti na yeye, hakutaka amalize akamkatisha na kuanza kushusha maneno mazito, mimi nikasema naenda kukojoa nikaunganisha huko huko, ndugu zangu nasikia walitoka pale hawaioni vizuri njia, wanatembea utadhani njia imejaa makorongo. Kifupi kila tukipanga kwenda kumshauri mambo mbalimbali yakiwemo ya namna bora ya kuendesha shughuri zake, tumekuwa tukiishia tu kupanga.

Mwisho nimpongeze Dingi yangu kwa kuwa na uwezo wa namna hii, kwa kweli hiki ni kipaji na ni power kubwa, wachache wana uwezo huu hasa ukizingatia watoto wake wengi tumesoma na kufuzu katika fani mbalimbali, wapo maengeneer, madokta, wanasheria, wahasibu na hata wachumi na wanasiasa, lakini kafanikiwa kutumentain na kutusambaratisha katika kila mkakati wa kumwingia, tumebaki waangaliaji tu.

Je wazee wa aina hii unawaingiaje, maana kinachoniuma kuna mambo mengi hayafanyi kisomi na hivyo sisi watoto kuonekana kama wapuuzi na jamii maana mnaonekana kama hammsaidii baba yenu?.
 
Ha ha ha ha ha ha ha, umenigusa na kunichekesha sana.
Nitarudi baadae. Ule ni u-mafia na utycoon (wana msemo wao-maskio ya binadamu huwa hayazidi kichwa), ubabe hadi 80's.
 
huyo mzee mtumieni mama yenu kumshauri ..... mama anaweza kuongea nae hata wakiwa chumbani au ni mkali mpaka chumbani?
 
huyo mzee mtumieni mama yenu kumshauri ..... mama anaweza kuongea nae hata wakiwa chumbani au ni mkali mpaka chumbani?

Chumbani unakuta bonge la zuzu

Nje sasa akiwa anapata moja mbili na jamaa zake kelelele nyiiingi sijuwi mnatumiaga nini?
 
Ha ha ha ha ha ha ha, umenigusa na kunichekesha sana.
Nitarudi baadae. Ule ni u-mafia na utycoon (wana msemo wao-maskio ya binadamu huwa hayazidi kichwa), ubabe hadi 80's.

usikimbie mkuu, nishauri, kwa kweli ana nguvu za ajabu hadi huwa nazitamani na mimi.
 
huyo mzee mtumieni mama yenu kumshauri ..... mama anaweza kuongea nae hata wakiwa chumbani au ni mkali mpaka chumbani?

hata mama hagusi, na yeye ni kama sisi tu dada yangu. Baba yangu ana nguvu aisee, kajaliwa, hiki ni kipaji. Hata wakati mwingine akiwa kwenye mood anawasimulia tu huwa anashuka nondo za hatari, walahi ni profesa.
 
Chumbani unakuta bonge la zuzu

Nje sasa akiwa anapata moja mbili na jamaa zake kelelele nyiiingi sijuwi mnatumiaga nini?

taratibu mkuu, unaweza kuibua ugonvi mwingine, hapa nimekuomba ushauri na si kutukana.
 
hata mama hagusi, na yeye ni kama sisi tu dada yangu. Baba yangu ana nguvu aisee, kajaliwa, hiki ni kipaji. Hata wakati mwingine akiwa kwenye mood anawasimulia tu huwa anashuka nondo za hatari, walahi ni profesa.

pole sana mkuuu aisee kumbe mimi nabahati sana naweza kumjoke ma dady
 
Ninahisi baba yako hizo ni tabia za kurithi toka kwa wazazi wake.
Au alishawahi kufanya kazi kama askari jela,
Jengeni urafiki wa karibu na marafiki zake watumieni kumueleza.
 
kumbuka hapa namuongelea baba yangu, hata kama ana makosa huwezi sema hivi, mapepo unayo wewe kwa kutukana wazazi wako.

Mkuu are u serious? Huyo mfanyieni suprise, kama ni house mjengeeni mkimaliza mpeni funguo, gari zuri (double cabin pick up) mnunulieni muone kama ataleta ukali. Sio mnaenda na kg ya sukari na maneno mengi mnachanganya na kizungu hawezi kuwaelewa
 
akaombewe kwa TB Joshua...ana mapepo huyo

Hakuna haja ya maombia hapa. Huyo baba ndivyo alivyoumbwa na anaamini kuwa anachokifanya ni sahihi na hata hivyo amedhihirisha usahihi wake kwa kiasi kikubwa
 
Huyo dingi noumaa,hivi ikitokea mtoto wake wa kike akapata Mimba kabla ya ndoa itakuwaje?
 
Mkuu are u serious? Huyo mfanyieni suprise, kama ni house mjengeeni mkimaliza mpeni funguo, gari zuri (double cabin pick up) mnunulieni muone kama ataleta ukali. Sio mnaenda na kg ya sukari na maneno mengi mnachanganya na kizungu hawezi kuwaelewa

serious mkuu, tatizo ni kuwa hakuna kitu mtapatia kikamsuprize, ana kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…