Ninamtafuta Anna Dominick, alisoma Ruvu Sekondari na alimaliza kidato cha nne mwaka 1989 akiwa ni binti mwenye akili sana na alipata division one na zawadi ya uandishi wa insha bora nakumbuka kwa World Food Day ya FAO miaka hiyo. Aliiletea shule ya Ruvu Sekondari heshima sana maana ilipata zawadi cash na vifaa vya maabara. Alijiunga na kidato cha tano Kilakala Sekondari, na jeshini Makutopora. Dada huyu yuko wapi na anafanya kazi gani? Sijawahi kumsikia kabisa maana hii ndiyo human resource inatakiwa kwa taifa hili. Alikuwa ni mchaga ila ila sijui ni wa eneo lipi. Rafiki yake wa kike alikuwa anaitwa Zenobia Mtenga , walikuw darasa moja. Tafadhali sana naomba mno mwenye taarifa zake ani PM.